Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka ni unafiki, ujinga na upumbafu uliokithiri!

Unstoppable;

Ninanukuu Kauli ya Dr Ulimboka baada ya Kurudi Nchini amesema "apewe muda awe na familia yake na ukweli ya yote aliyofanyiwa ni yeye tu ndiye anayeujua"Mwisho wa Nukuu.

Kwa kauli hiyo inatia shaka kidogo kwamba bado Dr Ulimboka anasimamia yale aliyoyasema siku ya kwanza baada ya shambulio,Kama angekuwa anayasimamia hayo jibu lilikuwa rahisi sana kama unavyosema kwamba angethibitisha tu kwa kusema nilishaeleza yaliyonikuta na wote mnayajua na isingekuwepo hoja ya kwamba ni yeye tu ndiye anayejua kilichomtokea,Hii inafanya wengine tuamini alichoeleza baada ya kipigo kile yeye mwenyewe hakiamini na siyo ukweli na ndiyo maana ukweli ni yeye tu anayeujua.Na hili linawezekana hasa kutoka na athari za kipigo au amesema hivyo kama mbinu ya kujipanga na kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuthibitisha yale aliyoyasema ndiyo hayo hayo.

Tafadhali naomba apewe muda ajipange na kama alivyoahidi nafikiri atatimiza ahadi,shauku yetu yakutaka kujua zaidi yasitufanye tusahau kuna maswala mengi kwake ya kuzingatia hasa baada ya yaliyomkuta na kuyapatia majibu likiwemo la ulinzi na usalama wake.
 
Last edited by a moderator:
Tanzania ushabiki mwingi! Huwa wanapenda vitu vipya kila siku na kutupa vya jana! Watanzania wanapenda 'umbea' na 'majungu' hapo humtoi! Ila kushinikuza, kufikiri kwa nguvu na kuamua kwa busara wengi wao hawajui. Binafsi yangu naungana nawe kwa 100%.

nimekusoma mnama!
 
baluhya M.

Wewe ndio unafahamu leo mkuu wangu? Sisi ni wanafiki kwa asili..na hata huyo Ulimboka mwenyewe ni mnafiki vile vile maana yupo ktk uzao wa wanafiki. Na ndio maana kashindwa kuwataja mahasidi wake kwa madai ya kwamba wakati ukifika atawataja.. Hii lugha tumeisikia kwa JK akishindwa kutangaza majina ya wauza Unga au hata kupambana na Ufisadi isipokuwa kwa kutoa hahadi za uongo. Unafiki upo hadi watu wa chini wanaotuchonganisha na wake zetu, waume zetu watoto zetu, ndugu zetu na kadhalika.

UNAFIKI ni sehemu ya maisha ya Mtanzania..
 
Last edited by a moderator:
Wewe ndio unafahamu leo mkuu wangu? Sisi ni wanafiki kwa asili..na hata huyo Ulimboka mwenyewe ni mnafiki vile vile maana yupo ktk uzao wa wanafiki. Na ndio maana kashindwa kuwataja mahasidi wake kwa madai ya kwamba wakati ukifika atawataja.. Hii lugha tumeisikia kwa JK akishindwa kutangaza majina ya wauza Unga au hata kupambana na Ufisadi isipokuwa kwa kutoa hahadi za uongo. Unafiki upo hadi watu wa chini wanaotuchonganisha na wake zetu, waume zetu watoto zetu, ndugu zetu na kadhalika. UNAFIKI ni sehemu ya maisha ya Mtanzania..
Nakubaliana na wewe kuhusu sisi kuwa wanfiki wakubwa.However nadhani tumpe Uli muda kidogo kabla hatuja conclude kuwa ni a coward.Nina uhakika maamuzi atakayoyafanya ni lazima awashirikishe watu wengi na kujipanga vyema.And that might take a little more time than we would've liked it to be or anticipated.

Nafahamu ulikuwa ukipinga mgomo wa madaktari.Lakini yaliyompata Ulimboka yanaweza kumpata mwanaharakati yeyote anayekwenda kinyume ama kupingana na serikali.

Ni matendo ya kinyama yenye kufanywa na serikali za kikatili na zenye kugandamiza demokrasia.
 
Achaneni na huyo jamaa c ameshapona,mbona wale waliokufa kutokana mgomo wake hamwazungumzii?kila kukicha ulimboka!ulimboka! Mnampa umaarufu tu.
 
NMkuu wangu tumpe muda tusimpe muda ni HULKA ya Mtanzania kufanya unafiki. Mbona Dr.Slaa alipopata list of shame na Richmond hakusubiri mtu, Zitto alipata habari za Buzwagi alizimwaga pale pale japokuwa unafiki wetu ndio ulizima kesi zile.

No matter what haya yote ni upepo yatapita JK mwenyewe alisema na kuna ukweli mkubwa sana kuhusu hoja zetu kuwa ni sawa na upepo. majuzi tu hoja ilikuwa wizara ya nishati na madini kina Ngeleja na Maige, leo hii wamesahaulika. Tunasubiri ya Ulimboka ambaye kesho tutamwona mitaani akidunda kama hakutokewa na kitu na narudia kusema if his life was in danger asingerudi nchini, maisha matamu mkuu wangu. Wewe nambie karudi nchini ili iweje?. kweli mtu unaweza jitumbukiza ktk kinywa cha Simba hivi hivi tu ndio nini ushujaa!.Think large, something is going on!
 
Achaneni na huyo jamaa c ameshapona,mbona wale waliokufa kutokana mgomo wake hamwazungumzii?kila kukicha ulimboka!ulimboka! Mnampa umaarufu tu.
Maneno kama ya wale wanaotumwa kutesa na kuuwa inthe name of national security and patriotism.No wonder unaongea ***** huku ukijiita eti Mtz mzalendo.Give me a break before I throw out...
 
Kila mtu analaumu mwenzake kisa. ili aonekane yeye bora kasema, I mean we are all ******
 
NMkuu wangu tumpe muda tusimpe muda ni HULKA ya Mtanzania kufanya unafiki. Mbona Dr.Slaa alipopata list of shame na Richmond hakusubiri mtu, Zitto alipata habari za Buzwagi alizimwaga pale pale japokuwa unafiki wetu ndio ulizima kesi zile.

No matter what haya yote ni upepo yatapita JK mwenyewe alisema na kuna ukweli mkubwa sana kuhusu hoja zetu kuwa ni sawa na upepo. majuzi tu hoja ilikuwa wizara ya nishati na madini kina Ngeleja na Maige, leo hii wamesahaulika. Tunasubiri ya Ulimboka ambaye kesho tutamwona mitaani akidunda kama hakutokewa na kitu na narudia kusema if his life was in danger asingerudi nchini, maisha matamu mkuu wangu. Wewe nambie karudi nchini ili iweje?. kweli mtu unaweza jitumbukiza ktk kinywa cha Simba hivi hivi tu ndio nini ushujaa!.Think large, something is going on!
Nakubaliana kwa kiasi na unayoyasema mkulu.Lakini natofautiana na wewe unaposema alitakiwa asirudi nchini.Hata ile siku aliyohojiwa akiwa hoi na baadaye kupelekewa airport,nakumbuka alisema atarudi?ila angependa damu yake isimwagike bure.The guy played his part big time.Lakini sisi nidhamu yetu ya woga ndo inakwamisha haki kutendeka.Hivi mkuu umeshawahi kujaribu kujiweka kwenye nafasi yake?ebu jaribu kidogo halafu useme ingekuwa wewe ungefanyaje.Tuanzie hapo mkuu.
 
Achaneni na huyo jamaa c ameshapona,mbona wale waliokufa kutokana mgomo wake hamwazungumzii?kila kukicha ulimboka!ulimboka! Mnampa umaarufu tu.
 
baluhya M.

Watanzania tumeisha kabisa. Angalieni watu wanaosotea rumande je ni wangapi wana makosa ya kweli? Angalieni uongozi wa nchi yetu ni nani kiongozi wa kweli? Angalieni matibabu yanayotolewa ni nani anatibiwa kweli? Ukweli tunao tena tunadai tupewe mwingine. Je ni upi? Dr. Ulimboka alitekwa, kuteswa, na kutupwa kama mnyama. Je mkenya angekuja kumtenda hivyo kwa kuwa alikuwa anatetea Kenya?

Tu wanafiki tunaotukana viongozi wa kweli. Angalieni matusi wanayopewa viongozi wa CDM hapa jamvini eti wamechangisha pesa toka kwa watanzania masikini. Ni nani aliyesababisha umaskini wetu? Tumejaa ujinga na woga. Kuliko mtu atetee haki yetu wote ni afadhali tumwue ili mafisadi waendelee kushiba.

Jamani angalieni watoto wetu, mama zetu wanavyokufa kwa kujifungua na kuonewa kwa kunyang'anywa haki zao. Kila tone la damu linalomwagika linaimwagikia Tamzamia. Huyu Kikwete na wenzake atajalaumiwa na wajukuu wake mwenyewe. Watakuwa navyo lakini hawataweza kuvila kwani watauawa na majambazi ambao taifa hili linawatengeneza kila kukicha. Ukimnyima mtoto shule unategemea nini?

Hii mifisadi inatumaliza na watoto wetu. Huyu rais na viongozi wengine wanaotumia billions kujisafirisha dunia nzima wanatumaliza. Hatuchukui hatua ila kulalama. Ulimboka alikuwa anatututea hatuoni kwani amcho yetu yamefumbwa na upuuzi, ujinga, ufisadi, ubinafsi na mengine.

Tugeuke tujitetee. Hawa polisi wanatumia kodi zetu kutuua na bado tunawachekea. Tufike wakati tufundishane adabu na ukweli.

Tuwaondoe hawa CCM Tanzania imefika ukingoni kabisa. Kadiri tunavyojidanganya ni kadiri hiyohiyo tunazidi kuangamia. Na hatimae tuache kuchezea uhai wa Dr. Ulimboka. Ni binadamu na anahisi maumivu kama wewe na mimi. Familia yake mlindeni kwa nguvu zote wala msikubali yeyote ajue aliko.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana kwa kiasi na unayoyasema mkulu.Lakini natofautiana na wewe unaposema alitakiwa asirudi nchini.Hata ile siku aliyohojiwa akiwa hoi na baadaye kupelekewa airport,nakumbuka alisema atarudi?ila angependa damu yake isimwagike bure.The guy played his part big time.Lakini sisi nidhamu yetu ya woga ndo inakwamisha haki kutendeka.Hivi mkuu umeshawahi kujaribu kujiweka kwenye nafasi yake?ebu jaribu kidogo halafu useme ingekuwa wewe ungefanyaje.Tuanzie hapo mkuu.
Well I have my doubts..Kama usalama wa Taifa wangemtaka nakuhakikishia ndege isingeruka labda na maiti na wala asingerudi nchini na kupokelewa Airport kwa kutanguliwa na taarifa kwamba Ulimboka anarudi nchini..Come on bro kwani taabu gani kutaja majina ya wahusika ikiwa Kubenea aliweza kutaja? anasubiri nini mwezi uandame?.
- Mimi naweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo.
 
Ulimboka alisema na kutaja ndio lakini kumbuka wakati ule alikuwa na maumivu na hata ongea yake ilitia shaka kama kweli mentally yupo okey au la! aliporejea akiwa Airport aliahidi kuwa ataanika wazi kila kitu sasa hapo ndipo tunataka aseme akiwa na akili zake timamu ataje majina mazingira na kila kilichotokea na pia aombe utaratibu wa kisheria uanze dhidi ya watekaji wake sasa yeye kaja anajificha haongei what follows???

Wewe hapo unapoongea ziko timamu?
 
This is the very mother of all truths that a majority of us wont be comfortable to put up with, unfortonutely it begins with me! ..............mercy
 
Well I have my doubts..Kama usalama wa Taifa wangemtaka nakuhakikishia ndege isingeruka labda na maiti na wala asingerudi nchini na kupokelewa Airport kwa kutanguliwa na taarifa kwamba Ulimboka anarudi nchini..Come on bro kwani taabu gani kutaja majina ya wahusika ikiwa Kubenea aliweza kutaja? anasubiri nini mwezi uandame?.
- Mimi naweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo.
tuko very exposed to the outside world now hawawezi tu kumwua hivihivi tena baada ya public kuwa aware of what's going on.

Hivi ni kweli hajawataja wahusika?ama taarifa zilizopo hazitoshelezi kujuwa wahusika ninani?awataje ili nani afanye nini?ni muhimu ajipange,tumpe muda.

What we need is justice to prevail.There is no justifications whatsoever of whatever went down.

Sisi ni binadamu,vitendo alivyofanyiwa lazima vimwathiri kisaikolojia,na anajuwa kuwa adui na serikali ni hatari kupindukia,serikali uishtaki wapi?labda kwa wananchi.

Na wananchi watafanyaje?maybe kwenye sanduku la kura watareact,na hilo ni 2015.Mwanahalisi limefungiwa kwa kusema haya ambayo mnataka yeye aseme,wananchi wamefanyeje?Si kuna wanaokosa vipato?Kubenea akale wapi?do you really care?ama tunarudi kulekule kwamba ndo tulivyo?sisi ni wabinafsi na wanafiki hadi inachefua.
 
Mkuu baluhya M, ulichokiandika ni ukweli tupu na nakuunga mkono!
Lakini tambua kuwa pamoja na hoja zooote na hasira zoote wana JF wanazoonesha hapa, hata huu uzi wako utapita hivihivi! Natamani kama tungetoka na uamuzi wa nini kifanyike juu ya hili.
 
tuko very exposed to the outside world now hawawezi tu kumwua hivihivi tena baada ya public kuwa aware of what's going on.

Hivi ni kweli hajawataja wahusika?ama taarifa zilizopo hazitoshelezi kujuwa wahusika ninani?awataje ili nani afanye nini?ni muhimu ajipange,tumpe muda.

What we need is justice to prevail.There is no justifications whatsoever of whatever went down.

Sisi ni binadamu,vitendo alivyofanyiwa lazima vimwathiri kisaikolojia,na anajuwa kuwa adui na serikali ni hatari kupindukia,serikali uishtaki wapi?labda kwa wananchi.

Na wananchi watafanyaje?maybe kwenye sanduku la kura watareact,na hilo ni 2015.Mwanahalisi limefungiwa kwa kusema haya ambayo mnataka yeye aseme,wananchi wamefanyeje?Si kuna wanaokosa vipato?Kubenea akale wapi?do you really care?ama tunarudi kulekule kwamba ndo tulivyo?sisi ni wabinafsi na wanafiki hadi inachefua.
Mkuu wangu unaishi dunia gani?.. Kolimba alikufa vipi? Mwaikambo, Chifupa, na hata majuzi jaribio la Mwakyembe. Kote kuna watu ama system ilihakikisha vinafanyika na hakuna cha Amnesty Int. wala mjomba wake.

Yule kapewa warning tu na hutamsikia tena ndio imetoka. Usifanye mchezo na system na wala sintomshauri lolote zaidi maana sisi wenyewe ni wanafiki. Hakuna kitu Justice nchini mkuu wangu wewe unaishi wapi?.. Mtu unakwenda kwa wakili (lawyer) anakupa bill ambayo ina include mgao wa Hakimu, sasa kweli unategemea kutakuwa na haki?.. Kila mtu Tanzania mwizi, fisadi na Mnafiki ni utamaduni unaokubalika na Ulimboka alitaka kuziba riziki za watu. Tusahau ya Ulimboka mwacheni ajipange kuanza maisha upya kama Mwakyembe - Upepo huu utapita.
 
Back
Top Bottom