raia_mwema
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 479
- 313
Heshima zenu wakuu!!!
Jamani kama kuna watu ambao siwaelewi ni hawa wanaoendekeza michepuko.
Utakuta mwanaume ana ndoa halali lakini huwachukua binti aliyeko single na kumpangishia kisha kumhudumia. Mzee mtu mzima ana kabinti ka 20's amekapangishia na anakahudumia, mwishowe wanazaa mtoto, hapa utamkuta binti anajidanganya eti wazee hawawapi presha bila kujua kuwa kuna mke halali wa ndoa ambaye anapata presha huko alipo.
Jaribu pia kufikiria future ya huyo mtoto pia, atapataje elimu na huduma nyinginezo za kijamii? Watoto wanaishia kunyanyasika na kuishi maisha ya shida, jiulize utakuwa mchepuko hadi lini? wenzako wanafamilia wewe mchepuko, halafu huku wazee hawanipi presha kwa hiyo siwataki vijana. una tofauti gani na kahaba anayejiuza? Maana na wewe pia unajiuza.
Mwishowe unajikuta ndio single mother unalalamika umetelekezwa. Hautaweza kutambulishwa popote wala hakuna yeyote atakayetambua mahusiano hayo ya nyumba ndogo.
Wewe unayeendekeza kuchepuka labda nikwambie tu mtu mwenye malengo na mipangilio mizuri ya kimaisha haendekezi kuchepuka wala haendeshwi na tamaa za ngono, Tambua kuwa maisha ni zaidi ya ngono. Binti kama unajitambua, unajiheshimu na kujithamini hautayumbishwa na vitamaa vya mali wala kukubali kuwekwa kinyumba na kutumika kingono.
Wanaume wenzangu tupunguze kuendeshwa na tamaa za kimwili. Hautakaa utunukiwe cheti cha kufuzu katika ubingwa wa kuchepuka au ngono. Tufikirie maisha na zaidi kuwa na upendo na wake zetu na watoto zetu zaidi. Chukua muda kujenga upendo na ukaribu na familia kuliko kukimbilia kwa michepuko.
Tusiendekeze zinaaa jamani wakuu
Ni hayo tu naomba kuwasilisha