Huu wizi wanaofanyiwa watoto wa wakulima hapa SAUT Mwanza haukubaliki

sema neno

Member
Feb 2, 2019
8
45
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine wamekuwa wakishuhudia wizi mkubwa wanaofanyiwa na chuo hiki huku zaidi ya millioni 700 zikiliwa mbele ya macho yao.

Serikali ilianzisha mpango wa wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa na Bima ya Afya kwa lengo zuri na kuwasaidia watoto wa wakulima kuweza kuapata huduma ya afya kwa unafuu kwa taratibu za NHIF ghalama za Bima kwa mwanafunzi ni Tsh 54,000 lakini SAUT wanawaibia hawa watoto wa masikini kwa kuwalipisha 100,000 kwa kila mtu kwa SAUT hii nafasi imekuchukuliwa kama nafasi ya kuwanehemesha baadhi ya wafanyakazi wa chuo hiki mwaka wa masomo 2017/2018 chuo chenye wanafunzi zaidi ya 8000 waliopata kadi za Bima hawakuzidi 1000 na wengine hawakupata huku wakiwa wamelipia kila mtu kiasi cha shilingi laki moja tena kwa lazima hata kwa ambao wanamiliki Bima za wazazi wao sijui huu mpango kama ni lazima au hiari ya mtu mbaya zaidi hata hao waliopata kadi hazikufanya kazi kutokana na kutolipiwa.

Katika mwaka huu wamasomo zoezi limeendelea vile vile watu wana kadi za bima za wazai wao ajabu wanalazimishwa kulipia tena bima huku wale ambao hawakupata mwaka jana wakilazimishwa kulipia tena huku pesa zao za mwaka jana zikiwa hazina majibu kuwa ziko wapi na zilifanya kazi gani?

PENALTY
Hapa pia kwenye penalty kumekuwa na wizi wa makusudi joining instruction ya SAUT inaonesha ulipaji wa Ada ni mara mbili kwa sermister lakini wadogo zetu wamekuwa wakifaniwa ndivyo sivyo Mdogo wangu karipoti chuo mwezi wa pili tu analazimishwa kulipa 911,000 ikipungua hata 100 anapigwa penalty ya laki moja na huu mchezo umekuwa endelevu jamani.

Baraza la Maaskofu sidhani kama alianzisha chuo hiki kuwaumiza watoto wa masikini bali ilikuwa kuwasaidia badala yake imekuwa ni maumivu mtu hana mkopo anajisomesha kwa kuungaunga halafu unampiga penalty huku ukimnyima hata kufanya mtihani.

Madogo wanatazamia kuanza mitihani Jumatatu lakini naambiwa wengi hawajapata kadi za mitihani sababu ikiwa ni penalty huku wengine system lao bovu likiwa linaonyesha wanadaiwa lakini hawadaiwi.

Jamani hebu tuhurumieni tunaosomesha tunaumia acheni hizi mambo.
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
7,515
2,000
Kumbe wewe ndugu mlalamikaji si mwanafunzi wa SAUT sasa ukiambiwa ulete ushahidi wa hilo povu lako utakuwa nao?
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,677
2,000
Wewe unalamimimka laki1 2019 mdogo wangu nilimlipia hiyo 2008. Ila ndivyo insurance ilivyo.
 

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
963
1,000
Badala ya kuungana na kukataa wizi, mko busy mnalialia kwenye mitandao mara WATOTO WA WAKULIMA mara WANYONGE ili muonewe HURUMA.

Wabongo bana, ndio maana huwa MNAKUNJWA SABA kwa kujilizaliza hivi.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,797
2,000
Hahaha kuna vitu vinachekesha, Yani mtu aliyeshindwa kulipa ada ya milioni moja kwa kuchelewa unampiga penalty alipie laki moja zaidi? Sasa wanamuadhibu mlipaji kwa kuamua kwenda chuo? Anyway labda wao wameona hiyo inawasaidia kuwafanya wasomaji walipie ada kama mkataba unavyosema.

Ukweli ni kwamba elimu ni biashara kam duka, Siyo sadaka kama wengi wanavyotaka iwe. Utashangaa waliosomeshwa bure ndio huwa wakwanza kudai mishahara mikubwa na ikichelewa kidogo tu utawaona wameanza kutumiana vimeseji. Labda hao SAUT watawafanya muithamini elimu mnayoilipia.
 

sema neno

Member
Feb 2, 2019
8
45
Kumbe wewe ndugu mlalamikaji si mwanafunzi wa SAUT sasa ukiambiwa ulete ushahidi wa hilo povu lako utakuwa nao?
mzee ukitaka ushahidi ulinza mwanafunzi yeyote anaesoma chuo hiki au somesha saut ndo utajua ninayoyasema mpaka sasa madogo hawana kadi za mtihani na j3 wanaanza mtihani ukiuliza sababu ni za kijinga haijawai tokea
 

hugo jr

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
286
500
wanafunzi wa SAUT kumbe mazuzu, yaani wanajua wanatakiwa walipe 50400 kwa nini walipe hiyo laki? ujinga wao waache waliwe kwanza hiko chuo kinaongoza kwa wanafunzi kupata mimba hovyo hovyo
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,729
2,000
wanafunzi wa SAUT kumbe mazuzu, yaani wanajua wanatakiwa walipe 50400 kwa nini walipe hiyo laki? ujinga wao waache waliwe kwanza hiko chuo kinaongoza kwa wanafunzi kupata mimba hovyo hovyo
Si SAUT peke yake kuhusu bima ya afya hata vyuo vya serikali vingine hili tatizo lipo au lilikuwepo. Waziri analifahamu hili na aliahidi kuliangalia ikiwezekana wanafunzi walipe moja kwa moja.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,754
2,000
Kwani hapo SAUT Hakuna Serikali ya Wanafunzi?

Kama M nashindwa kutetea kitu kidogo Kama hicho mtatetea jambo gani mkimaliza Chuo?

alama Moja wapo ya kudorora Elimu Ni kuzalisha Wasomi waoga wanaoshindwa kutetea Hata haki zao Za msingi Na Za Moja kwa Moja Kama hiyo

Wanafunzi wa Siku hizi Nyoro nyoro Sana
Sie enzi zetu Udsm tukiwasha Moto Nkuruma Hall wanapata Mafua mpaka Ikulu ya Kambarage sio Chancellor!

Jambo dogo Kama Hilo sio la kuomba huruma ya Jamii Sijui TCU Ni nyinyi Wenyewe kukabili Management ya Chuo

Au Siku hizi kazi Za Serikal ya Wanafunzi zinaishia Kwenye Kufuatilia Mikopo Na Kuandaa concert Za Muziki kwenda Kutongozana na Kuuza Kadi Za Vyama vya Siasa?
 

natoka hapa

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
8,499
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom