Huu ugonjwa wa vipele unasumbua sana

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Jul 17, 2018
713
1,181
Wakuu kuna ndugu yangu anasumbuliwa na vipele vidogo vinamuwasha sana vipo kichwani kwenye nywele akikuna unatoka unga mweupe, vipo kifuani mgongoni makwapani.

Alienda hospital mara 3 akaambiwa fungasi ya damu lakini akitumia dawa inatulia then inarudi upya

Msaada

IMG_20200802_120924.jpg
 
Matibabu ya fungus ni ya muda mrefu, anaweza awe kwenye tiba kwa miezi sita. Pamoja na hizo za kunywa angepata na dawa za kupaka na nywele aondoe zote.

Asishirikiane taulo na mtu mwingine, nguo zake afue na sabuni na aanike juani pia apige pasi.

Ajikaushe vizuri baada ya kuoga.
 
hakikisha kila siku asubuhi unakunywa kijiko kimoja cha unga wa majani ya mlonge changanya na maji kabla hijala chohcote.

usile nyama kwa wingi, masoda, chai, bia etc. kula sana matunda mbogamboga, vitu visivyokobolewa njoo unitafute baada ya mwezi mmoja unipe buku teni ya pongezi.

utaangahika bure usipojali ninachokuambia mkuu
 
Hizo ni scabbies wala siyo fangus. Nenda pharmacy nunua sawa inaitwa Scaboma beinyake ni kuanzia 8,000 mpaka 15,000. Tumia wiki mbili. Usipopata nafuu nicheki nikuelekeze kwa mtaalam namba moja wa magonjwa ya ngozi. Fata maelekezo ya pharmacist. Ukipata nafuu usiache kuleta mrejesho.
 
Hizo ni scabbies wala siyo fangus. Nenda pharmacy nunua sawa inaitwa Scaboma beinyake ni kuanzia 8,000 mpaka 15,000. Tumia wiki mbili. Usipopata nafuu nicheki nikuelekeze kwa mtaalam namba moja wa magonjwa ya ngozi.
Fata maelekezo ya pharmacist. Ukipata nafuu usiache kuleta mrejesho.
Sawa inaitwa scabboma
 
Ushauri murua
 
Wakuu kuna ndugu yangu anasumbuliwa na vipele vidogo vinamuwasha sana vipo kichwani kwenye nywele akikuna unatoka unga mweupe, vipo kifuani mgongoni makwapani.

Alienda hospital mara 3 akaambiwa fungasi ya damu lakini akitumia dawa inatulia then inarudi upya

MsaadaView attachment 1524731
This is not fungus. Hii ni a topic dermatitis with acne.

Matibabu yake
1. Cetirizine tabs 10mg od for 10 days
2. Gentrisone cream apply bd 10 days
3. Doxycycline caps 100mg od for 28days
4. Epuka animal protein food and it's products kipindi chote cha matibabu.
Tumia Vaseline mafuta ya kupaka yasiyo na harufu.
Nywele anyoe kabisa.

Nitafute inbox baada ya wiki moja unambie progress yake
 
Hizo ni scabbies wala siyo fangus. Nenda pharmacy nunua sawa inaitwa Scaboma beinyake ni kuanzia 8,000 mpaka 15,000. Tumia wiki mbili. Usipopata nafuu nicheki nikuelekeze kwa mtaalam namba moja wa magonjwa ya ngozi.
Fata maelekezo ya pharmacist. Ukipata nafuu usiache kuleta mrejesho.
Siyo scabies hii. Scabies inakaa kwenye mikunjo mainly. Mfano kwenye vidole. Kwapani, miguuni nyuma ya goti nyuma ya sikio nk
 
kila mwili wa mtu huwa unamadudu, mafungus mabacteria na kila takataka maana hata kama upendi utayavuta ukipita karibu na barabara utayapata kwa uzembe wa mtu mwingine.

Dawa niliyokupa sio dawa tu bali n kuingiza vitu sahihi ili kuyacontrol hayo majamaa yasikuletee sio tu upele bali hata homa na kila aina ya ugonjwa.
 
ndugu yako au ww

Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa watu wa JF kwani ningekuwa mimi ningeshindwa kuandika kama ni mimi?, kuna anaenijua humu?, ushawahi kuona nandika uzi mara kwa mara kusema ntaona aibu...okay basi tufanye ni mimi aya tuendelee kusaidiana
 
Matibabu ya fungus ni ya muda mrefu, anaweza awe kwenye tiba kwa miezi sita. Pamoja na hizo za kunywa angepata na dawa za kupaka na nywele aondoe zote.

Asishirikiane taulo na mtu mwingine, nguo zake afue na sabuni na aanike juani pia apige pasi.

Ajikaushe vizuri baada ya kuoga.
Unashauri atumie dawa gani..kwasababu akienda hospital anagewa ambazo hazifiki miez 6
 
Siyo scabies hii. Scabies inakaa kwenye mikunjo mainly. Mfano kwenye vidole. Kwapani, miguuni nyuma ya goti nyuma ya sikio nk
nilishawahi kupata scabies nilihangaika miezi ya kutosha kuja kukutana na scaboma haikuchukua hata wiki kila kijidudu kimeshasepa na mapere yakaisha.

ile kitu sio mchezo
 
hakikisha kila siku asubuhi unakunywa kijiko kimoja cha unga wa majani ya mlonge changanya na maji kabla hijala chohcote.

usile nyama kwa wingi, masoda, chai, bia etc
kula sana matunda mbogamboga, vitu visivyokobolewa njoo unitafute baada ya mwezi mmoja unipe buku teni ya pongezi.

utaangahika bure usipojali ninachokuambia mkuu
Shukran
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom