Huu wizi ukiachwa ni zaidi ya ESCROW,huu siyo msimu wa MATESO kwa Watanzania

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
Kila moja anafahamu ni adha gani wanazopata watanzania hasa wakati huu kuelekea mwisho wa mwaka ambapo UFISADI ZOELEFU hufanyika kwa kuwapandishia watanzania nauli kwa makusudi kabisa ili kuwafanyia dhuluma na ujambazi wa wazi wazi.
Mara nyingi makampuni WIZI yamekuwa yakiweka kiwango cha juu cha nauli hasa kwa mabasi ya mikoani na hivyo kuleta usumbufu kwa watanzania.
Huu ni wizi,ujambazi na ufisadi wa wazi ambao wahusika wanafahamu kuwa wanafanya dhuluma kwa watanzania.
Hivyo ni jukumu la viongozi na wanasiasa wetu kulikemea hili kama kweli wanauchungu na wapo kwa ajili ya watanzania.
Iwapo upandaji wa nauli utafanyika,litakuwa ni jukumu la viongozi wetu kupeka HOJA bungeni na kujadili kuwa WIZI NA UJAMBAZI HUU,UNAFANYIKA KWA MASLAHI YA TAIFA AU WATU BINAFSI,na siyo kila siku wananchi kuibiwa.
Ufike wakati sasa,watanzania tuseme BASI-TUMESHACHOKA.
 
Back
Top Bottom