Huu utata Toby was wizara ya elimu na ufundi kuwapangia wanafunzi kwenda vyuo binafsi ni kweli au ni utapeli ?

Madikizela

JF-Expert Member
Jul 4, 2009
675
439
Wadau, kuna kijana yatima kamaliza kidato cha nne nina mfadhili. Jana nimeletewa form zinazoonesha amechaguliwa na wizara ya elimu na ufundi, kwenda kujiunga na chuo cha ufundi moshi ambacho ni cha binafsi. Kuna mapungufu mengi kwenye makabrasha hayo ukiwa ni pamoja na tofauti ya mafunzo baina ya form ya wizara na ya chuo hicho binafsi.
Nawaombeni msaada wenu wa mawazo kama ambavyo fomu ambatishi zinavyo jieleza
IMG_7594.JPG
IMG_7595.JPG
IMG_7593.JPG



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Fuatilia kwa umakini unaweza kukuta yatima amejiongeza kimjini hajachaguliwa hicho chuo na wizara.

Au ni kweli ila muendelezo wa taratibu zetu za ovyo pale wizarani na ubabaishaji wa vyuo binafsi.
 
Fuatilia kwa umakini unaweza kukuta yatima amejiongeza kimjini hajachaguliwa hicho chuo na wizara.

Au ni kweli ila muendelezo wa taratibu zetu za ovyo pale wizarani na ubabaishaji wa vyuo binafsi.

Nashukuru, hizi fomu kazipata shuleni alikosoma


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hapa uwe makini, kwanza ujue aliomba kwenda kusoma wapi na kozi ipi. Hayo maombi alipeleka lini? Chaguzi zinatakiwa kupitia NACTE hivyo wawe na record za kuchaguliwa huyo kijana, lakini pia fuatilia shuleni na hakikisha chuo kimesajiliwa na NACTE. Wanaochaguliwa na waizara pamoja na Tamisemi bado chaguzi zao hazija toka labda mwezi wa Tano/Sita.
 
Back
Top Bottom