Huu wizi wa muda wa maongezi ya simu nani atusaidie?

Gosheni

Senior Member
Oct 28, 2008
199
138
Ndugu zangu hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku,nani atatusaidia ili kuepukana na hu wizi tunaoibiwa pesa na makampuni ya simu. kwa ujumla ukiangalia pesa tunatozwa wa muda wa maongezi haviendani kabisa na matumizi halisi kutokana na viwango tulivyo kuwa tukitozwa.

Mimi ninatumia laini mbili za simu ambayo ni tigo na voda.lakini laini yangu kuu kabisa ni tigo,voda huwa naitumia kwa maswala ya mpesa.

Nilivyo kuwa nafahamu,kabla ya july2012 tulikuwa tunalipa 1Tshs/sec, ikiwa na maana ukipiga simu kwa dakika1 itakugharimu 60tshs,hapa kama haujaweka maswala ya kodi,ila ukiweka na kodi na maswala mengine ya makato nategemea dakika1 itanigharimu si zaidi ya 100tshs.hivyo kama dakika tano haitakugharimu zaidi ya 500tshs.

Lakini kitu ambacho nimegundua sasa, 500tshs,ninauwezo wa kuongea dakika2 tuu.

nikafikiri labda haya maongezeko ni kwa sababu ya ongezeko la kodi lilifanyika july kwenye gharama za kupiga simu,lakini ongezeko ni kidogo.

hii hapa ni sehemu ya ongezeko la gharama za simu kutoka kwenye hotuba ya waziri wa fedha.

Kuongeza Ushuru wa bidhaa kwenye muda wa maongezi (airtime) kwenye simu za mkononi kutoka asilimia 10 kwenda asilimia 12. Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa bidhaa unaotozwa kwa huduma hii katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wakati huu ambapo tupo kwenye soko la pamoja.

sasa hapa mimi ninaona kunaongezeko la asilimia mbili tu,lakini makato ni mara2 ya matumizi ya awali.je ongezeko la 2% inamaana ongezeko mara2 ya matumizi?

Kabla nilipo kuwa nikipiga simu nje ya nchi ilinigharimu 1000tshs kwa dakika3,lakini sasa inanigharimu 2000tshs kwa dakika3.hapa ninaona kunaongezeko la mara2,hili nimeliakikisha kwa ukaribu zaidi.

Pia watu wanalalamika,mtu akiweka vocha kama 1000tshs,bila ya kufanya matumizi yoyote anakuta kunaupungufu wa pesa kwenye simu,ambapo anaweza kukuta imebaki kama 940tshs,sasa hizi zingine zimeenda wapi bila ya matumizi?kama sio wizi ni nini?

Juzi nilikutana na rafiki yangu ambaye tulikuwa hatujaonana kama kwa miaka3,kama kawaida kunakupeana historia kwa ufupi moja wapo ni kuhusu kazi.Aliniambia yeye alikuwa ameajiliwa tigo,ila kwa sasa yupo kwenye kampuni lingine,nami nika muuliza kulikoni kutoka tigo na kwenda kwenye hilo kampuni alilopo? Yeye akaniambia,kule tigo alikuwa analipwa kama 1400000tshs,sikumbuki aliniambia ni nini kilichotokea kwenye kampuni la tigo,ila tigo waliamua kupunguza mishahara ya wafanyakazi wao.kwa mfano kama yeye kutoka 1400000tshs hadi 800000tshs,hili likamfanya ahame,na jambo hili halikufanyika kwake tu ila kwa wafanyakazi wote.


Mambo haya yananijia kichwani.
1. Je wizi hu unafanywa na wafanyakazi bila kampuni kujua?
2. ni sera kampuni imeamua kuweka ili kuongeza wigo wa faida?
3. TCRA ina majukumu gani katika kuwalinda raia na wizi wa namna hii?
4. TCRA inataratibu gani wa kuyakagua haya makampuni?
5. Je hili swala la kuibiwa ni mimi peke yangu ndio ninaliona?
kwa kweli ni pesa nyingi wanachukua ukizingatia kama watamuibia kila mtu 200tshs kwa watu 1000000 kwa siku1,ina mana watapata 200,000,000tshs.hizi ni pesa nyingi sana jamani tunaibiwa.na nilizani tatizo hili lipo tigo tu peke yake,kumbe hata voda.

haya ni mambo nafikiria kufanya....

1. nimeona zantel wanafanya matangazo yao, labda wao hawana wizi kama huu,wenye uzoefu na huu mtandao mnisaidie.

2. labda kunamna ya kujiunga na tariff fulani ili kupunguza gharama, kama kuchajiwa kwa sekunde au kwa dakika.

Nina mengi ya kuongea kutokana na wizi huu,lakini naona niishie hapa,ninaomba wote kwa pamoja tuinue sauti zetu kukemea wizi huu.waandishi wa habari,wabunge,na watu wote wenye nafasi za kupaza sauti zao.
 
Hivi mtahama hama hadi lini. Kama watu wanakuibia dawa ni ku-deal nao sio kukimbia na kuwaacha waendelee kuwaibia wengine.
 
Achana na teknolojia ya simu za mkononi, zInaongozwa na jambazi mkuu TCRA. Utalalamika na machozi yako yatakauka, hamia kwenye redio koll ndio mambo yote.
Kwa ishu za pesa za mtandao ndio utumie hiyo m pesa yako
 
Achana na teknolojia ya simu za mkononi, zInaongozwa na jambazi mkuu TCRA. Utalalamika na machozi yako yatakauka, hamia kwenye redio koll ndio mambo yote.
Kwa ishu za pesa za mtandao ndio utumie hiyo m pesa yako

Hahahah....this sound so drunk (and its a 9:45 post)... hahahah
 
Back
Top Bottom