Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu Utapeli Wa Wakenya Utaisha Lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MJERUMANI, Oct 23, 2007.

 1. M

  MJERUMANI Member

  #1
  Oct 23, 2007
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 77
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Watanzania wanasifika kote ulimwenguni kwa upole na ukarimu wao ambao imekuwa kama mila na ndesturi kwetu.Ni desturi ya Watanzania kupenda wageni wetu na pia majirani zetu.Tunawapenda Wakenya,Waganda,Warundi,Wanyarwanda,Wazaire na majirani zetu wote.Tunawapenda majirani zetu kwa sababu ndivyo tulivyofundishwa na wazazi wetu ama vitabu vya dini.Watanzania tunasifika kwa upole na unyenyekevu pia.

  Ila sasa,naona huu upole na unyenyekevu wetu tulio nao kwa majirani zetu umevuka ipaka na unazidi kuididimiza Tanzania kwa mambo mengine.Kutokana na upole wetu,Majirani zetu,hasa Wakenya wanatutumia vibaya.Ninavyosema wanatutumia vibaya namaanisha kwamba wanatudharau na kutuona kwamba hatujui kujitetea na sisi tuko kwa ajili ya kunyonywa na hatujui kusema hapana.

  Kinachonisababisha nidiriki kusema maneno haya ni kwamba wenzetu wakenya kutokana na ujanja wao,wanatumia rasilimali zetu,ambazo ziko ndani ya nchiyetu,Tanzania,kujitangaza.Wanatumia rasilimali zetu kuvutia utalii.Wanatumia rasilimali zetu kuwavuta watalii kwenda nchini mwao kwa sababu wameutangazia ulimwengu mzima kwamba vivutio vingi vya utalii,hata vile vilivyoko Tanzania,viko Kenya,na watalii wanaelewa hivyo.

  Mfano mzuri ni Mlima Kilimanjaro.Kila Mtanzania anajua kwamba Mlima Kilimanjaro uko Tanzania.Lakini cha kushangaza ni kwamba wenzetu Wakenya wanautangazia ulimwengu kwamba Mlima Kilkimanjaro uko Kenya,na ukienda kenya utapanda Mlima Kilimanjaro.Matangazo kama haya nimekutana nayo kwenye train za Uingereza si mara moja.Ni maajabu kwamba picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo ni mojawapo ya vivutio vikubwa vya watalii,inatumika kuwavuta watalii kwenda Kenya na wala si Tanzania.Wakenya wanajua kabisa kwamba Mlima Kilimanjaro uko Tanzania na ni mali ya Tanzania,lakini binadamu hawa walivyo wajanja,matapeli wa hali ya juu,wanautumia mlima wetu kuutangaza utalii nchini mwao na kujipatia mapesa mengi kutokana na utalii.

  Hili linasababisha wao kuingiza mapato makubwa yanayotokana na utalii kuliko wamiliki wa mlima.Wanaenda Watalii wengi sana Kenya kuutazama Mlima Kilimanjaro,kwa sababu wanajua kwamba upo kule.Na kutokana na ukweli kwamba view nzuri ya Mlima Kilimanjaro inapatikana upande wa Kenya,basi Wazungu wao wanaamini kwamba Mlima Kilimanjaro uko Kenya.Na ndo maana wanatoka kwao Ulaya kwa wingi kwenda Kenya kuuona Mlima Kilimanjaro.Mahoteli yao yanajaa watalii,huku mahoteli yaliyoko Tanzania yakibaki na watalii wachache.Kipato kikubwa kinaingia Kenya,Watanzania tunabaki na ile fee ya kupanda Mlima peke yake.Haya mapato ya Hotel na Fee ya kupanda Mlima vingechanganywa pamoja,Tanzania ingekuwa inajipatia kipato cha kutosha kutokana na Mlima wetu,Mlima ambao ni mali yetu.Kusema la Ukweli hili suala limekuwa linaniumiza sana,huu upole wetu unatupeleka wapi????

  Kama miezi minne iliyopita,Tanzania ilipata bahati ya kutembelewa na Wabunge vijana wa EU.Wabunge hao walipokuja walipewa majarida mbalimbali,mojawapo lilikuwa linaonesha vivutio vilivyoko Tanzania.Huwezi kuamini kwamba wale Wabunge vijana kutoka EU walishangaa sana kuona kwamba Mlima Kilimanjaro upo Tanzania.Waliuliza na wakajibiwa kwamba Mlima huu uko Tanzania na ni mali ya Tanzania pekee.Wajua wale Wazungu walishangaa sana,kwa sababu wao siku zote wanajua kwamba Mlima Kilimanjaro uko Kenya,na hivi ndivyo Wakenya wanavyowaambia.Wale Wazungu waliwaacha Watanzania na Ujumbe kwamba Wakati Umefika kwa Tanzania kutangaza Utalii wake vya kutosha ndani na nje ya nchi.Yaani mpaka hawa Wazungu walituonea huruma mpaka wakaamua kutupa ushauri kwamba tuitangaze Tanzania na vivutio vilivyoko Tanzania ili Utalii uweze kuliingizia taifa Mapato ya kutosha.Hili suala hatukuwa tunahitaji Wazungu kuja kutukumbusha,niWajibu wa kila Mtanzania kuitangaza nchi yake na pia serikali na wale wenye mashirika ya Kusafirisha na kuhudumia Watalii kuhakikisha kwamba ujumbe unawafikia walengwa kwa usahihi kabisa.

  Hili la Mlima Kilimanjaro tuliweke pembeni kidogo.Nikiwa Uingereza pia,ndani ya Treni na kwenye vituo mbali mbali vya Utalii vinavyomilikiwa na Wakenya,nilishangaa kuona pia wanaitumia Mbuga yetu ya Serengeti kujitangaza na kuutangaza utalii nchini mwao."COME TO KENYA AND SEE ANIMALS FROM SERENGETI".Haya ni baadhi ya matangazo ambayo kwa wadau wa Uingereza na nchi mbali mbali za Jumuiya ya Ulaya wanakutana nayo kila siku.Tunajua kwamba Serengeti iko Tanzania,iweje Wakenya waitumie kujitangaza na tuwanyamazie?

  Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo inazalisha madini ya Tanzanite.Lakini cha ajabu ni kwamba Kenya na India ndo nchi zinazojulikana kama wauzaji wakubwa wa madini ya Tanzanite.Na kama mnakumbuka,ni kwamba Kenya ilishawahi kuzawadiwa klutokana na kuuza Tanzanite yenye ubora na nyingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

  Hii ni mifano michache tu ya ufisadi ambao Wakenya wanawafanyia Watanzania.Kinachoshangaza ni kwamba Viongozi wetu wamekaa kimya,hawasemi chochote na hawahoji chochote.Masuala haya yanaandikwa mara nyingi sana kwenye magazeti na nakumbuka hata JK alipotembelea Uingereza mwaka jana,alikumbana na swali kuhusu Mlima Kilimanjaro,majibu aliyoyatoa yalikuwa ni ya kisiasa na hayakumaliza tatizo kwa njia moja ama nyingine,na wakenya wanaendelea kuutumia Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Serengeti na mali asili nyinginezo kujtangaza.

  Mimi naona wakati umefika sasa kwa viongozi wa Tanzania kuwaambia hawa majirani zetu Wakenya kwamba sasa basi.Huu ndo muda wa serikali kutoa tamko kwamba Kenya hawaruhusiwi kujitangza kwa kutumia rasilimali na vivutio vya Tanzania.Huu ndo wakati muafaka kumwamsha Professor Jumanne Maghembe,Waziri wa Maliasili na Utalii,ambaye analijua hili na anajua kwamba Mlima Kilimanjaro uko nyumbani kwao,lakini bado amekaa kimya.Mheshimiwa Maghembe,chukua hatua za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba huu utapeli wa Wakenya unaisha.Wakenya wametudharau vya kutosha,wanajua kwamba hatuna cha kuwafanya ndo maana wanaamua tu kutumia mali zetu kujipatia mapato.Uchumiwao unakuwa kwa kasi,na utalii ni sehemu ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ukuaji wa Uchumi wa nchi yao,huku uchumi wetu ukianguka siku hadi siku.

  Ni wakati muafaka sasa wa kuwaambia Wakenya kwamba inatosha.Vinginevyo watakuja kudai kwamba Mlima Kilimanjaro ni mali yao na hapo ndo tutakaposhangaa kwamba tuliacha kuziba ufa,na kutokana na hilo inabidi tujenge ukuta.Waswahili wanasema ,"Mdharau mwiba,Mguu huota tende".Sasa naomba Watanzania,Viongozi wa serikali,Mheshimiwa Maghembe,tuache ufisadi na kujisifu tu,tuangalie pia haya mambo ya muhimu kwa taifa letu.Vinginevyo kuna siku tutakosa maelewano mazuri na hawa majirani zetu.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,195
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante Mjerumani kwa habari hii.

  Hata hivyo nadhani viongozi wetu wa serikali wanatumbua pesa zetu zaidi ya hao wakenya wanaofaidika na mlima kilimanjaro.
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,097
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 180
  ....i withdraw!
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,574
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Too long

  cant read all that

  [​IMG]
   
 5. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,483
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
 6. S

  Son Of Dead Millionare Member

  #6
  Oct 23, 2007
  Joined: May 30, 2006
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usijali, mie nawasiliana na mkuu wa nchi ili tuwachape hawa siku moja ndio watajua kama hawana kitu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 690
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mjerumani huu unatokana na ubwege wa vioungozi wetu na taasisi zetu. Mimi nakumbuka wakati fulani nipo Jpn kukawa na African festival nilijitahidi sana kutafuta banda la ubalozi wa Tanzania sikulipata ila kulikuwa na wajapan kibao na NGO zao za kutangaza utamaduni wa mtanzania na kuuza Khanga za kitanzania moja kama dola 40 niliongea nao wanaongea kiswahili kizuri sana na wanaitwa Waswahili Club hawa jamaa waliniambia hivyo hivyo Tanzania tona portential nyingi sana lakini serikali yetu haifanyi jitahada zozote.

  Nikakuta siku hiyo kulikuwa na mabanda manne ya Ubalozi wa Kenya wanauza Tusker, vinyago, Khanga, ugali Nyama choma na kuutangaza utalii kwa kutumia mlima Kilimanjaro. Mara nyingine tena nilienda kwenye festival nikakuta kuna banda moja la Ubalozi wa Tanzania na aliyekuwa pale si mtanzania bali ni mjapan ambaye haielewi hata Tanzania kweli roho iliniuma sana.

  Siku nyingine nilikawa napresent paper mwishoni nikawakaribisha washiriki kuwa Karibuni Tanzania karibuni nchi ya Mlima Kilimanjaro. Kuna Profesor mmoja Mhindi prominent profesor akaniuliza kwani Kilimanjaro iko Tanzania? then kuna dada mmoja wa Kenya nae alikuwepo jamaa akamuuliza kwani Kilimanjaro iko Tanzania? Yule dada bila aibu na ni msomi alisema uko Kenya Tukabishana nikawaambie wakasome kwenye Mitandao.

  Siku nyingine niko Londoni nikatumia wafurushi na rafiki yangu Mkenya kwenye stamp zao kuna picha ya Mlima Kilimanjaro na wanasema karibu utembelee Mlima Kilimanjaro Kenya na naaminii stamps ni za serikali. Hii inaonyesha kuwa serikali kwa kusirikiana na wananchi wake wanatuhujumu. Lakini ninataka kusema tuu waache watuhujumu kwasababu:

  YA UJUHA, UVIVU NA UJINGA WETU. TUKILALAMIKA HAITOSHI. MJERUMANI NADHANI HII ARTICLE YAKO UNAWEZA KUMTUMIA WAZIRI NA HATA KATIBU MKUU MAANA WANAJIFANYA HAWAELEWI KINACHOEENDELEA.
   
 8. P

  Pedro Senior Member

  #8
  Oct 24, 2007
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 115
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hata kichwa cha habari tungekibadilisha kiwe Ufala wetu na ulaza utaisha lini? au Ufala wa watanzania utaisha lini?

  Mimi binafsi pia nimejikuta mara kadhaa nikiutetea mlima wetu, lakini kinachoniuma zaidi ni pale ninapowaambia jamaa ninatoka Tanzania wanakuwa hawana idea mpaka niwaamie tupo karibu na Kenya ndo wanasemaa "aah!ok! i know where that is".

  Wizara ya utalii na mali asili hivi wanafanya nini? hawana strategy plan yoyote for the next 5 years? hivi ukiwauliza where do you see youself in 2011 wanajibu nini? labda lengo ni kuwa na Land Cruiser Baloon mpya.
   
 9. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 690
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wapo busy wanauza magogo yetu nnje ya nnchi huku wakila rushwa kwa kwenda mbele na kuharibu mazingira. Hivi issue ya makontena ya magogo yako wapi?

  Kuna kitu kimoja kilifurahisha sana. Nilisoma kuwa kila mtalii anaeenda Okinawa Japan anatakiwa kupanda mti mmoja na wanaweka jina lake kwenye huo mti na ukija hata baada miaka 10 unaukuta na serikali ya hiyo prefecture wanakutumia picha ya mti wako kila baada ya mwaka. Hebu niambie kama wanakuja watalii milioni moja kwa mwaka ina maana miti milion moja inapandwa kwa mwaka na watalii wanajisikia very proud kupanda miti. Local government yenyewe ina miche tuu ukija unapewa. Nadhani ni mbinu nzuri ya kuusaidia mlima kilimanjaro.


  Pia kuna kamlima kanaitwa fuji yaani jamaa wanavyokatangaza huwezi kuamini na nikamlima kakupanda kwa masaa machache. Kenya sasa wanaanzisha program ya community tourism ambapo watalii wanakuja na kuishi na wananchi wa Kenya na kujifunza utamaduni wa Kenya (Home Stay) na target yao ni watalii kama wanafunzi na etc kutoka nnje.
   
 10. H

  Hume JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 329
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Brazameni acha uvivu. Tukiendekeza uvivu hatuwezi kuendelea!
   
 11. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 237
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mjerumani,
  Tatizo sio Kenya,ujinga upo kwa viongozi wetu,kwani wakati Kenya wanatangaza siye huwa tupo wapi?Ngoja wafaidike na maliasili zetu.
   
 12. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 690
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa hisani ya SHY naweka huu wimbo wa safari soundi hapa mjionee waKenya wanavyotangaza mlima wetu.

  [media]http://www.youtube.com/watch?v=bKNzSfoKeK8[/media]
   
 13. m

  mdau halisi New Member

  #13
  Oct 24, 2007
  Joined: Oct 17, 2007
  Messages: 1
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafurahi wabongo wengi mnaliona hili, hawa ndugu zetu kutoka kenya wamekuwa hivyo muda mrefu sana. Sasa hivi tunavyoongea nafurahi kwamba serikali ilshachukua hatua muda mrefu na ndio maana ukiangalia takwimu zinaonyesha utalii unakuwa bongo. Hatua mojawapo ni kufunga mpaka wa kutoka amboseli national reserve kenya kuingia sinya game reserve. Hivyo mtalii akitoka Kenya hawezi kupanda mlima bila kupitia kwenye mipaka inayojulikana, na guide aliyeko naye ataulizwa working permit hivyo mtalii huyo atapanda mlima na guide wa Tanzania.
  Kuhusu swala la kuona wanyama wa serengeti ukiwa kenya ni kweli coz kuna Serengeti migration baadhi ya wanyama wanafika masai mara national reserve ya kenya. nako kulikuwa na mpaka miaka ya 80 mwanzoni walikuwa wakiingia serengeti from masi mara nao umefungwa hivyo kuwafanya utumia mipaka inayojulikana na watalii hupelekwa serengiti na watanzania wenyewe. Hiyo ni sababu mojwapo ya wakenya kutaka shirikisho la africa mashariki liharakishwe, ili waweze kuendelea kutunyonya. kwenye hoteli zote za kitalii walikuwepo managers, ass. managers,chief cooks supervisors na engineers kutoka kenya serikali imewaondoa wengi sana, kwa kutokuwa na vibali vya kufany kazi na vile vile wapo wabongo wenye uwezo na qualifications za kufanya kazi hizo. Lakini hawa jamaa walitutangulia sana na wametunyonya vya kutosha.
   
Loading...