Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,900
- 21,987
AFP waunga mkono Karume aongezewe muda
Nora Damian
CHAMA cha Alliance for Tanzania Farmers (AFP), kimetaka Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aongezewe muda, ili awe katika nafasi mzuri ya kuunda serikali ya mseto.
Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na hoja zinazokinzana, kuhusu kiongozi huyo ama kuongezewa au kutoongezewa muda wa kuongoza serikali ya Zanzibar.
Mapema wiki hii, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa, alikaririwa na gazeti dada la The Citizen, akitaka Rais Karume, aongezewe muda wa kuwa madarakani, lakini baadaye Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema huo si msimamo wa chama chake.
Pia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), kilichomweka madarakani Rais huyo kimesema hakina mpango wa kumuongezea kwa sababu utaratibu hauruhusu.
Hoja ya kutaka Rais Karume aongezewe muda wa kuwa madarakani, imeibuka katika majuma ya hivi karibuni baada ya kiongozi huyo na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad, kukutana na kukubaliana kuzika tofauti za kisiasa, jambo ambalo limewaletea sifa viongozi hao.
Akizungumzia hoja hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa AFP, Said Soud Said, alisema si dhambi Rais Karume,kuongezewa muda wa kuwa madarakani na kwamba dhambi ni kutoa wakimbizi wanaotokana na machafuko yanayoweza kutokea baada ya uchaguzi
Alisema Wanzanzibari, wanahitaji mno kuwepo kwa serikali ya mseto, ili hatimaye waweze kuishi kwa amani na utulivu huku wakiwa wamoja.
Sais alisema Zanzibar inaongozwa na katiba ya nchi na kwamba kwa kupitia katiba hiyo, Rais Karume ana uwezo wa kuunda serikali ya mseto akivishirikisha vyama vyote vya siasa, hatua ambayo alisema italeta utulivu katika visiwa hivyo.
"Kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar, kutasaidia kuindoa nchi hiyo katika mitafaruku ya mara kwa mara ya kisasa inayotokana na msimamo wa viongozi walioko madarakani, kukataa serikali ya mseto," alisema Said.
Hivi karibuni, CCM kupitia Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Pius Msekwa, ilisema haiwezi kumuongezea muda Rais Karume, muda wa kuwa madarakani kwa sababu ni kinyume cha katiba.
Msekwa alisema katiba ya chama hicho, inataka marais wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika nyadhifa hizo kwa mihula miwili ya miaka mitano, kwa kila muhula.
Katika hatua nyingine, chama cha AFP kimeiomba serikali kutoa msamaha wa kodi kwa vyama vya siasa ili waweze kuingiza nchini vifaa vya kampeni ambavyo alidai kuwa ni rahisi kuvinunua nje kuliko hapa nchini.
Chama hicho ambacho kimeanzisha operesheni ijulikanayo kama 'pomboo' kuhamasisha wananchi kujiunga nacho pia kimemtaka rais Jakaya Kikwete akutane na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kabla ya muda wake wa uongozi kumalizika ili waweze kumweleza mambo mbalimbali