Huwa nahisi aibu na hatia baada ya kufanya ngono

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
2,972
9,260
Wakuu salamu kwenu wote, kama kichwa cha habari kinavyosema.

Hivi ni kwa nini kwa baadhi ya watu( ikiwemo mimi pia) kuna hali fulani ya kuhisi hatia na huzuni ndani ya nafsi baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Na pia wakati mwingine kuhisi roho fulani ya aibu na uzito imekuvaa ndani yako.

Na hili limepelekea kuwa na mtazamo hasi Sana kuhusu mambo yote yanayohusu ngono, kiasi kwamba sina long standing relationships.

Kama kuna wataalamu wa maswala ya saikolojia au yeyote aliyeweza kukabiliana na hizi changamoto anaweza kunisadia hili nitashukuru.

Karibuni wadau.
 
Hiyo ngono inakuwa umefanya na mtu ambaye humpendi, ulifanya ukiwa na mihemuko mingi. Ukifanya na unayempenda hali hiyo haitokei lakini umebeba 'Dada poa' au Mdada wa kazi n.k lazima usikie hiyo hali
Hapana ndugu
 
Hakuna jipya, swali je, umeoa mkeo ama ni mke wa mtu?
NB; mke wa mtu si lazima awe ameolewa, tafuta mkeo.
 
Dini zinatuambia kwamba,Shetani humtia majaribuni Binadamu ili atende dhambi,Binadamu akisha tenda hiyo dhambi basi shetani/Ibilisi humkimbia Binadamu coz lengo lake linakua limefanikiwa tayari,

So,unapokua na ushawishi wa kufanya zinaa/Ngono unakua unasukumwa na nguvu ya Shetani/Ibilisi ila ukisha maliza kutenda dhambi hiyo basi Ibilisi hukukimbia na wewe ndipo akili zako hukurudia na kutambua kua umemuasi Mungu kwa kutenda dhambi ya kufanya zinaa,

Mkuu unaonekana una imani sana katia misingi ya kumuamini Mungu,so ushauri wangu tafuta Mke wa halali uoe,kua makini sana usije ukaharibu maisha yako yote kwa starehe ya madakika tu,

Good luck.
 
Hofu gani tena ? Unapomaliza unajisikia mwepesi na akili inachangamka! Kwani umebaka? Kuwa na amani, ni starehe Muumba kaiweka kwa kusudi maalumu! Tunamsaidia Mungu katika uumbaji
 
Back
Top Bottom