GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,409
- 108,516
Wakati huku Afrika ( hasa nchini Tanzania ) Wachina pamoja na Serikali yao wakionekana ni Watu Wema na Marafiki wazuri kwa Sisi Waafrika tayari Wachina wameanza Kutuonyesha Waafrika ile Rangi yao halisi iliyomo Mioyoni mwao na pengine hili sasa litakuwa Fundisho kwa Mamlaka zetu.
Habari ikufikie hapo hapo ulipo kwamba kwa muda wa Siku Tatu nzima sasa Waafrika ( Watanzania wakiwemo ) waishio Mji wa Guangzhou ( Gwanzuu ) huko nchini China wameanza Kunyanyasika kwa Kubaguliwa na Wachina huku wakifukuzwa katika Nyumba zao wakidaiwa Kusambaza COVID-19.
Na taarifa ya muda si mrefu tu inaeleza kwamba Waafrika wengi hivi sasa wa huo Mji wanalazimika Kulala Mabarabarani huku wakiteseka na Baridi na wana Mazingira mabaya wakati wengine wakipigwa na Wachina na Kufukuzwa wakishutumiwa kuwa Wao ndiyo wanaeneza na wamepeleka huko Kirusi.
Tayari Serikali za Kenya na Afrika Kusini zimeanza Kulaani na Kuhoji hili hivyo basi nategemea haraka sana hata Serikali ya Tanzania nayo kwa kupitia Balozi wake huko watatoa Tamko na ikiwezekana hata Kulaani ila mkae mkijua ya kwamba hivi sasa Waafrika wenzetu Wananyanyasika huko China.
Watu tukiwa tunasema kuwa Wachina siyo Watu Wema na hawana Utu wala Huruma kwa Waafrika muwe mnatuelewa. Ila yawezekana hatutaeleweka katika hili kwakuwa tu hapa Kwetu Wachina wanaonekana ni Mungu wa Pili na Mshirika mwema wa Maendeleo na Misaada kwa Mamlaka.
Kwa Habari Kamili na za ndani kabisa juu ya Taarifa hii tembelea upesi Gazeti la Mtandaoni la The CITIZEN japo hata Radio One nao katika Taarifa yao ya Kutwa nzima ya Saa 4 Kamili hadi Saa 4 na Robo wameigusia pia katika Habari za Kimataifa. Tuwasaidieni Waafrika wenzetu huko Guangzhou.
Nawasilisha.