huu udhalilishaji ndio ulisababisha mtu akajipiga kiberiti kule tunisia

Inaumiza sana. Ni kweli hata yale ya kule Tunisia yalianza hivi hivi, ipo siku watajua ni nini kilimtimua Zine madarakani. Huo ni ukandamizaji na udhalilishaji wa hali ya juu. Ni vyema wasamaria wangemtetea

Hakika wa Tz tunachotafuta tutakipata muda siyo mrefu: wetu wengi humu janvini wanashabikia mambo yanayoendana na kanuni za maisha, huyo aliyepigwa picha akikamatwa na wanamgambo wa Jiji ni mamantilie aliyekuwa akiuza chakula chake barabarani- kwa mawazo mengi ya wana jf ameonewa. tukiwa na mawazo kama haya hatujitendei haki, kuuza chakula barabarani ni uvinjaji wa sheria lukuki za taifa, kwa sisis tuliobahatika kujua kusoma na kuandika tunapaswa kupinga ufanyabiashara holela kwa unaleta matatizo mengi katika jamii ikiwemo usambazaji wa magonjwa kama kipindipindu na kuhara. kazi kwenu.
 
Hapo wamezidi. Kina mama TGNP, TAWLA, haki za binadamu mnaona ni sawa mwanamke kudhalilishwa hadi maziwa/matiti na mapaja kuonyeshwa hadharani wakati mtu anatafuta riziki yake? Jiji hivyo ndivyo mliyowatuma mgambo wenu kufanya kazi hiyo? angekuwa mkeo baada ya wewe kustaafu kazi/umgambo ungejisikiaje? Hatua zimechukuliwa?
Tafakari, chukua hatua,
The day will come................ tena very soooon
 
HAYA YOTE KISA ANAKUJA WAZIRI
HUU NI UNYAMA NA SI UBINADAMU
Tuiombee sana nchi yetu
 
Back
Top Bottom