MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hivi kweli inaposikika sauti ya mtu yeyote awe kiongozi yeyote wa serikali anaposema kua tunataka kuipeleka Tanzania kufikia nchi ya kipato cha kati unajisikiaje? Halafu yule yule kiongozi natendo yake hayaendani na kauli zake, si hadaa ni nini? Si ndoto za mchana ni nini?
Nimeshangazwa sana na kitendo cha baadhi ya wabunge hasa wale wa viti maalumu sijui wale wateule wa Rais kushiriki katika uchaguzi wa mameya katika wilaya za Kinondoni na Ilala, Sasa kama ni hivi waendelee kushiriki na vikao vyote vya madiwani kila vitakavyofanyika katika manispaa hizo, Washiriki maamuzi yote yatakayokua yanafanyika ndani ya Manispaa hizo!
Lakini pamoja na hayo ni sheria ipi ambayo inamruhusu mtu aliyeshiriki kwenye uchaguzi mkoa mwingine akashindwa lakini Leo anaingia kwenye baraza la madiwani la Manispaa nyingine kumchagua Meya? Je, ndilo lengo hasa la kumleta mtu asiyehusika na eneo husika ni nini? Yeye nafasi yake ya udiwani katika manispaa ikoje? Imaana hawa hata kama kungekua na mgogoro wa uchaguzi wa mameya huko Arusha kwakua ni wateule wa Rais wangepelekwa kujazia palikopelea? Huu si utaratibu hata kidogo unaua demokrasia nchini na unafanywa kwa maksudi kabisa.
Tunajinasibu kufikia nchi ya kipato cha kati lakini sisi ndio tunategemea kuongoza kiujanja ujanja, kuunga unga bila kufuata taratibu, kwa tabia zetu hizi hizi tutaendelea kuota hicho kipato cha kati mpaka mwisho wa dunia.
Hakuna kiongozi mwenye nia njema na taifa hili hata kidogo, kila moja anachunga mkate wake ili aendelee kutafuna! Uzalendo haupo kabisa.