Huu ulinzi anaopewa mgombea urais kwa tiketi ya CCM ni sawa kikatiba?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
809
Jana wakazi wa jiji la Mwanza walionja adha ya kutembelewa na amgombea kiti cha urais kupitia CCM mheshimiwa sana Dr. John Pombe Magufuli, barabara zilifungwa zaidi ya masaa matano.

Hakukuwa na gari inaruhusiwa kuelekea airport, maeneo ya Gold Crest barabara ilikuwa nyeupe hakuna chombo cha moto kiliruhusiwa.

Nilipatwa na wasiwasi sana na uelewa wangu ulikuwa kuwa huyu bado hajawa rais hivyo alitakiwa apite kama waziri wa ujenzi period!!!

Hivi hata mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo,UKAWA,UDP na vyama vingine atapewa nafasi sawa na huyu wa CCM ambaye tayari ameshaanza kampeni hata kabla ya pazia kufunguliwa?

Tafadhari mwenye uelewa zaidi yangu anisaidie.
 
Qn #2
Ndege ya serikali anayoitumia kuipanda kuzunguka nayo ni sawa kikatiba??
 
Jiongeze na wewe ndugu. Embu zunguka hata vijiwe 10 kwa sample yako alafu uliza rais ajaye ni nani Alafu leta majibu humu. Ukishaleta majibu jiulize sasa anastahili ulinzi au la?
 
TUFIKIRI PAMOJA, TUSEME PAMOJA NA TUTENDE PAMOJA

SEMA:-
NIMECHOKA KUUAWA, NIMECHOKA KUIBIWA, NIMECHOKA KUTESWA NA KUNYANYASWA NDANI YA
NCHI YANGU, NIMECHOKA KUITWA MPINZANI NIMECHOKA KUDHARAULIWA.

SITAKI TENA UTUMWA NDANI YA NCHI YANGU, SASA NI MIMI NA TANZANIA HAPANA CCM OCTOBA 2015.

msema yote

Magufuli ni haramu hata kwa CCM.Magufuli niliweka uzi hapa hana tofauti na wale viongozi wa afghanistani na somalia waliochaguliwa nje ya nchi na kulazimishwa kwa wananchi.Ulinzi wao ni kuliko wa bank kuu.
 
Qn #2
Ndege ya serikali anayoitumia kuipanda kuzunguka nayo ni sawa kikatiba??
Hivi waziri haruhusiwi kutumia ndege ya serikali? Magufuli amekuwa akipatiwa ulinzi na serikali tofauti ma mawaziri wengine muda mrefu sana tangia wakati wa serikali ya Mkapa na kisha serikali ya JK
 
Hivi waziri haruhusiwi kutumia ndege ya serikali? Magufuli amekuwa akipatiwa ulinzi na serikali tofauti ma mawaziri wengine muda mrefu sana tangia wakati wa serikali ya Mkapa na kisha serikali ya JK
Angeruhusiwa pia kutumia akienda kuvist ka small house kake.
 
kisheria ukishateuliwa kuwa mgombea urais ukathibitishwa na tume unatakiwa kupewa ulinzi ila kwa mazingira aliyopita magufuli inabidi apewe ulinzi kwa usalama wake
 
kisheria ukishateuliwa kuwa mgombea urais ukathibitishwa na tume unatakiwa kupewa ulinzi ila kwa mazingira aliyopita magufuli inabidi apewe ulinzi kwa usalama wake

Sasa mkuu ni siku gani tume ya uchaguzi imempitisha kua ni mgombea halali?Acha upoyoyo NEC aijatoa form na cheti kwa mtu yeyeto kama mgombea urais 2015
 
Hivi waziri haruhusiwi kutumia ndege ya serikali? Magufuli amekuwa akipatiwa ulinzi na serikali tofauti ma mawaziri wengine muda mrefu sana tangia wakati wa serikali ya Mkapa na kisha serikali ya JK
mkuu hawa viroboto watahangaika sana lakini hata hivyo mwishoni itabidi wakubaliane tu na hali halisi kuwa magufuli ndo rais wao ajaye baada ya Kikwete.
 
Ukawa wakimtangaza mgombea wao wa urais atapewa ulinzi kama mapalock? Hawa askari na walinzi wa nchi hii wanalipwa kwa kodi zetu iweje ulinzi wapewe mgombea wa ccm tu? Nauliza tu jamani.
 
mkuu hawa viroboto watahangaika sana lakini hata hivyo mwishoni itabidi wakubaliane tu na hali halisi kuwa magufuli ndo rais wao ajaye baada ya Kikwete.
Pia nadhani kuna watu hawaelewi kwamba ndege za serikali zinakodiwa. Kwamba unaweza kukodi ndege ya serikali kwa wakala wa ndege za serikali.
 
Ukawa wakimtangaza mgombea wao wa urais atapewa ulinzi kama mapalock? Hawa askari na walinzi wa nchi hii wanalipwa kwa kodi zetu iweje ulinzi wapewe mgombea wa ccm tu? Nauliza tu jamani.
Nao watapewa tu mkuu lakini huwa hawataki wanataka kutumia mabaunsa!
 
Sasa mkuu ni siku gani tume ya uchaguzi imempitisha kua ni mgombea halali?Acha upoyoyo NEC aijatoa form na cheti kwa mtu yeyeto kama mgombea urais 2015
wewe ndio poyoyo umesoma na kuelewa nilichoandika au unarukia tu mambo kuna sehemu nimeandika kathibitishwa na tume
 
Pia nadhani kuna watu hawaelewi kwamba ndege za serikali zinakodiwa. Kwamba unaweza kukodi ndege ya serikali kwa wakala wa ndege za serikali.
mkuu wengi humu ni misukule tu. uwezo wao ni mdogo sana wa kuelewa mambo na mara nyingi wananedeshwa na hisia tu.
 
Back
Top Bottom