Huu wimbo wa zamani naupenda sana

kuna ule wa mpenz stela jamaa alienda kumpoke mchumba akakuta anarud na mjapan na mtoto.
 
kuna ule wa mpenz stela jamaa alienda kumpoke mchumba akakuta anarud na mjapan na mtoto sijui unaitwaje na aliimba nan! Ila duble duble na vunja mifupa
 
Kuna wimbo sijui unaitwaje na umeimbwa na nani, nasikia tu neno "FATIMATA". Anaeujua umeimbwa na nani?
 
Kuna wimbo sijui unaitwaje na umeimbwa na nani, nasikia tu neno "FATIMATA". Anaeujua umeimbwa na nani?

Hahaha...mgumu huo kuuandika, tusubirie BANA BA KONGOO baelezee maneno ya ngambo hiyo.
 
1. Utakuja nitafutaa...mashariki na magharibiii, utaliaaa...utaliaaa....aaaa....aaaa, usinioneeee!!

2. Nimetuma wakusalimie barua pia nimetuma usomeee.....(malizia)

3. Mwanetu kaza moyo uishi na mumeo..mumeo huyooo...ni wewe mwenyewe uliempenda. Tulikufahamisha mapema, kuwa mchumba wako ni mleviii...hukutaka kutusikiaaa, leo umeyaona mwenyewee, mwanetu eeee....

4. Nyimbo za Monica Seka na Oliver Ngoma nazo unifanya nitulie kidogo mpaka ziishe.
 
SaidAlly,
huo wa kaza moyo uishi na mumeo ni mtamu sana. Barua nimetuma ni mapenzi ya simu sitaweza samba mapangala.
 
FirstLady,
Yaani hizi nyimbo za zamani ni balaa. Hawa jamaa walifaidi sana miaka ile.
 
1. Utakuja nitafutaa...mashariki na magharibiii, utaliaaa...utaliaaa....aaaa....aaaa, usinioneeee!!

2. Nimetuma wakusalimie barua pia nimetuma usomeee.....(malizia)

3. Mwanetu kaza moyo uishi na mumeo..mumeo huyooo...ni wewe mwenyewe uliempenda. Tulikufahamisha mapema, kuwa mchumba wako ni mleviii...hukutaka kutusikiaaa, leo umeyaona mwenyewee, mwanetu eeee....

4. Nyimbo za Monica Seka na Oliver Ngoma nazo unifanya nitulie kidogo mpaka ziishe.

Kaka said.. No 1. Unaitwa Sikujua kama utabadilika, sauti tamu kabisa ya mzee Abeli Kifuto bendi ikiwa inatwa Simba wa nyika.
 
upande wa taarab kuna patricia hilarly, nazipenda sana.

Kuna taarabu nyingine wanaimba

'sina mimi sina mwingine zaidi yako wewe
sina mimi sina atakayekushinda wewe'

'ni bure zenu fitinaaa, si wala hatuzijaliii
wenyewe tumependana, kuachana ni muhali'

hivi naweza pata wapi taarabu za 80's na early 90's. Natamani kupata collection yake lakini wapi.
 
basi ndo huo, nlishasahau hata kaimba nani

kuna mwingine sijui ni wa Hamza kalala

'eng'ombe, jamalwa madundo
nalila masomanda eeeh
eyeyeyeye iyo yeee eyeyeye iyo yeee'

Kongosho...huo ni wa DDC mlimani park, nadhani kaimba pia Cosmas chidumule.
 
una balaa wewe

unanikumbusha, binti mmoja
yalimkuta ya dunia baada ya kufiwa wazazi
huu wimbo ndo ulikuwa hit, miaka hiyo.

Mi nakumbuka nilienda kunywa bar moja huwa inakesha pale K'ndoni(BM?),ila iko kwenye kona kama opp na Open University...

Na siku hiyo ndiyo alikuwa ametoka kuagwa pale Biafra(Remmy)... Sasa katika show zilizokuwepo,kuna jamaa waliigiza kama Remmy katika wimbo huo wa Kifo..

Sasa tatizo lilikuwa wameandaa mdoli mkubwa wakamfungafunga kama marehemu asiyekuwa na jeneza.. Wakamlaza mbele... Waimbaji wakawa wanaigiza wimbo kwa vitendo.. "kifoo kifooo kifoo ee kifo hakina hurumaaa..."

Wateja walikuja juu sana.. " imbeni tu ila toeni sanamu hilooo" jamaa wakawa wanaendelea kuimba tu...
Baadaye walevi wengi wakazidi kulalamika.. Toa sanamuu... Toa sanamuu
mimi nilicheka sana...
 
kuna ule wa mpenz stela jamaa alienda kumpoke mchumba akakuta anarud na mjapan na mtoto sijui unaitwaje na aliimba nan! Ila duble duble na vunja mifupa

Hii imenikumbusha wimbo mmoja jamaa alimtongoza dada mmoja wakaelewana kesho yake aende nyumbani anakoishi yule dada.

Hiyo siku iliyofuata jamaa alipokwenda,alimkuta yule dada KAFA!!

Mwenye kumbukumbu na huu wimbo,tukumbushane..
 
Habari za wkend,

Jamani kuna huu wimbo unaitwa AFRO wa les Wanyika mwenzenu unanichanganya sana. Kila niusikiapo natamani ninyanuke nicheze.

Na nyie wenzangu nyimbo gani ya zamani inawagusa?

Mwanameka wa Marijani rajabu nomaa.. yani mtoto alivomtega Mussa mpk akaingia line, unanikumbusha Hawa alivomtega Adam kuleee Eden bustanini. halafu 'Cassanova' wa LeVert aaah mi HOI..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom