Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 7,913
- 13,373
Wasalamu .
Sina maongezi mengi sana juu ya hili kwa sababu maongezi yangu kwa upana wake yataitaji ufafanuzi mrefu ambao sipo tayari kuuweka kama sehemu ua uzi huu labda kama 'comment' ndogo ndogo.
Huu wimbo unatokana na wimbo wa 'Kwangaru' ulioimbwa na wasanii Diamond na Harmonize, kiukweli bado nawaza hatima ya taifa letu hasa kimaendeleo kama tunahamasishana kwa nyimbo kama kwangaru remix.
Sanaa ya nyimbo imefanya vizuri sana kwenye kuhamasisha hapa nchini ila ilipofikia sasa haihamasishi ujenzi wa taifa imara tena, badala yake tunachukulia kujenga taifa imara kama kitu cha mchezo mchezo.
Huu wimbo Kwangaru remix hauwezi fananisha na wimbo kama 'Alisema Mwalimu' ule orijino sio huu wa kijana Ney wa Mitego.
Hakuna taifa linatumia nyimbo za kucheza cheza katika kuhamasisha shughuli ka kujenga/kukomboa taifa, hili jambo ni Tz tu limeanza kushika kasi.
Pia bado sijajua huu wimbo nausikia hadi kwenye vituo vya redio, nayliza huu ni wimbo wa kampeni, kusifia au kuhamasisha?, je hatujaanza kampeni kabla ya muda?.
Sijaweza pangilia hoja yangu hii japo ni nzuri sababu kiukweli ninashangazwa na kushindwa kujua tunaelekea wapi kama taifa, ni wapi tunawapeleka vijana wetu.
Mimi ningekuwa ni raisi Magufuli huu wimbo ningekataza kupigwa na ningewatuma basata waufungie kabisa pengine ingesaidia kufanya watumishi na watendaji kuchapa kazi na si kunisifia sifia na kujipendekeza kiuongo uongo tu.
NB: mnivumilie sijapangilia hoja yangu
Shukrani.