Huu usemi/methali huwa maana yake ni nini?

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
4,950
2,000
Nimekuwa nausikia sana ukitumiwa sehemu mbalimbali lakini nimeshindwa kabisa kujua maana yake na matumizi yake.

"Kumkoma nyani giladi"

Kumkoma na giladi huwa ina maana gani na inatumikaje?
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,967
2,000
Kumtega nyani kwa werevu wake --- kumgeuzia mtu kibao kwa maneno au matendo yake --- kumtendea mtu wema (kinyume na hiana yake) ambao ni sawa na wema mchungu kwake.

Kumkoma = kumtega/kumnasa
Giladi = werevu, hila, ujanja ambao huendekezwa kwa upofu.
 
Shukran mkuu
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,047
2,000
Nimekuwa nausikia sana ukitumiwa sehemu mbalimbali lakini nimeshindwa kabisa kujua maana yake na matumizi yake.

"Kumkoma nyani giladi"

Kumkoma na giladi huwa ina maana gani na inatumikaje?
Ni usemi wa kizaramo sio kiswahili sanifu... Yaani ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni utaona huruma
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,047
2,000
Kumtega nyani kwa werevu wake --- kumgeuzia mtu kibao kwa maneno au matendo yake --- kumtendea mtu wema (kinyume na hiana yake) ambao ni sawa na wema mchungu kwake.

Kumkoma = kumtega/kumnasa
Giladi = werevu, hila, ujanja ambao huendekezwa kwa upofu.
Mmh hapana
Kumkoma ni kibantu yaani kumuua
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,047
2,000
Vipi kuhusu " Muenda tezi na omo marejeo ngamani" hii inamaanisha nini na inatafsirikaje?
Hiki ni Kiswahili cha pwani, maana yake ni ...
Nenda popote lakini utarejea ulipotoka

Tezi na omo ni sehemu kwenye jahazi au mashua au jahazi
Ngamani ni ufukweni ama katikati ya chombo
Tezi ni sehemu ya mbele na omo ni sehemu ya nyuma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom