Msemajiwao
JF-Expert Member
- Sep 12, 2016
- 639
- 1,532
Habari wanajamvi,
Pamoja na kazi nzuri ya Jeshi la polisi, kuna baadhi ya matukio ambayo yananifanya nisiwe na imani katika mambo kadhaa. Leo nimepeleka chakula kwa mtuhumiwa ambaye yupo central polisi ambapo kashikiliwa.
Nashangaa tumefika pale mda wa kupeleka chakula ulipowadia, wote tuliokuwa tumepeleka chakula tukaambiwa tuwakabidhi polisi vyakula, wanachokifanya wanaandika jina la ndugu yako kwenye kikaratasi ambacho wana ki-attach kwenye chombo cha chakula, wanakuambia onja chakula halafu wanakichukua pamoja na vya watu wengine vinakusanywa. Baada ya kukusanya mnaambiwa ondokeni.
Swali;
Nani anayethibitisha kama chakula kile kitabaki salama kabla ya kupewa mtuhumiwa? Nina wasiwasi kwa muanya huo kutumiwa ndivyo sivyo kwa polisi ambao siyo waaminifu. Chakula hakipo salama kabisa kwa utaratibu huu wanaoutumia kituo kikuu cha polisi (Central police).