Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Kuna kautulivu flani unakaona kwenye nchi, kuna kauhuru flani unakaona kuanzia vijiweni,makazini,barabarani na kwenye mitandao ya kijamii watu wakijadiliana mambo kwa Uhuru bila kukamatwa na hakuna athari ya Usalama iliyoripotiwa.
Kuna upendo flani umeanza kuonekana baina ya viongozi wa kisiasa, Leo wanasiasa wanaweza kukaa wakabishana kwa mbaali bila kutuhumiana au vyama vyao kuwaona wasaliti.
Upo upendo wa kiimani umerudi ambapo hata akina Bagonza, Ni'mugizi na wengine wanaheshimika nakuonekana mashujaa wa kupigania haki tofauti na awali walipoonekana kama wasaliti na wasio Wazalendo.
Kuna Uhuru flani umeanza kuchomoza ambapo kesi zinafutwa na viongozi wetu wa dini wa Uamsho wanaanza kuona progress ya kesi zinazowakabili.
Kinachotokea ndani ya miezi miwili kimetoa nuru kwa wafanyabiashara na wananchi kuendelea kufanya kazi na kutoa mchango wao kwa Taifa.
Swali: Tunaanza kujadili kurejea kwa Uhuru,amani na utulivu kutokana na ukweli kwamba viongozi waliokuwepo walilivuruga Taifa, walishindwa kutambua kwamba maendeleo yanatokana na furaha ya watu. Lakini pia hawakufanya makusudi bali walifanya kwa sababu katiba na sheria zilizokuwepo na zilizopo zinatoa mwanya huo. Mhe. Rais ni lini utaamua kufungua mjadala wa Katiba mpya nakuusimamia ili tuwe na amani yakudumu? Ni lini utatuondoa kwenye dhana ya CCM ni ileile? Ni lini utakubali kwamba hakuna CcM bila Tanzania?