The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
juzi nilimskia simon siro kamishna wa police kanda maalum ya dar akiongea nyuma ya kinasa sauti kua eti watawakamata wanaume wanaonunua madadapoa, jambo ambalo pia nimemskia waziri ummy mwalim akirirudia tena kwa msisitizo kama alivyosema siro ni dhahiri kua jambo hili linakera sana lakini kuna wakati najiuliza kuhusu dhamira ya viongoz wetu kushughulikia kwa mambo kwa dhati ukweli ni kwamba hao dadapoa wanafahamika maeneo yao ya kazi siro anayajua ummy anayajua watendaji wa tarafa kata mitaa wanayajua na kama hawayajui ntashakia uraia wao mi nilitegemea wangefanya ziara za kushtukiza ili tuwasikie wamekamatwa dadapoa na wanaume kadhaa ili wengine waogope badala ya kupiga makelele nyuma ya maiki mikwara ya namna hii tushaisikia sana namshauri siro wale migambo wa jiji waachane kwanza na mamantilie na machinga waje huku tandika walahi waje na makarandinga ya kutosha kwani huku ni biashara rasmi kila mtu anaijua nimewahikuskia kua hata kodi inakusanywa.