Huu wizi wa vifaa vya magari bandari ya dar utakwisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu wizi wa vifaa vya magari bandari ya dar utakwisha lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ufunguo, Aug 22, 2012.

 1. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi karibuni niliagiza gari ndogo (980 CC) kutoka Japan kutokana na unafuu wake (mafuta na bei) ili kukidhi mahitaji mbalimbali kulingana na mwenendo wa maisha ya sasa. Pamoja na kwamba serikali iliongeza kodi ya uchakavu kwenye magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 iliyopita, nilijikamua na kulipia gharama zote za ushuru. Cha kushangaza pendekezo hilo kwa sasa limekataliwa na bunge na sijajua utaratibu unakuwaje kwa watanzania ambao wamekumbwa na tatizo hilo la kulipia ushuru ambao haukuwa umepata baraka za bunge. Anyway, tatizo langu la msingi hapa ni kwamba baada ya gari kufika bandarini na kukaa kama wiki moja kabla ya kutolewa, gari ilikutwa imeibiwa control box na power-window. Baada ya kuhoji sana nikapewa document na bandari inayoonesha eti gari ilipokelewa bila control box na power-window wakati vitu vyote hivyo vilikuwepo wakati gari inasafirishwa hadi inafika bandarini Dar. Baada ya kuzama kwa undani zaidi nikagundua kumbe kuna mtandao kamili. Mkaguzi wa bandari anaweza kusema kitu X hakipo katika fomu ya ukaguzi wakati siyo kweli halafu baadae anawaambia vijana wake wakavyofoe vitu hivyo katika gari husika nafikiri kwa ushurikiano na agent. Kibaya zaidi ni kwamba wanafanya unyama huo huku mmiliki wa gari tayari ameshalipia gharama zote za storage ikiwa ni pamoja na faini ya siku zilizozidi. Naamini tatizo hili si langu tu bali watanzania wengi limeshawapata, sasa tufanyeje wadau?. Je watanzania wakianza kupitishia mizigo yao bandari za nchi za jirani kama Kenya walaumiwe?.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu inauma sana hii tabia wabongo na serikali yetu legelege!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hata majumbani siku hizi wanaiba wanaacha gari kama chuma chakavu. Njaa imekithiri mitaani watu wanakuwa wadokozi
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huu udokozi sijui utakwisha lini kwa kweli inaudhi sana,pole sana mkuu
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi walilamba CD changer!
  Hawa nyangau wamezoea sana huo mchezo naona apo Mwakyembe itabidi atusaidie mwenye namba pls ili hii msg aforwdiwe
  Bse atleast imefanywa kwako mtz imagine huwa wanawafanyia ata wacongo such that kuna jamaa aliwaambia uko uko Japan ngoeni power window mtume separately.
  Wajapan walimuuliza why akasema bandarini watazingoa so kheri wazingolee uko uko
  AIBU AIBU
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kuna haja ya kutumia bandari za nchi jirani, maana hii tabia inakera sana
   
 7. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  duh pole ,hatuna amani TZ.
   
 8. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mi jamaa walikomaa wakalegeza nati za propela shaft ya defender yangu pale bandari, yani ningechelewa kidogo tu kuitoa bandarini ningekuta propela shaft ya nyuma imekwenda.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Cha msingi ni kuwafungulia kesi ya madai na kuwadai fidia ya mil100 ili iwe fundisho!
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mkuu pole sana Bandarini ni mahali pa wezi!!, niliingiza RAV4 2010 wakang'oa redio, mwaka huu pick up wakadhani kuna mzigo nyuma, ilikuwa imefunikwa wakavunja lile hard board
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi ni kweli ili Tatizo haliwezi kuwa solved?
  Kwa nini wahusika bandarini wasiwe wanahusika na huo upotevu!
  Haingii akilini eti mtu nasema gari imekuja haina power window au wanazani uko nje kuna vishoka wezi kama apo bandari
  Nilishakiamuliaga gari zangu zote hupitia mombasa maana apa Bandari salama si salama tena
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Gari ikiwa imefika bila hivyo vifaa, inatakiwa isiteremshwe melini kabla ya kujaza fomu za mapungufu baina ya bandari na agent wa meli, ukiiteremsha melini kabla ya kuwajulisha agents, ambao wanatakiwa wawepo wakati magari au mizigo yoyote inateremshwa, inakuwa kosa ni lako uliyeteremsha na umeshapokea huo mzigo ukiwa salama na hapo inatakiwa bandari wakulipe.

  Tanzania ni ubabaishaji na wizi wa huko Barbarian, ni kweli Mwakyembe kwa kuwa hizi bandari zipo chini yake, inatakiwa afanye kazi ya ziada.

  Kinachonishangaza ni haya makundi ya kutetea haki za binaadam na hawa mawaziri vivuli, kwanini huwa hawasimamii kuelimisha raia mambo ya kufanya katika hali kama hizi. Ikiwwa Waziri husika kashindwa basi hata kivuli chake nacho kimeshindwa? na kazi yake ndio hiyo ya kusimamia mapungufu na kuyaainisha? na waziri kivuli si bungeni tu, ni kila siku.
   
 13. R

  Rweza79 JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Utaishaje kama CCM bado ipo madarakani?
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145


  duh!!kweli noma
   
 15. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Wale vijana ambao wanakaa karibu na geti watakuuzia vitu vyako ... Solution ni kushushia mizigo Mombasa. Bei nafuu zaidi, TRA unachagua (Tanga, Kilimanjaro au Musoma).. Bandari la Dar ni mateso tuu... Nimewakoma
   
 16. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kimsingi wamejitahidi tahidi kupunguza naona mkuu bahati mbaya ilikuwa kwako tu. Jamaa yangu kaingiza Verosa bahati mbaya wao ktk ushushaji wakakwangua bumper la mbele walimlipa,waliitunza gari kwa gharama zao wakaagiza bumper lingine hadi limefika ndo ikafungwa na jamaa akakabidhiwa gari
   
Loading...