Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,314
Nchi huongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu. Lakini pamoja na hayo utamaduni ni jambo muhimu na la msingi katika kuongoza na kuonyesha uongozi. Rais Mstaafu Mzee Mkapa alianzisha utaratibu wa kuongea na wananchi /Taifa kupitia hotuba za kila mwezi. Aliemfuata nae suala hili alilipa kipaumbele.
Raia wetu Mh Magufuri tangu aapishwe hatujamsiki wala kumwona akitoa hotuba ya kila mwisho wa mwezi. Pengine bado mapema lakini ni vizuri akafuata utaratibu walioutumia watangulizi wake. Fursa hii ya kila mwezi ilikuwa ni jukwaa nzuri la wananchi kupata ufafanuzi ulio wazi na bayana kutoka kwa Rais. Lilikuwa ni jukwaa zuri kwa Rais kujipambanua na kuonyesha msimamo na mlengo wa serikali anayoiongoza.