Huu utamaduni wa Kipuuzi sasa ufike Kikomo na Wahusika mjitathmini haraka

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,417
108,519
Kwa siku za hivi karibuni kamezuka ‘ katabia ‘ ka ajabu sana ambako nadiriki kukaita ni ka ‘ kipumbavu ‘ mno pale ambapo utaona siku Kiongozi fulani akiwa anafanya ziara yake mahala fulani basi ghafla tutaona Watu wanaenda na ‘ mabango ‘ yanayoonyesha ‘ kero ‘ zao zinazowakabili na mara nyingine utaona ‘ Wajane ‘ nao wanaomba kwenda mbele alipo huyo Kiongozi kumlalamikia.

Viongozi wa Tanzania wakumbuke kwamba Tanzania ya leo si ile Tanzania ya miaka ya nyuma ambapo ‘ uelewa ‘ wao ama uliminywa ‘ kiaina ‘ au ni kweli ulikuwa ni mdogo na ndiyo maana wakawa wanapelekwa pelekwa ila sasa wajue kuwa Watanzania wa sasa ni ‘ waelewa ‘ tena pengine hata kuwazidi wao ( Viongozi )

Ni kweli yawezekana kabisa kwamba hao ‘ Wananchi ‘ wakawa na madai yao ya kimsingi kabisa na hao akina Mama ‘ Wajane ‘ na wao pia wakawa na matatizo yao ila hapa ‘ logically ‘ tu kuna maswali mengi ya kujiuliza ambayo ukiyapatia maana utagundua ya kwamba ‘ mbinu ‘ hii ni ya ‘ Kipumbavu ‘ mno na ikiwezekana iachwe / ikome haraka sana.

Hivi hao Watu wanaokwenda na hayo ‘ mabango ‘ ina maana huwa wanasubiri tu hadi ‘ Viongozi ‘ wao wafanye ziara huko walipo ndipo wayaandae hayo mabango? Hivi hayo mabango walishindwa kwenda nayo Ofisi za ama Wakuu wao wa Wilaya na Mikoa ili wayashughulikie hasa ukizingatia kwamba hawa ‘ Viongozi ‘ huwa wanakuja tu na kuondoka lakini hao Wakuu wa Wilaya na Mikoa huwa wanakuwa nao hapo muda wote?

Hivi hawa akina Mama ‘ Wajane ‘ ambao kutwa huwa ‘ wanavizia ‘ tu hadi Viongozi waende huko walipo nao walishindwa kweli kuyapeleka hayo malalamiko yao ya ‘ kudhulumiwa ‘ kwa Wakuu wao wa Wilaya au Mikoa ili yashughulikiwe haraka mpaka wanasubiri ‘ Kiongozi ‘ aende huko halafu wanatulilia ‘ Kisanii ‘ ili tu ‘ wawahadae ‘ Watu?

Nirudi kwenu nyie ‘ Viongozi ‘ mnaopenda kutafuta ‘ cheap popularity ‘ na ‘ public sympathy ‘ kwamba hii ‘ Leadership ‘ style yenu wala haina ‘ tija ‘ kwa dunia ya sasa na sana sana tu mnaonekana ni wa ‘ hovyo hovyo ‘ mbele ya Watu ‘ waliobarikiwa ‘ akili / upeo na Mwenyezi Mungu. Ikiwezekana jitafakarini haraka na mbadilike kwani hii mbinu inawaacheni tu ‘ uchi / watupu ‘ na taratibu mnaanza ‘ kudharaulika ‘ na Jamii mnayoiongoza.

Mbinu kubwa ambayo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akiitumia na kiukweli ndiyo ilimsaidia kuongoza Tanzania kwa miaka yake yote ile 23 ilikuwa ni ya ‘ ushirikishaji ‘ Wananchi bila kujali Elimu, Dini, Uchumi wao na Makabila yao ambayo iliweza kumsaidia kuyajua mengi hata yale ambayo yalijificha na ‘ nyeti ‘ zaidi.

Kiongozi mzuri ni yule tu ambaye hata kama ni ‘ Mkali ‘ lakini ana ‘ Ukali ‘ wa kujenga na siyo wa ‘ Kuharibu ‘ kabisa. Nyerere alikuwa ni ‘ mkali ‘ kweli ila alikuwa ni ‘ makini ‘ halafu hana dharau, hana maneno ya karaha, haendekezi chuki, visasi na unafiki lakini alikuwa ni Mtu anayependa mno mawazo ya Watu wake anaowaongoza na ndiyo maana ili kuliamini hili Nyerere hakuwa ni Kiongozi anayelindwa sana kwa misilaha mikubwa mikubwa na maduribini mengi huku wengine wakipanda katika miamba kumlinda kama akiwa mahala penye milima.

Halafu nitoe tu ombi kwenu nyie ‘ Viongozi ‘ kwamba embu basi siku zingine mnapokuwa mnawapanga hao ‘ Wajane ‘ kuja mbele ‘ Kuigiza ‘ wawe wameiva kweli ili hata sisi ‘ Mangumbaru / Wajinga ‘ akina GENTAMYCINE tusiweze kung’amua / kushtukia ‘ chezo ‘ haraka. Hivi inakuwaje ‘ Mjane ‘ anaitwa kuja mbele halafu kwanza anaanza kulia kisha ananyamaza ghafla mara tena analia huku machozi hayaonekani mara tena analia halafu akipewa tu hela huko kulia kunakoma ghafla na tabasamu la ‘ Kutukuka ‘ linaanza kuonekana ‘ usoni ‘ mwake?

Nyie Viongozi ni nani aliyewaambieni kwamba kukimbilia kutoa ‘ Hela ‘ kwa hao ‘ Wajane ‘ ndiyo suluhisho pekee la kutatua ‘ Kero ‘ zao? Na kama kumbe huwa mnajua kuwa huwa mna ‘ Hela ‘ za kuwasaidia ‘ Watanzania ‘ wenye matatizo na mahitaji sasa kwanini hizo ‘ Hela ‘ ambazo huwa ‘ mnajishebedua ‘ kuzitoa ‘ majukwaani ‘ msiwe tu mnazi ‘ inject ‘ moja kwa moja katika Vyombo husika au Taasisi au Mashirika husika ya misaada ili badala ya kumfaidisha huyo ‘ Mjane ‘ mmoja basi ‘ wafaidike ‘ wengi?

GENTAMYCINE namalizia kwa kusema kwamba nyie Viongozi wetu wa ngazi mbalimbali hapa Tanzania mkitaka muongoze vyema, mkubalike na mje kukumbukwa hata mkiondoka basi wekezeni sana katika kuwashirikisha Watu wote bila kujali anatoka upande gani wa Kisiasa, heshimuni mawazo ya Watu hata ya wale ambao mnawaona ni ‘ maadui ‘ zenu na pia mjenge dhana ya ‘ Kuvumiliana ‘ na mtambue kuwa moja ya dhana nyingine ya ‘ Uzalendo ‘ ni Kupendana na Kutobaguana hasa tukiamini kwamba Tanzania siyo ya Mtu mmoja tu bali ni ya Watu takribani Milioni 50.

GENTAMYCINE nimechoka na ‘ mazingaombwe ‘ na ‘ matukio ‘ yenu yasiyo na Kichwa wala miguu. Jirekebisheni!

Ni imani yangu kubwa kwamba ‘message sent and delivered ‘ kule kunakohusika na wahusika watajitathmini.

Nawasilisha.


 
Mkuu umenena vyema sana, Jana nilifikiria sana juu ya hili...

Ina maana hakuna haja ya kuwa na RC,DC,RAS na DAS, maana yule mama malalamiko yake Mkurugenzi wala viongozi wengine hayakufika juu ya meza yao lakini imewezekana kufika kwenye meza ya RAIS..

Kihaki kabisa ilibidi RAIS autumbue uongozi mzima wa mkoa maana kero hazitatuliwi mpaka RAIS aje sasa..
 
Wenye akili watakuelewa na watayafanyia kazi maoni yako.
Ahsante.

Naamini kwamba ' message sent and delivered ' kwa watakaoguswa na ' uzi ' wangu kwani sasa tumechoka na hizi tabia za ' Kipumbavu ' ambazo sioni ' tija ' yake yoyote zaidi tu ya kuwadhalilisha na wao kujichoresha vile vile mbele ya Watu wenye ' akili ' zao za Kutukuka.
 
uzuri mmoja IKULU huwa inachukuaga mawazo yako(raisi awe anaandikiwa hotuba).
WATALIFANYIA KAZI.

Sijaiandikia IKULU bali nimewaandikia ' Viongozi ' wote waliopo nchini Tanzania ambao wanajukumu la kuwaongoza Watu wao wanaowaamini. Katika ' content ' yangu hapo kuna mahala labda nimeandika neno IKULU Mkuu? Kuhusu mawazo yangu mengi ambayo huwa nayaandika humu JamiiForums kuchukuliwa na kufanyiwa Kazi kwa ' umakini ' wake wala hujakosea na hilo nina uhakika nalo tena 100% kwamba kuna ' Njemba ' mbili zipo humu ' maalum ' kuangalia ninachokiandika na kama ni very ' sensitive ' kinajadiliwa na kufanyika hivyo naamini kwamba kwakuwa hata huko huko ' IKULU ' na kwenyewe kuna ' Viongozi ' kama waliopo maeneo mengine basi na Wao pia haya mawazo ya GENTAMYCINE watayazingatia na kama na Wao wanafanya huu ' upuuzi ' basi wataachana nao na watajirekebisha haraka.
 
Naamini kwamba ' message sent and delivered ' kwa watakaoguswa na ' uzi ' wangu kwani sasa tumechoka na hizi tabia za ' Kipumbavu ' ambazo sioni ' tija ' yake yoyote zaidi tu ya kuwadhalilisha na wao kujichoresha vile vile mbele ya Watu wenye ' akili ' zao za Kutukuka.
Umesahau kuongezea Utapeli kupitia haya mabango. Si ajabu huyo mama hana haki ila kwa vile ni mjane!!!!! Hii tabia ya Mabango na kuita watu majukwaani ni hatari na ya ..... Aidha kutoa fedha hadharani kwa Mkuu si halali. Nyerere tangu awe Rais hakuweka hela mfukoni mwake mpaka kifo
 
Back
Top Bottom