Huu unyanyapaa kuhusu korona usipochukuliwa hatua utaleta shida siku moja

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nimeshuhudia tabia hii mbaya siku moja nikiwa nateremka katika basi nikitokea Arusha.

Vijana wa stendi walianza kupiga mikelele miingi .".koronaa ...koronaa!"Nilihamanika kutokana na zomea zomea hiyo.

Jambo baya ni pale vijana wanapoona mtu mweupe. Wanafanya matendo ya wazi wazi ya ubaguzi huku wakizomea.Huu utamaduni ni mpya hapa kwetu na inapaswa udhibitiwe upesi.

Ni matumaini yangu serikali itakemea vikali na kuchukua hatua dhidi ya hawa vijana zomea zomea walioko stendi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya watu ambao utoto bado unawasumbua,
waliruka stage hao
 
Umetaja tu Arusha ulikotoka, lakini hujasema ulipofika na kupigiwa kelele za corona ni stendi ya mji gani
 
Duuh, malipo ni hapa hapa aisee, nakumbuka stori za waliokwenda huko majuu miaka ya huko gizani wanakuambia namna walivyokuwa wanabaguliwa. Ubaguzi ni jambo baya sana.
 
kibaravumba, Elimu duni mdau.... na bado hatujastaharabika.



_____________________________
" With or without religion, good people can behave well and bad people can do evil; but for good people to do evil - that takes religion.
 
Back
Top Bottom