huu unafiki wa kwenye taarabu unaanzia wapi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huu unafiki wa kwenye taarabu unaanzia wapi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bacha, Aug 24, 2010.

 1. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni mara nyingi kumkuta/kuwakuta watu wakiongea in a negative perception kuhusu nyimbo za taarabu mbele ya watu!utakuta mtu akisema, "ooooh unajua nyimbo za taarabu mimi sizipendi kabisa kwani zimejaa mambo ya kiswahili na yasiyo ya kistaarabu".

  Lakini cha ajabu ni huyu huyu mtu utamkuta anapokuwa kwenye mialiko ya harusi na sherehe mbailbali pindi inapopigwa miziki ya taarabu anaicheza vizuri na kwa ufasaha kabisa na wakati mwingine anakuwa na CDs au DVDs home.Sasa unashangaa hii ikoje?hebu nisaidieni wana JF mmeshakutana na hii hali?
   
 2. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,416
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Taarabu ni miziki ya mwambao na ni miziki ya kitanzania wala sio kosa kuipenda ni kama tu nyimbo nyingine mimi binafsi napenda sana muziki tena aina mbalimbali ikiwemo Bongo flava, nyimbo za dini, reggae, taarabu, mchiriku, Hip hop, R&B na aina nyingine nyingi tu za nyimbo nachoangalia haswa ni nafsi yangu kupenda hicho kinachopigwa wala sichagui kwa sanaaaa
   
 3. m

  mramba Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo anayeikandia taarabu ni akili mgando tu kwani hiyo ndo miziki ya kitanzania. Sasa hiyo yote anayosifia kama bongo flavor utakuta imeanzia Marekani, bolingo ni huko Kongo, rege ni huko Latin America, charanga ni huko Caribean countries n.k
  Wengine wanapenda ila kwa akili mgando zao wanafikiri huo ni uswahili kupenda taarab kumbe ni uzalendo wa kupenda vya kwako
   
 4. D

  Dick JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao waitwa wanafiki.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Taarabu asilia ni nzuri sana, za akina Issa Matona na the like, Lakini taarabu za Bongofleva wa Sasa hazina hata maana, hata kucheza wanashika p**bu na kurusha miguu! yo yooo nyiingi kama kunguru. Taarabu naskiliza sana za zamani-Mwenye Liblary ya taarabu za kitambo tuwasiliane
   
 6. msikonge

  msikonge Senior Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo umenena, taarabu za sasa sinatia kichechefuuuuuuuuuuuuu!
  Taarabu za enzi hizooooo zilitugwa kwa hekima na zilikuwa na mafundisho mazuri sana, za sasa zikijitahidi sana zitafunsisha ushoga tu!
  Usiwalaumu wanaozikataa, laumu wanaozitunga!
  Mimi binafsi nazichukia kubita kiasi taarabu za kisasa, na mwenzi wangu ndio haswa, ukita mgombane, fungulia tv kwenye chanel ya taarabu! Lakini za enzi hizoo nasipenda. Ukimuona mwanao mdogo anaanza kupendelea taarabu, uanze kumuweka sawa mapema!
  Huo ni ushauri wa bure!
   
 7. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 45
  hayo matusi ya njenje yametokea wapi, au ndio mafundisho ya kwenye taarab, inabidi kuwa makini, inawezekana huyo unaemuambia hivyo baba yako, au has smarter iQ (brain) several folds than you! Fikiria kwanza kabla ya kujibu! By the way muziki wa ki-Tz is not limited to taarab!
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nionavyo mimi, taarabu ni sanaa, kama sanaa nyingine. Kwa vile ni sanaa inayotumia lugha, basi tunaiita "fasihi" (literature) na imo katika tapo la "fasihi simulizi" (oral literature).

  Kama ilivyo sanaa yoyote ile, taarabu ni kitu kiko pale kwa ajili ya matumizi ya jamii. Sasa huwezi ukasema taarabu ni mbaya au ni nzuri kabla hujaitumia, au kabla haijawekwa kwenye matumizi, au kabla haijaimbwa, kama ambavyo huwezi kusema kisu au moto ni mbaya kabla havijatumika. Kisu ni kizuri kikitumika kukatia vitu tunavyotaka kukata, au kumenya, lakini kinaweza kuwa kibaya kikitumika kwa mfano kuulia. Vile vile moto ni mzuri ukikuivishia chakula, au ukikupashia joto maji ya kuoga, au ukikupa joto wakati wa baridi, lakini unakuwa ni mbaya ukikuunguzia nyumba, au ukitumika na watu kama akina Kibwetere kuteketeza wenzao, tena makanisani.

  Taarabu nayo ni nzuri ikitumiwa na watu wenye busara, kwa kuimba nyimbo ambazo hata mtu na heshima zake anaweza akaimba akiwa popote, au hata Rais anaweza kuunukuu kwenye hotuba zake, kama ambavyo Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi alivyowahi kumnukuu Siti binti Saad. Lakini taarab ni mbaya ikiwa itaimbwa na mtu domo kaya, asiyeona tabu kuharisha kwa kupitia mdomoni. Kuharisha ni kutokwa na kitu katika hali ambayo si ile ya kawaida. Tumbo likichafuka utaharisha, kwa maana ile haja kubwa itatoka bila ya mpangilio. Vile vile ubongo ukichafuka, basi maneno nayo hutoka bila ya mpangilio. Mtu akila uchafu, tumbo huchafuka naye huharisha. Vile vile mtu akinywa uchafu (mfano pombe), ubongo huchafuka, naye pia huharisha kupitia mdomoni, maana maneno yake hutoka bila ya mpangilio.

  Nilichogundua mimi ni kwamba taarab imevamiwa na watu wasio na ubongo uliotulia. Watu wasio na la kuwaambia watu zaidi ya kuchukua choko choko za mtaani na kuzifanya ndio maudhui ya simulizi zao, kama ambavyo fasihi andishi ilivyovamiwa na watu wasio na falsafa za kuipa jamii. Leo meza za magazeti zimejaa trashes zenye mambo ya kijinga, utakuta vijarida vimeandikwa uharo mtupu; sijui "Mtandao wa mapenzi", "Hadithi za Chumbani", "Shemeji Kula", n.k. Utashangaa leo, hata shuleni, katika somo la Kiingereza, kwa mfano, vitabu vingi vinavyosomwa vimeandikwa na watu wa Afrika ya Magharibi tu, akina Achebe, Armah, Sembene, n.k. Kutoka Afrika Mashariki yuko Ngugi (Kenya) na p'Bitek (Uganda). Wabongo wachache na vitabu vyao havisomwi. Hao niliowataja hapo juu, vitabu vyao vina mafundisho mazuri sana, lakini vinasomwa kwa kulazimishwa, kwa vile kuna mtihani.

  Tatizo ni kwamba, narudia, taarabu imevamiwa na watu wasio na asili nayo. Taarabu ina wenyewe, kama Marehemu Kolimba nilivyomsikia wakati fulani akisema C.C.M. ina wenyewe. Akina ustadhi na akina Al-Anissa ndio walikuwa wakiimba taarab, sasa hivi hata wa-kuja nao eti wanaimba. La kuimba hawana ni "Mambo iko huku eeeh mambo iko kule", basi!

  Kwenye taarabu watu wastaarabu walikuwa wanakwenda kutulia kupata burdani, leo walevi nao taarabu imekuwa yao. Kwenye taarabu kumeshaingizwa utamaduni wa pombe, na raha ya kilabuni, muziki uwe na fujo na ghasia na matusi ndio panakuwa na "raha". Hili ndilo tatizo la kwanza la kuharibiwa kwa taarabu, starehe ya waungwana imevamiwa na watu waso haya wala haiba.

  Pili, jamii nayo inalikaribisha hili. Ndio maana nasema, mafunza hustawi kwenye kinyesi. Pakiwa na kinyesi lazima funza watastawi. Taarabu chafu sasa hivi imeshamiri kwa sababu wachafuzi wa mazingira wamefanikiwa sana kuyachafua. Jamii imeoza. Jamii yetu si jamii tena bali ni kinyesi, na ndio maana mafunza, yale yanayoandika na kuimba upuuzi, ujinga, matusi, yanastawi. Unadhani kama pasingekuwepo na watu wanaopenda mambo ya kipuuzi yaandikwayo, au yaimbwayo, waandishi hawa na waimbaji hawa wangekuwepo? Au hata kama wangekuwepo, wangepata pa kuuzia uharo wao?
   
 9. msikonge

  msikonge Senior Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sina cha kuongeza! mtoa mada na mtukanaji naamini kama bongo zenu hazimo ktk hayo yaliyosema mtakuwa mmeelewa!
  kamanilivyosema, msiwalaumu wasioipenda taarabu waraumuni wanaotunga!
   
Loading...