EL ELYON
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 1,563
- 1,886
Salamu wakuu
Awali ya yote mimi ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi na ni diwani wa kata fulani na kiongozi wa chama
Huwa najiulza haya maswali lakini sjawahi kupata majibu
1. Hili suala la tozo: Imeonekana wana CCM wenzangu wengi wanalishangilia sana na kufurahia as if wao hawalipi wala haliwagusi na nikiangalia maisha yao na hata ya wale wanaopnga kwa ujumla ni magumu sana hata mlo mmoja ni wa kuunga unga. Je, wanaposhangilia unyonyaji huu wa Serikali huwa wana maana gani?
2. Unyanyasaji wa viongozi wa upinzani: Nalo nimegundua wana CCM linawafurahisha sana yaani mpinzani hata akiuwawa wana ccm wanafurahia sa nabaki najiuliza shida iko wapi kama hivi vyama vya upinzani sisi wana ccm huwa tunasema havipo vilishakufa tunahangaika nao wa nini kwa kutumia jeshi la polisi, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa, TISS.
3. Kuhusu Bunge: Wakati Bunge lina mchanganyiko wa wabunge wachache wa upinzani viongozi wetu walikuwa wanatuaminisha wapinzani ndio wanatuchelewesha. Sasa sasa hivi mpaka madiwani, viongozi wa mitaa, wabunge wote ni CCM lakini kile walichokuwa wanakisema viongozi wetu wa chama na kiserikali kwamba wapinzani wanatuchelewesha mbona sioni jipya au kucheleweshwa ni haya matozo au nini.
Cha ajabu zaidi chama na Serikali wanalazmisha tena uwepo wa wapinzani Bungeni wasio na chama wakati viongozi wetu walikuwa wanatwambia wapinzani ni wacheleweshaji wa maendeleo.
4. Viongozi wetu wa CCM wakati wapinzani wapo bungeni hawa viongozi hawa walikuwa wakienda kwenye majimbo na kata za wapinzani walikuwa wanawaambia wananchi hamna maendeleo maana mmechagua wapinzani lakini cha ajabu majimbo mengi ya chama chetu CCM tokea uhuru yako chini ya CCM lakini ukiangalia hakuna jipya mfano jimbo la Ndugai kule hakuna kitu hata maji tu ni shida.
5. Kila kitu ndiyoooo: Pale bungeni wabunge wetu wao kila kitu ndiyooo hata kama hakina maslahi kwa taifa na wananchi wao ni ndiyooo tu. Mfano wakati wa Kikwete alisema pesa za Escrow ni za binafsi wapinzani wakasema ni za umma cha ajabu wabunge wetu wote wa CCM walisema ni za binafsi ndiyooooo
Akaja Magufuli akasema ni za umma na zirudishwe wabunge wetu wa CCM cha ajabu wote wakasema tena ndiyoooo
JE, TATIZO HUWA NI NINI NDUGU ZANGU NAOMBENI MWENYE MAJIBU YA HAYA.