Huu upumbavu wa PF 3 utakoma lini?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Mwanzoni mwa mwaka 2000 nilimpoteza rafiki yangu wa karibu kufuatia ajali mbaya ya gari.Ndio- kifo ni mapenzi ya Mungu kama wengi tunavyoamini lakini kwa upande mwingine bado naamini kwamba rafiki yangu huyo angeweza kuwa hai hadi leo hii kama kusingekuwa na huo ujinga wa PF3. Baada ya kuchomolewa kwenye gari na wasamaria wema, alikimbizwa hospitali iliyokuwa karibu na eneo la tukio lakini kwa mshangao wa wengi, wauguzi wa hospitali hiyo walikataa kata kata kumpatia matibabu ya aina yoyote bila PF3. Marehemu by then alikua bado ana uwezo wa kuongea, ikabidi akimbizwe tena kwenye kituo cha polisi cha karibu, hadi mizengwe na maswali ya polisi inakwisha na PF3 kutolewa- hali ya marehemu ilishaanza kuwa mbaya na sadly alikata roho hatua chache kabla ya kuingizwa tena hospitali.

Tukio jingine limetokea tena juzi baada ya ndugu yangu mmoja kupata ajali ya gari, ilikua bahati kwamba mmoja wa waliokuwa wakimpeleka hospitali alikuwa aware na huo upuuzi wa PF 3 ikabidi mtu mmoja apitie kituo cha polisi kuchukua hiyo PF3 wakati majeruhi akikimbizwa hospitali. Polisi wanakuwa wepesi kutoa hiyo form kama utawaendea na majeruhi wako kituoni, lakini ukienda peke yako, maswali na mizengwe inakua mara mia na most of the time ili kuspeed up hilo zoezi unajikuta huna budi 'kuinunua'.

Hivi kweli kipande cha karatasi kinaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko uhai wa binadamu? Kwanini watu wasitibiwe tu kwanza kwenye cases za emergency then mambo ya paper works yafanyike baadae? Hivi utaratibu huu unafutwa pia na viongozi wa serekali wanapopata ajali?
 
ni lack of roho ya utu kwa upande wangu nionavyo mie...hata kama ni procedure za kufata hao ndugu zetu wa mahospitalini na polisi wakitetea..
wanijibu hoja hii umempelekea daktari mama yake ameponea chupu chupu ajalini akiwa hoi kweli atakuuliza pf3 ya mama iko wapi na siwezi kumpa huduma yoyote ya kidaktari mpaka ukalete PF3 yake??kweliiii??
plz jamani kuna some procedures yabidi ziangaliwe upyaaa
 
Ni kweli kunahitajika some kind of flexibility, na wakati mwingine nahisi ukifika huko hospitali kama huna hiyo PF3 wauguzi huko nao wanaona deal- kuna uwezekano wa kuvuta kidogodogo. Sidhani kama una kisu cha kueleweka na huna hiyo PF3 watakutosa.
 
Pole sana KKN,


Police Form #3
Mwenye uwezo wa kuiweka hiyo form hapa aiweke! Naona kuna umuhimu wa kuichambua Ilianzishwa kwanini? na lini?-Kwanini ipo?, Inamsaidia nani? na vipi?, Kwanini kusiwepo na mtandao utakaoondoa kero za PF#3, kwanini kero hizi zipo na hakuna aliyeipitia na kuondoa hizo kasoro?

Kama sijakosea Mheshimiwa J. Mwapachu alihaidi kupitia na kuchunguza sheria zilizopitwa wakati, pamoja na sera zinazoendana nazo, aidha alisema kuwa zitafanyiwa marekebisho. Naamini alitaka kuondoa sheria ambazo zililengwa kumlainisha na kumdhalilisha mtanzania wa kawaida wakati wa ukoloni. Naamini Sheria nyingi tumerithi na kwa namna moja au nyingine haiendani na Mtanzania alipofikia-pamoja na kuleta kero na maafa-Kwanini bado hizo kasoro zipo?

Kama hawajasikia Nyani Giladi basi kaibuka tena-Je Kuondoa kero na kasoro hizo mpaka kupitia tena katiba...........@!$^%#$^ shabash!!!! Nauliza. Je hakuna watu wa kupitia na kufanyia marekebisho hivo vijifomu? nafikiri ni wakati muafaka wa kuuliza.

Naomba kitengo cha mawasiliano cha Polisi Tanzania(rejea hapo juu) itueleze na kutuwekea hiyo fomu hapa. Au mnataka kishinikizo? Mnabisha?
 
Kila siku tunasikia waheshimiwa wamepata ajali na kukimbizwa hospitalini. Je nao wanaulizwa hio PF. 3 au inajazwa wakiwa kitandani? Tatizo la hizi sheria gandamizi ni kuwa haziwagusi wanaozisimamia kwa hiyo hawatambui adha yake. Sheria(?) kama hii ilitakiwa ifutwe mara moja. Haina nafasi katika mazingira ya sasa hivi! Kwa uelewa wa polisi wetu, hii hutumika kuwanyanyasa wasionazo. Ifutwe mara moja.
 
Hivi hamjui kuwa mnaishi kwa kudra za viongozi??? kama hamuamini mtaona hata hiyo pf3 haitarekebishwa labda tuandae list ya kero zetu kwa watakaogombea 2010

INAUMA KWELIKWELI
 
Msanii nimecheka kidogo! Imepunguza jazba, manake ulivosema inauma kwelikweli ni Kweli. Hii haitaji siasa za roketi au kurakabisha katiba. Mimi nimeleta hoja na maswali 'kuna umuhimu wa kuichambua Ilianzishwa kwanini? na lini?-Kwanini ipo?, Inamsaidia nani? na vipi?, Kwanini kusiwepo na mtandao utakaoondoa kero za PF#3, kwanini kero hizi zipo na hakuna aliyeipitia na kuondoa hizo kasoro?- nafikiri majibu ya hayo juu yatakuwa ni vigezo/kigezo kizuri cha kuendelea na mjadala huu. Hizo information wananchi wanazo jaza hapo ni- kwa manufaa ya nani: ya Bima,ya Hospitali, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, NSSF,REDET- ni nini hasa umuhimu wa kuwepo na fomu hii?
 
mkuu syloggist
nakubaliana nawe ktk maswali yako ila naona kuna wanaojua historia yake labda hawajatembelea thread hii.
ila na pressume ilianzishwa na wakoloni ili kuratibisha na kuadabisha watawaliwa wakorofi.
je ni kweli bado viongozi wetu ni wakoloni??

ila nasubiri kupata historia na sababu zake kutoka kwa members
 
Kila siku tunasikia waheshimiwa wamepata ajali na kukimbizwa hospitalini. Je nao wanaulizwa hio PF. 3 au inajazwa wakiwa kitandani? Tatizo la hizi sheria gandamizi ni kuwa haziwagusi wanaozisimamia kwa hiyo hawatambui adha yake. Sheria(?) kama hii ilitakiwa ifutwe mara moja. Haina nafasi katika mazingira ya sasa hivi! Kwa uelewa wa polisi wetu, hii hutumika kuwanyanyasa wasionazo. Ifutwe mara moja.

1.Ni sheria gani inayoendesha sera hiyo?
2.Je ni mpaka Katiba ibadilishwe kwa kasoro zilizopo?

Fundi Mchundo nakiri tupo pamoja kwenye hili lakini tukumbuke tunaweza rudi nyuma kidogo tukauliza ni nini? Incidental report? Accident report, Victims Report? ofcoz tunaelewa ni ya polisi Ina lengo gani-au hio ni nyeti nayo?
 
mkuu syloggist
nakubaliana nawe ktk maswali yako ila naona kuna wanaojua historia yake labda hawajatembelea thread hii.
ila na pressume ilianzishwa na wakoloni ili kuratibisha na kuadabisha watawaliwa wakorofi.
je ni kweli bado viongozi wetu ni wakoloni??

ila nasubiri kupata historia na sababu zake kutoka kwa members


Msanii
Sidhani kama viongozi wetu wakoloni!:D Nimesoma thread moja huko ya kurithi, na kama tumerithi, hiyo kutoka kwa wakoloni, tuwaitaje hawa? Wana nadharia gani?

Anyways maswali ni mengi na mie nitasubiri tu nione kama tutapata kahistoria. Asante mkuu.
 
Kingine kinachoniuma zaidi ni ukweli kuwa kuna wakati vituo vyetu vya polisi vilikuwa na uhaba wa makaratasi ikiwa pamoja na fomu zilizochapishwa tayari. Sitashangaa nikisikia kuwa kuna mgonjwa alifika akaambiwa aende kutoa copy kwenye kibanda jirani ndiyo ashughulikiwe! Nadhani wazo la SYLLOGIST na msanii ni zuri. Tutafute historia na makusudi ya fomu hii. Lakini wakati yakifanyika haya hatua zianze kuchukuliwa kuifanya hii fomu batili. Wanaumia wengi jamani!
 
Hivi wakuu hadi leo hii jeshi letu la polisi halina website? Jana nimejarbu kuitafuta bila mafanikio, nilitaka niwatumie maswali kadhaa kuhusu hiyo form.
 
Assuming Jeshi letu la Polisi na la kule Uganda havina tofauti kwenye mambo haya...


What is a PF3 form

The PF3 form is a document that is used by all victims of crime to document physical or other injury. The form is divided into two sections, to be filled in by the police – recording the reporting of the crime and the state of the victim and by the doctor to record any injuries.

Who Fills in the Form


The police generally require that the PF3 form must be filled in by government medical doctors. In total there are about eight government doctors in northern Uganda. These medical officers also have to cope with the huge need for health services in the region. The police do not accept that qualified medical personnel other than medical doctors may conduct the medical examination and sign the PF3 form.



Source:Amnesty.org:Lack of access to justice for female victims of sexual and gender-based violence in northern Uganda



Gonga hapa kwa zaidi...http://www.amnesty.org/en/alfresco_asset/6068628b-a2bb-11dc-8d74-6f45f39984e5/afr590052007en.html



Halafu tuendelee!
 
Hivi wakuu hadi leo hii jeshi letu la polisi halina website? Jana nimejarbu kuitafuta bila mafanikio, nilitaka niwatumie maswali kadhaa kuhusu hiyo form.

Yaani karibu na mie nilie kuhusu usumbufu wa Hizi PF3! Shabash

Kana-ka-Nsungu Kwanza hongera za cheo. Pili kwanini haujarudi hapa? Unaogopa polisi wewe! Tehe hehe -Utapata wapi PF3 baada ya mdundo?
Utani mbali, umefikia wapi na maswali kadhaa?
 
Yaani karibu na mie nilie kuhusu usumbufu wa Hizi PF3! Shabash

Kana-ka-Nsungu Kwanza hongera za cheo. Pili kwanini haujarudi hapa? Unaogopa polisi wewe! Tehe hehe -Utapata wapi PF3 baada ya mdundo?
Utani mbali, umefikia wapi na maswali kadhaa?

Asante Mkuu. Kuna mtu ameniahidi kunitafutia hiyo form then nitaiweka hapa tuichambue. Bado sina uhakika kama ni kweli jeshi letu la polisi halina website hadi sasa. The plan was to email my questions to them.
 
Kama nilivyopata kusema hapo awali,kuna vitu vingi sana nchi hii ambavyo vinahitaji majibu ya kina sana. hata askofu wa dodoma (RC) alirudia hili wakati ibada ya kumsimika askofu kule musoma. Hili la PF3 ni la muhimu sana kufanyiwa kazi
 
Asante Mkuu. Kuna mtu ameniahidi kunitafutia hiyo form then nitaiweka hapa tuichambue. Bado sina uhakika kama ni kweli jeshi letu la polisi halina website hadi sasa. The plan was to email my questions to them.


Kana-Ka-Nsungu

Mkuu nakuamini na hiyo,
Nilikuwa na wasiwasi,
Tumeishia wapi?

Asante.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom