Huu utapeli unaujua ? Wamekomaa na mimi jana leo nimewashtukia

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,538
1,753
Huu ni utapeli wa style fulani, yawezakana ulisha kuwepo ila kwangu ndio nimekutana nao jana na leo asubuhi ndio nikashtuka baada ya kuambiwa sasa tuma pesa ili tununue hii tender documents kwa sababu tumeona kampuni yako ndio inauwezo wa ku supply hizi huduma kweye picha
Namba ya anaejifanya ndio msamamizi wa mradi:
067 752 9340 na huyu 0714976568 ndie muhasibu feki anasema sasa tuma pesa ya tender
IMG_0918.JPG

View attachment 1224418
 
Sasa hapo tutaelewaje mkuu walikupigia tu wakakuambe uwatumie pesa? Hujasema ilianzaje alafu majibu yako yanaonyesha haupo vizuri afya ya akili

Mbona nimesema wazi kabisa walisema bird document inauzwa nitume pesa laki na 18 ndio nikashutuka . Na jinsi alivyo kuwa anaharakisha, tutakutumia kwa basi sio ?
 
Hivi wanafikiri kila mtanzania ana kampuni!?..huu utapeli hauna muda mrefu mjini bora hata ule wa ile hela..

Sema usipokuwa makini unaweza pigwa unajua utulivu ni jambo muhimu sana kwenye maamuzi. Anakupigia jamaa wala haongei mambo ya pesa. Sasa anajua list ya hivi vitu huwezi tuma quotation kwa haraka hivyo anakushauri wahi kwanza kupata tender document kabla ya deadline anakupa namba nyingine anazuga ni ya mtu wa procurement au muhasibu sasa huyu ndio ana kwambia gharama
 
Juzi wamenitumia meseji "mtoto anaumwa hospitali".......
Nilicheka sana, mtoto nampatia wapi mie

Sasa hawa ni wapuzi saana hili jina walilotumia la manyunyu girl’s secondary ni shule fulani ya njombe nakumbuka nikiwa Njombe secondary miaka fulani tulisha wahi letewa tucheze nao mziki nikampigia jamaa moja wa njombe ka ni link na mwl mmoja kasema hakuna kitu kama hicho
 
Matapeli bwana

hawa viumbe sijui hata wanaroho gani

details wanapozipata ndio wanaponchosha
 
Juzi wamenitumia meseji "mtoto anaumwa hospitali".......
Nilicheka sana, mtoto nampatia wapi mie
Kuna watu wanapigwa hivyo mdogo wangu nusu apigwe hivyo hata ww kama ungekuwa na mtoto tena awe anasoma boarding halafu unaambiwa mtoto wako anaumwa mimi mwalimu mkuu inahitajika kiasi fulani..kwa kuchanganyikiwa huwezi kuuliza mara mbili mbili na kuhoji kama una moyo mdogo unajikuta tu umetuma hela ya matibabu😂😂
 
Sema usipokuwa makini unaweza pigwa unajua utulivu ni jambo muhimu sana kwenye maamuzi. Anakupigia jamaa wala haongei mambo ya pesa. Sasa anajua list ya hivi vitu huwezi tuma quotation kwa haraka hivyo anakushauri wahi kwanza kupata tender document kabla ya deadline anakupa namba nyingine anazuga ni ya mtu wa procurement au muhasibu sasa huyu ndio ana kwambia gharama
😂😂 Hasa kampuni yako ikiwa haijapata tender muda mrefu na usawa huu unatumiwa quotation kama hiyo wewe hata huulizi hii tender inatoka wapi unatuma tu hela usipopajua....
 
Bila kusahau makampuni ya kubeti, kila kukicha nakutana na vimbwenga vya moja spesho, sijui jack pot yani ni utapeli juu ya utapeli.

Kwani bila kubeti siishi?

Kwani lazima kila Mtu awe mcheza kamali?
 
Back
Top Bottom