Huu uzuzu wa kudhani kila kitu kutoka nje ni kizuri utatuisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu uzuzu wa kudhani kila kitu kutoka nje ni kizuri utatuisha lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Oct 13, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakika jamii yetu inashangaza,si mkubwa wala mdogo kila kitu kutoka Marekani au Ulaya ndicho cha kuigwa.Tumeiga hata visivyoigwa.Mabinti zetu sasa wanatembea uchi kwa visingizio vya kwenda na wakati.Lundenga nae mabinti zetu anawafolenisha uchi huku wazazi tunachekelea!Makampuni ya simu nayo hayako nyuma, matangazo yao ya watu wajirushe,yana hamasisha kutenda dhambi wazi wazi,hata bila aibu na watu tunachekelea.Matangazo yanayo hamasisha ngono yako kila mahali lakini hatuonekani kustuka.Kondom zilipoingia hata kutamka neno kondom watu tulikuwa tunaona aibu.Neno hilo lina ukakasi,halifai kwa kuwa linapiga picha mambo ya sirini.Katika hali isiyo ya kawaida makampuni haya ambayo yanamilikiwa na mitandao ya kishetani,yametumia utaalam walio nao katika kufahamu jinsi ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi kuwakilisha ujumbe wao.Na hakika jumbe zao ikiwa pamoja na za kondom zimekubalika.Watu hatuhoji tena kuhusu jumbe zao nyingi ambazo zina utata kupindukia.Matatizo hayaishii hapo.Tumeingizwa mkenge hata katika mikataba mingi ya kimataifa.Si siri tena kwamba katika hali isiyo ya kawaida kabisa tumetoa rasilimali zetu bure kwa hawa wahuni,wenzetu wamechukua alimasi,sisi wametuachiwa chupa.Tumeingizwa mkenge kwa hali hiyo hiyo katika ubinafsishaji,na katika mikataba mingi ya kimataifa.Wenzetu wanachukua alimasi,sisi tunachukua chupa huku tunachekelea.Katika hali ya kawaida huelewi kwa nini mtu mwenye akili timamu ashabikie utanda wazi.Huu ni uzuzu wa kupindukia.Utanda wazi ungekuwa halali tu kama wote tungekuwa 'on equal footing,' kiuchumi,kijamii,kisiasa nakadhalika.Kinyume cha hapo ni upuuzi mtupu kwa kuwa kama hakuna usawa 'the other remains to loose.'Katika uzuzu wetu tukakubali kwamba ubeberu ndio suluhisho la uchumi wa dunia.Kiko wapi sasa,hao waiotuingiza mkenge na udanganyifu wao, wenyewe wanalia kilio cha Mbwa.Si miaka mingi ijayo watakuwa a 'third world country.' Jee, bado tumelala?Ni vema tukaamka sasa tukahoji kila kitu.Mungu amempa kila mtu akili ili kuweza kuwa 'diagnostic.' Tutumie akili hizo vizuri ili tuweze kufanya vitu original,ku-copy copy kutatumaliza.Wameshachukua alimasi yetu nyingi,tugangamale na hii iliyo baki,tusikubali tena.
   
Loading...