Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka ni unafiki, ujinga na upumbafu uliokithiri!

Nani hasiyejua kwamba Watanzania Mnaongoza Kwa Kupiga Mdomo..utendaji Zero...Ndio Hulka iyoo Kwisha Habarii...

Vitu vingapi vikubwa zaidi ya Ulimboka vimepita pasi kujua hatima yake ? Tume nGapi zimepita Pasi Majibu...Badilikeni

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nakuunga mkono mkuu, umeelezea kwa hisia kali sana mpaka inatiisha huruma. Sisi watanzania sijui ni lini tutanyanyuka na kutembea naona bado tunatambaa tu kila miaka inavyozidi kwenda!!!!! Hatuendelei, tutabaki na upumbavu wetu ingali haki zetu tunazijua lakini kamwe hatuwezi kuzipigania.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nani hasiyejua kwamba Watanzania Mnaongoza Kwa Kupiga Mdomo..utendaji Zero...Ndio Hulka iyoo Kwisha Habarii...

Vitu vingapi vikubwa zaidi ya Ulimboka vimepita pasi kujua hatima yake ? Tume nGapi zimepita Pasi Majibu...Badilikeni

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Vingi sanaaaaaa havihesabiki, inasikitisha kwakweli. Hivi ni nani atakua mkombozi wa watanzania???!!!!
 
ukiona mimi Edson nimekugongea ''like'' ujue umeongea point sana....safi sana na ukweli mtupu
 
Last edited by a moderator:
'Mimi na Mwenyezimungu pekee ndio tunaojua ukweli wa kutekwa kwangu'-Dkt Ulimboka. Haya maneno kayasema mchana kweupe siku aliporejea toka Matibabuni Afrika ya Kusini sasa tusaidieni nyinyi mnaojifanya mnajua ukweli je ndo Mungu wa Ulimboka alosema anaujua ukweli?
 
kWANI WATANZANIA WOTE NDIO TUNA MAMLAKA YA KUCHUKUA HATUA MAELEZO YAKE ? UNAFIKI UNATOKA WAPI? ARUDIE KUWEKA MSISTIZO...NATHAN UKISEMA WATANZANIA UNAKOSEA TUANZE NA SERIKALI NA POLICCM!!
 
Mkuu, hii inatia hamasa sana na kwa kusema ukweli mtupu, unafiki kwa wa TZ ndo tatizo kubwa sana, na hii inaturudisha nyuma sana hata kwa maendeleo!
 
Dr Ulimboka amewaangusha MaDaktari wenzake, wanaHarakati na WATANZANIA kwa jumla kwa kuamua kukaa kimya. Hamasa yoote ile tangu siku anateswa, anapelekwa kwenye matibabu, anarudi, imeishia kwenye kauli tulioizoea: YOTE NAMWACHIA MUNGU!
 
Jisomee Kutoka: Aliyemteka Ulimboka huyu hapa | Gazeti la MwanaHalisi

Halafu kweli MIJINGA na MIPUMBAFU inakuja kudai mtu KANYAMAZISHWA...... Kama Madokta walirudi kazini kimya kimya baada ya mwenzao kuponea kwenye TUNDU LA SINDANO, ni UNAFIKI wao. I
la Mwisho wa siku, ni TANZANIA nzima kwa ujumla, ukiacha wachache wanaotibiwa India, ndiyo tulikuwa tuwasaidie Madaktari ila sisi tukajifanya hatuoni.

Misomi MIZIMA inakosa msimamo. Naamini maneno ya Rev. Msigwa wa Chadema kuwa tumekuwa taifa la Waoga na Wanafiki. Prof. mzima akianza kuchangia hana tofauti na mtoto wa darasa la pili. TOO SAD




 
Last edited by a moderator:
Mkuu una mwandiko mbaya na akili nyingi kama daktari...lakini nimekuelewa. Na ninakuunga mkono 100%. Tunahitaji kiongozi wa kusimama na kutuelekeza jinsi ya kuupinga huu udhalimu kwa kupinga nguvu ya huu udhalimu.

Binafsi nilikerwa sana na uamuzi wa madaktari wetu kushindwa ku-devise modality na kuuendeleza ule mgomo wao mara baada ya kilichomkuta Dr. Ulimboka. Kurudi kwao kazini ilikuwa ni kama ishara yao kwa serikali kuwa wamesalimu amri,wao ni waoga na pengine kuwapa nafasi wengine kuamini kuwa pengine Dr. Ulimboka alikuwa anapigania maslahi yake binafsi,ama alitumwa na taasisi fulani na kuwa madktari wengi walikuwa naye tu sababu walitishwa na wenzao wachache walioongoza mgomo..this was very,very unfair kwa Dr. Ulimboka has baada ya ku-endure yale maumivu yote na kuteswa kwa ajili yao.

Naunga mkono watanzania tuache uoga na unafiki...we need a leader!!!
 
Dr Ulimboka amewaangusha MaDaktari wenzake, wanaHarakati na WATANZANIA kwa jumla kwa kuamua kukaa kimya. Hamasa yoote ile tangu siku anateswa, anapelekwa kwenye matibabu, anarudi, imeishia kwenye kauli tulioizoea: YOTE NAMWACHIA MUNGU!

kipi ambacho hukijui mpaka sasa?.....
 
Mimi nawalaumu akina mama Bisimba. Ofisi yake LHRC ilitoa tamko kali ambalo nikiwa karibu na computer nitaweka hapa. Tamko linaloitaka serikali ishughulikie suala hilo na hata walipendekeza utaratibu ambao ufuatwe

Mama Bisimba yupo wapi? Pia napenda kusema kwamba mama Bisimba na serikali wote wajue kwamba hili suala la Dr. Ulimboka siyo suala kati ya hizo mbili tu na sisi wananchi ni wadau hapo ukizingatia kwamba serikali ambayo inaendeshwa kwa kodi zetu ndo inatumiwa kufanya unyama huu.

We unafikiri H.K. Bisimba na LHRC wanaweza fanya nini zaidi ya tamko lao na walivyodemonstrate Ulimboka alipokuwa anapelekwa SA an alipokuwa akirudi pia? Unadhani Ananilea Nkya atafanya nini cha ziada zaidi ya walichofanya tayari? Bisimba, Nkya ni mtu mmoja mmoja tu....LHRC ni taasisi moja tu...maDaktari ni fani moja tu...this is bigger that just one person, one institution, one discipline! Hili ni la Taifa zima...

Wewe kabla hojaona 'kibanzi' kwenye jicho la mama Bisimba na Nkya, toa ji'boriti' hilo jichoni mwako kwa kujiuliza kwa nafasi yako wewe umefanya nini kupinga hili? Ni lini tutaacha kutegemea watu fulani ndio watusolvie matatizo yetu!? Ni lini tutaona haya matatizo yetu yanatuhusu sisi mmoja mmoja kwa ujumla wetu and 'do something about it' badala ya kulaumu kina Bismiba, sijui Nkya...sijui Chadema/CUF et al!

Wanaharakati wanahangaika kila siku kutuamsha...tunajifanya hatuamki...wakati tumeshaamka zamani, waoga tu tunavuta shuka na kujifanya bado tumelala! acha kulaumu watu...jilaumu wewe kwanza kwa kutotimiza wajibu wako kama mTanzania Mzalendo!
 
mfano bahati mbaya ingetoke katika hali ile huyu ndugu angepoteza maisha..je kile alichokisema kisingefanyiwa kazi?..mtu amesema kila kitu tena akiwa katika maumivu makali sana, amevimba, ametapakaa damu...bado aliweza kuongea na kusema yote mwanzo mpaka mwisho alipofikishwa huko mabwepande na kufukiwa na hata aliweza kukumbuka namba ya daktari mwenzake ndipo taarifa za kujua mahali aliko zikapatikana....bado watu wanamnyoshea kidole na kusema aseme nani alimteka..aseme nini wakati alishasema?..huu ni unafiki na upuuzi mkubwa sana..naungana na mleta mada alivyosema kuwa watz kwa wingi wao ni wapumbavu na wanafiki sana......
 
Hata mimi nilihoji toka mwanzo kabisa.. Dr Ulimboka amezungumza yote YOUTUBE.com, tena kwa hisia kali zilizokua zinamtoa mpaka machozi, Kubenea nae akakolezea wino wake.. Mpaka leo hakuna jipya.. Nakuunga mkono mkuu..
 
SAWA. Lakini kwanini Dr Ulimboka akae kimya mpaka leo?? Hata kama mtu unataka kumtetea utaanzia wapi..?? Haya mambo ya kimbea mnayosema, yanasababishwa na yeye mwenyewe kukaa kimya?? Afunguke, asipoteze ujasiri. Kitu kingine kinachofanya waTZ kuwa hivi ni namna ya Utawala na Upatikanaji wa Haki nchini, my be katiba mpya itatubadirishia mifumo mingi.
 
baluhya M.

Nimekugongea likes. Hakika umenena na ninakuunga mkono kwa 100 pc +!

Tanzania ni nchi ya viongozi wanafiki,waoga,wapuuzi,majuha,waongo na wasiotaka ukweli hata kama ukweli huo umewekwa wazi mbele yao. Kwa ujumla ni nchi ya watu walio sawa na maiti kama jamaa mmoja alivyosema. Kwamba nchi hii unaweza kufanya chochote unachotaka,unaweza kuua,kuiba,kufisadi kwa kuiba fedha ya serikali kwa mabilioni na kuipeleka nje ya nchi, believe me HAKUNA MTU ATAKUULIZA!

Tumewahi kusikia kauli za viongozi wa CCM mmojawapo akiwa Rais Kiwete mwenyewe akisema HUO NI UPEPO WA KISIASA TU,UTAPITA MAANA WATASAHAU! Kiwete ana uhakika na anachokisema. Kwamba Watanzania ni wataalamu kwa kupiga makelele ya siku mbili tatu na baadaye husahau moja kwa moja!Hata hii lugha ya HII NI NCHI YA UDUGU,UMOJA,UPENDO NA MSHIKAMANO ni lugha ya kuwalaghai na kuwazuga watu ili wasifikirie kufanya maasi kwa viongozi dhalimu wa CCM kutokana na longolongo kama hizo.

Tumesikia Bungeni upande wa Upinzani ukitoa hoja zenye nguvu lakini wameishia kuzomewa,kubezwa na hata kusimamishwa na kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge. Tumesikia hoja za matrilioni ya shilingi za Kitanzania yaliyoko nje ya nchi zikitolewa na upinzani lakini mtu kama Spika anamrukia Mbunge aliyetoa hoja hiyo yeye ndiyo athibitishe kwa kuwataja wahusika vingine atapelekwa mbele ya Kamati ya maadili ya Bunge!!!

Tujiulize kwa mfano kwanini viongozi wanapatikana na tuhuma kwenye nafasi zao na kutakiwa kujiuzulu wanakuwa wakali na wanakataa katakata kabisa kuondoka madarakani? Wanajua Watanzania hawawezi kufanya chochote kuhusu kuwawajibisha viongozi hao kwa vile ni wajinga,majuha,wanafiki wakubwa. Mtu ataishia kusema tu kuwa yeye ni mteule wa Rais kwahiyo mpaka hapo mteule wake atakapomwambia kuwa ajiuzulu! Ujinga huu unapatikana Tanzania tu, maana nchi za wenzetu hawanaga upuuzi kama huu.

Kweli nchi yetu inahitaji msaada wa Mungu pekee ndiyo itaweza kubadilika. Bila ya Mungu kuingilia kati we are all doomed!
 
Last edited by a moderator:
WOTE MLIOCHANGIA HUU UZI NADHANI SIYO WATANZANIA! KAMA KWELI NI WATANZANIA BASI TUCHUKUE HATUA KUKEMEA UPUMBAVU WETU KWA VITENDO, MWENZETU KATUFUNGUA MASIKIO HIVYO TUJIPANGE KUTETEA WANYONGE WENZENTU COZ LEO KWAKE KESHO KWETU, NAAMINI WANAHARAKATI,MADAKTARI NA WABUNGE WAPAMBANAJI WALIOPO HAPA JAMVINI WAMEINAMISHA VICHWA CHINI KWA UKALI WA UZI HUU. AIBU KWETU.

Nisione tena mtu kaandika naunga mkono 100% hii kauli mjengo ndo imetufikisha hapa, nataka kuona mbinu na hoja zenye mashiko za kutukomboa kwenye huu upumbavu wetu.

WAO WALISEMA LIWALO NA LIWE! NASI TUJE NA KAULI YETU YENYE NGUVU NA AKILI
 
kila m-tz angepata fursa ya kuchangia hapa, kila mchangiaji angesema watz ni wanafiki huku yeye mwenyewe akidhani si sehemu ya tatizo! Kila mchangiaji humu angechukua hatua ya kukataa udhalimu kwa vitendo tungefanikiwa. Wengi wetu hata humu jf, ni wajasiri wa kukaa kwenye keyboard na kurusha shutuma si watu wa vitendo! Mbona hata gazeti lililo kua linatoa habari hizo lilipofungiwa tumekaa kimya? Si ndio upepo wenyewe unaopita huu?
 
Back
Top Bottom