Huwa mnachukua hatua gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huwa mnachukua hatua gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, Aug 10, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sijajua kama mada kama hii imeshawekwa humu au la. kama bado ni hivi, una rafiki yako, naye ana mwenza, mnapokwa nae anakuwa anawasiliana na mahawara zake kwa uhuru sana hata kukutana nao mkiwa nae. then mnaenda hadi kwa rafiki yako unamuona shemeji yako na kusikitika tu kwa yale anayofanya rafiki yako. hapo ni hatua gani ya kuchukua? kubaki kimya tu au kutafuta namna ya kumweleza shemeji? (hili liko kwa jinsia zote)
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ukiona kitu kama hicho mwonye rafiki yako lakini usiwe ndio kimbelembele kuchonganisha.Utakuja kuonekana mbaya mwisho wa siku.Haya mambo ni magumu sana ndugu yangu!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kuonya tu inatosha?
   
 4. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, mapenzi ya watu yaguse kwa fimbo ya mbali kama unavyogusa nyoka.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  unajua, unapokaa kimya hata wewe huwezi kujua unazungukwa na mtu, hasa ukitegemea enzi hizi za ukimwi. kama usingekuwepo ni bora
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mziwanda anachosema dada WoS ni kweli kabisa, onya kisha hakikisha unakata mguu kama ni rafiki yako na haonyeki jitahidi kujiweka mbali naye kwa sababu siku ya siku akijafichuliwa utaambiwa wewe ndo kuwadi!! USIJARIBU KUMWELEZA SHEMEJIO. Acha ataambiwa na wengine kwani huoni peke yako ndugu yangu na ukumbuke hakuna siri duniani.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nimewaelewa wandugu. ahsanteni
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unatakiwa kuumpa full warning. Huwezi kuwa rafiki yake kama hamsaidiani katika ishu kama hizi. Unatakiwa uumpe warning kwamba aache na amuheshimu mwenzi wake ama sivyo itabidi urafiki wenu ukome au hata kumwambia huyu mwenzi wake. Huu ndo msaada unaoweza kumpa. Akichukia basi, akikubali fresh. Lakini wewe usikubali kuwa mfungwa wa matendo yake. Hadi wewe kuja kuandika hapa, ina maana hupendezwi na tabia yake hata kidogo. So do something about it. Urafiki hauna maana yeyote kama mnashirikiana katika maovu.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nimekupata mzee, ila si mimi peke yangu. na wengine pia wapate huu ujumbe. haipendezi kucheat waziwazi hivyo
   
 10. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kikijalipuka ujue wewe ni accomplice na haman mwizi na accomplice...utakuwa umemsaidia katika kufanya maovu yake and u will be equally guilty...anza kujitoa mapema kwa kumwambia wazi kuwa anvyofanya sio vyema..tell him kuwa huwezi kuendelea na urafiki kama huu. ama nyote mwasaidiana jamani??

  Juzi kwenye klabu moja jamaa mmoja alipigwa vibao na dada mmoja..kisa na maana.. alikuwa nid bestman kwa haruis yake huyo binti na mumewe.kumbe hata heshima hawana wanaleta vimada to the same club mpaka wakafumaniwa.si kasheshe iliyokuwa hapo!! jamaa alitiwa mangumi akalia kama mtoto..huyo dada naye pia yumo!! chunga yasije kufika na wewe!
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mziwanda,usijaribu kabisa kumweleza shemeji yako,kwanza unaweza kuonekana ni mchonganishi maana jamaa anaweza kumlainisha mke wake na maneno matamu halafu wewe ukaonekana unaleta uchonganishi kwenye ndoa ya watu,na kingine mwonye rafiki yako na umweleze wazi kuwa hupendezewi kabisa na hiyo tabia,mpe hasara za kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake na pia jaribu kumwuliza maswali kama ikitokea mke wake akafanya hayo anayofanya yeye atajisikiaje? Na ukiona haelekei katika maonyo uliyompa its better ukaachana nae maana hamna sababu ya kuwa na rafiki mwenye tabia kama hizo.
   
 12. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mziwanda ulishajiita mtu wa watu na sasa unameremeta ukiongeza sifa ya umbeya/uchonganishi mji si utakushinda?
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kuna memba mmoja mgeni alinikoment na kusema huko uswazi kwao mtu wa watu ina maana 'mbaya' so nikaona isiwe tabu. hata hivyo si unaona ninameremeta hapo? halafu hiyo mada nimeleta tu kwani haya mambo yapo. ningetaka kusema ningesema juu kwa juu bila kuja humu jamvini. nadhani ni kwa faida ya wote
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  acheni kudanganyana!mapenzi ya watu wawili usiyaingilie bwana.wewe hujui wamekutana vipi,wana miikataba gani,wana matatizo gani,kwanini uweke kivuli chako?
   
 15. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  mapenzi ya mambo mengi jamani, unaweza peleka neno likakurudia. Unapokuwa na rafiki kama huyo mweleze ukweli na ukeep distance nae hana faida kwako zaidi ya kuendelea kuona fyongo anazocheza.

  Keep distance and sometimes quite sounds better
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kweli hii ni critical! kumbe haya mambo yana siri hivi? naungana na Dr. mkoloni wa Wagosi wa kaya kwenye wimbo wao wa humjui mkeo/mumeo. majirani wanamjua zaidi. msitetee sana huu usiri wajameni maana yaweza kuwa yanawakuta bila kujua. shauri yenu!
   
 17. Violet

  Violet Member

  #17
  Aug 12, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh mapenzi ya watu kuyaingilia, utapatwa na aibu, baadae wewe ndio utaonekana mbaya, kumbe ulitaka kusaidia. Ni kunyamaza tuu , atajua tuu au tayari anajua ila anangangania tuu. Kuna wanawake wale wanaogopa kuwa peke yao
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  katika hali ya kawaida wala nisingeweza kusema chochote, labda angekuwa dada yangu anafanyiwa hivyo si mtu baki tu. ila ninachosema ni kuwa mkeo/mumeo wanamjua wengine kuliko wewe. hii mbaya sana
   
Loading...