Huu urembo wa kucha kwa wanawake.....Mh!!! mi hoi kabisa.............

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Last week end nilikuwa maeneo ya mwenge pale nikiwa na mwandani wangu. Kimsingi aliniomba nimsindikize akatengeneze kucha zake. Tukatia timu, mwenyewe anadai kuna kijana ambaye humtengeneza hizo kucha mara kwa mara. Tukafika mwenge na yule jamaa tukamkuta, kwa kuwa alikuwa na mteja mwingine tukalazimika kusubiri. Then ikafata zamu ya honey wangu. Mamaaa akavua viatu akaweka miguu kwenye mapaja ya kale kajamaa, kakaanza kumnyoosha vidole vya miguu kama masaji fulani hivi. Nikimuangalia demu wangu sikuamini, amejiachiaaaa katuliaa jamaa anabonyeza vidole then ndio akaanza kumsafisha hizo kucha na baadae kumpaka rangi kwa mtindo aliotaka....Alipomaliza tukiwa kwenye gari tunarudi nyumbani nikamwambia next time akitaka kusafisha kucha na kupaka rangi hilo zoezi nitalifanya mimi tukiwa chumbani kwetu kwani sikupenda jinsi jamaa alivyokuwa anamchezea miguu ni wazi alikuwa anamtekenya kimtindo.....Huwezi kuamini alinigomea kwa nguvu zote...Hivi wana nini wale jamaa pale mwenge???
 
Wewe ndiyo unamatatizo! Kwanin humwamini honey wako? au ulishang'wata na nyoka one time mkuu? ndio mana hutaki tena machungu yakurudia nini?
 
Utafanya mangapi kaka?Hiyo niprofessional ndio maana si wote wnafanya.
Acha kuingilia kazi za watu
Si alipendeza?
 
..Namuamini sana sikupenda lake kajamaa kushika shika nyayo za mke wangu..we ukiguswa huko unajisikiaje??

Atacheka na kutabasamu! wife alifanya hivyo hivyo nini! hapo mkuu lazima uso ujikunje kama umenusa tumbaku!
 
Kweli huo ni wivu uliopitiliza, Mgosi anakutana na wateja wengi kwa siku atatembea nao wote????

Akiwa kazini hakutazami usoni yuko busy kuingiza kipato.
 
Mwandani..Mamaa na demu juu!Kaazi kweli kweli!Acha kumuonea wivu mshkaji anafanya kazi yake tu...ongeza mapenzi nyumbani ili usikose kujiamini!
 
Mwandani..Mamaa na demu juu!Kaazi kweli kweli!Acha kumuonea wivu mshkaji anafanya kazi yake tu...ongeza mapenzi nyumbani ili usikose kujiamini!
...Sio mchezo mwanawane!!!
 
We unafikiri ni nini?? Umekaa na mkeo anasafishwa kucha upo hajafanywa kitu roho inakuuma kama si wivu ni nini
...acha kuuma yaweza kuchomoka bana! we vipi?? akashike makanyagio ya mkewe huko!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom