Huwa sielewi Dr. Boaz na diet yake

berno

Member
Mar 2, 2011
37
30
kwa maelezo yake hapo chini anashauri kuacha vyakula vya wanga kabisa ili kuweka mwili kwenye afya nzuri mimi sijaelewa unawezaje kukwepa vyakula hivyo

haya ndio maelezo yake pia unaweza kumfollow facebook DR. BOAZ MKUMBO
Jamaa Yetu Inatakiwa kuelimishwa, Mwili wa binadamu hauhitaji kiwango kikubwa hivi cha sukari!
Tunaumiza Miili yetu," Linda sana afya yako kulikochochote ulindacho"

Ulaji wa namna hii sio Mzuri hata kidogo, Halafu unakuja kushangaa kwa nini una kitambi? kwa nini una kisukari? Kwa nini una upungufu wa nguvu za kiume? kwa nini tendo la ndoa kwako ni maumivu mwanzo mwisho? Kwa nini una usaulifu? Kwa nini una pumu?

Ndugu yangu magonjwa hayo yote na Mengineye niliyosahau kuyataja yananipa tafisiri ya kwamba "Mwili wako umeonesha dalili y kutoendelea kustahimili vyakula vya namna hii na tiba yke ni kuupumzisha"

Hivyo ushauri ulitakiwa "Acha vinywaji vya sukari,Ugali,wali,chapati,mandazi,keki,chapati,mikate,juisi za matunda" Halafu kula "Nyama ,samaki,mboga za majani,karanga,kuku,mayai,Nazi,parachichi,olive oil,siagi,mboga za majani"

Ukisikia mtu anakwambia "Kula kidogo" Utambue kwamba hakwambii tu ukweli kwamba "Hicho sio salama kwako" Ila mimi nakwambia huna haja ya kula "Kaugali Ngumi yako" wakati sukari imeziidi kwenye damu na wewe ni mgonjwa wa kisukari!

Soma kitabu changu nimejibu hoja "Namna ya kuirudisha afya yako uliyopokonywa na uhujumu wa wanga na sukari jikoni mwako"

Anza maisha mapya mwezi 7 2017 ni katikati ya mwezi,Yatupasa Kuanza Upya na weka malengo ,historia katika maisha yako! Epuka ulaji huu kuanzia Leo!
 
Mh.Ngumu sijaelewa.Mbona hizo ni mboga tu.Kwa leo jioni mimi na familia yangu tule Samaki tu bila hata wali kidogo au ugali.Tuelewesheni wataalamu wa hizi mambo.
 
Back
Top Bottom