Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 362
Mwanzoni mwa mwaka 2000 nilimpoteza rafiki yangu wa karibu kufuatia ajali mbaya ya gari.Ndio- kifo ni mapenzi ya Mungu kama wengi tunavyoamini lakini kwa upande mwingine bado naamini kwamba rafiki yangu huyo angeweza kuwa hai hadi leo hii kama kusingekuwa na huo ujinga wa PF3. Baada ya kuchomolewa kwenye gari na wasamaria wema, alikimbizwa hospitali iliyokuwa karibu na eneo la tukio lakini kwa mshangao wa wengi, wauguzi wa hospitali hiyo walikataa kata kata kumpatia matibabu ya aina yoyote bila PF3. Marehemu by then alikua bado ana uwezo wa kuongea, ikabidi akimbizwe tena kwenye kituo cha polisi cha karibu, hadi mizengwe na maswali ya polisi inakwisha na PF3 kutolewa- hali ya marehemu ilishaanza kuwa mbaya na sadly alikata roho hatua chache kabla ya kuingizwa tena hospitali.
Tukio jingine limetokea tena juzi baada ya ndugu yangu mmoja kupata ajali ya gari, ilikua bahati kwamba mmoja wa waliokuwa wakimpeleka hospitali alikuwa aware na huo upuuzi wa PF 3 ikabidi mtu mmoja apitie kituo cha polisi kuchukua hiyo PF3 wakati majeruhi akikimbizwa hospitali. Polisi wanakuwa wepesi kutoa hiyo form kama utawaendea na majeruhi wako kituoni, lakini ukienda peke yako, maswali na mizengwe inakua mara mia na most of the time ili kuspeed up hilo zoezi unajikuta huna budi 'kuinunua'.
Hivi kweli kipande cha karatasi kinaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko uhai wa binadamu? Kwanini watu wasitibiwe tu kwanza kwenye cases za emergency then mambo ya paper works yafanyike baadae? Hivi utaratibu huu unafutwa pia na viongozi wa serekali wanapopata ajali?