mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,661
- 18,035
Pale kituoni kura zikihesabiwa na kujazwa kwenye form (34A), kila wakala anaipiga pcha na kuwarushia watu wake, anapata hard copy kisha hiyo form inakuwa uploaded kwenye mfumo wa tume ya uchaguzi. Kila mtu anaweza kudownload na kujijumlishia ili kuona mwenendo wa mgombea yeyote, kisichotakiwa ni kutangaza tu kuwa nani ni mshindi maana hilo ni jukumu la Tume ya uchaguzi. Huku kwetu waliojaribu kuweka kituo cha kujijumlishia pale mliman city walikiona cha moto!!. Kwa wenzetu ruhusa kujumlisha lakini haramu kumtangaza yeyote kuwa ni mshindi!!
Kila chombo cha habari kimejijumlishia na kuweka wazi matokeo bila kutamka nani ni mshindi. Gazeti la The Daily Nation (online) la kenya limeweka tayari majumuisho zaidi nya asilimia 94% za kura zilizopigwa, na imeyaanika kama ifuatavvyo:
49.92%
6,702,438 Votes
49.41%
6,634,135 Votes
0.44%
59,449 Votes
0.23%
31,265 Votes
Kwa mujibu wa kura zilizojumulishwa la The Daily Nation: Jumla ya kura zilizojumilishwa ni 13,427,287.
Jumla ya kura zilizopigwa ni 14,164,561 sawa na asilimia 65.4% ya watu waliojiandikisha.
Kwa hiyo kwa mujibu yaliyooneshwa (siyo yaliyotangazwa), kura ambazo bado hazijajumlishwa ni 737,274 (zikiwemo zile zilizoharibika), Kwa hiyo kuna kila dalili kuwa uchaguzi utarudiwa kwa kuwa hakuna anayeelekea kupata asilimia 50 + 1. (Ruto ana 49.92% na Raila Odinga ana 49.41%).
Kama nia ipo, na sisi tunaweza kujifunza kitu kutoka kwa majirani zetu, ikizingatiwa kuwa Rais wetu mstaafu Kikwete yuko huko kama kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi ya Afrika ya mashariki!!
Ukizingatia walivyokaribiana vikali kati ya Ruto na Odinga, bila UWAZI katika mwenendo wa kuhesabu na kujumlisha kura hakuna ambaye angeridhika kuwa katendewa haki kama akishindwa!

William Ruto
UDA49.92%
6,702,438 Votes
Raila Odinga
AZIMIO49.41%
6,634,135 Votes
George Wajackoyah
RPK0.44%
59,449 Votes
David Waihiga
AGANO0.23%