huu udhalilishaji ndio ulisababisha mtu akajipiga kiberiti kule tunisia

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
3.JPG
 
Hata yule jamaa alikuwa anauza mboga mboga wakamchukulia toroli lake,yanaanzaga hivihivi.
 
Hata yule jamaa alikuwa anauza mboga mboga wakamchukulia toroli lake,yanaanzaga hivihivi.

halafu jamaa alikuwa amemaliza chuo akawa mtaani tu anauza mboga ....kuna siku kitanuka ..mambo kama haya wanatakiwa kuyatafutia alternative mapema sio kulipana tu mwadowans
 
Very sad... Halafu mafisadi wanapita vip lounge pale airport na kwenda ikulu kuangalia premier league
 
Inaumiza sana. Ni kweli hata yale ya kule Tunisia yalianza hivi hivi, ipo siku watajua ni nini kilimtimua Zine madarakani. Huo ni ukandamizaji na udhalilishaji wa hali ya juu. Ni vyema wasamaria wangemtetea
 
Yaani kutengeneza uadui na jamii kwa sababu ya pesa???!!! Kule kwetu kuna ardhi kubwa sana yenye rutuba na hali ya hewa safi sana, NITARUDI NYUMBANI kuliko kukaa mjini kutumikia MAFISADI
 
Kwa kweli huyu dada walimdhalilisha kupitiliza khaa....Serikali ina wajibu mkubwa wa kuliangalia suala hili kwa macho mawili, Tanzania siyo kisiwa ambacho hakioni mambo yanayotokea upande wa pili, ya Tunisia yasije yakajirudia. Na kwa nini tufike huko, kweli wamekosa ufumbuzi wa suala la wafanyabiashara ndogondogo? Na hao mgambo wetu hapo kifikra washajiona FBI!
 
Back
Top Bottom