ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Tumekuwa nchi ya kijinga sana, nchi ya kinafiki sana, nchi ya watu wasiothaminiana, nchi ya ambayo Raia wake wanafanikiwa kwa kusema uongo, nchi ambayo raia wake wanaosema ukweli wanakwamishwa katka nyanja zote za maisha, nilikuwa na naendelea kuamini kwamba Dr. Ulimboka steven aliyetekwa,kuteswa na kutupwa katika msitu wa pande alianika taarifa zote za msingi kuhusu kutekwa kwake kabla ya kwendaSouth africa kutibiwa, alifanya mahojiano ambayo yalirekodiwa na yako katka mtandao wa U-tube, amesema kuanzia nani aliyempigia simu,amesema aliyempigia simu anafanya kazi wapi, ameeleza vizuri jinsi alivyotekwa na kuteswa na watu ambao yeye aliwaita kuwa wako trained,[ni kutokana alivyowaona yeye], alieleza jinsi alivyopelekwa kwenye jumba ambalo pamoja na yeye [ulimboka] kupiga kelele hakuna mtu aliyejitokeza kumsaidia. Gazeti la Mwanahalisi lilikuja na namba na majina ya watu waliofanya mawasiliano na Doctor Ulimboka kwa mara ya mwisho, lenyewe limeishia kufungiwa tu!
Lakini leo kila mtu anahoji ukimya wa Dr. Ulimboka,mfano wandishi/wananchi/ wanaharakati/wanasiasa/ n.k wanahoji kwa nini Ulimboka hawataji waliomteka, wengne wanaenda mbali na kusema Ulimboka kanyamazishwa na watu wanaowaita vigogo n.k, huu ni upumbafu, unafiki, unaweza kuongeza majina mengne yanayomanisha tabia za kipumbafu na kinafiki, jiulize, je sisi kama taifa na kama wananchi wanyonge tumezifanyia kazi kwa kiwango gani taarifa ambazo tayari Doctor katoa?? Je tumedai kwa kiasi gani kukamatwa kwa watu/ mtu aliyempigia simu doctor mara mwisho kabla ya kutekwa? Tumedai kwa kiasi gani serikali kuruhusu tume huru?? Kama tumeshndwa kama taifa kuinuka na kutaka wahusika wote wakamatwe na matokeo yake watu wameishia kukamata Joshua mlundi tu,tunapata wapi ujasiri wa kuendelea kumshinikiza Doctor ulimboka atoke hadharani na kuwataja wahusika?
Kumbuka Doctor ulimboka pamoja na maumivu aliyokuwa nayo alijitahdi kuelezea scenario ya kutekwa kwake yote,lakn kwa sababu taifa letu limekuwa la wanafiki na wapumbafu tumeshndwa kufanyia kazi taarifa ambazo zipo tayari na matokeo yake tumejikita katika kumlazimisha ulimboka aache kupumzika ili aje kutoa taarifa za kutekwa kwake! Ambazo kimsingi haziwezi kuwa tofauti na zile ambazo ziko u-tube na ambazo mwanahalisi liliandika.
Huu tunaomfanyia Dr Ulimboka steven ni unafiki,ujinga na upumbafu uliokisiri. Na kama taifa tumeonesha kwa kiwango kisichotia shaka kwamba hatuna uwezo wa kurisk maisha yetu kwa kiwango chochote kwa ajili ya kuteteana wanyonge kwa wanyonge. Mwisho kabisa nataka ieleweke kwamba mtu yeyote awe wa serikalin, CCM,CDM, CUF, TLP,MAGAZETINI, NGOs ,KANISANI, TELEVISION akisimama na kusema anahitaji taarifa zaidi kutoka kwa Doctor Ulimboka juu ya kutekwa kwake mtu huyo apelekwe Milembe mara moja.
umesahau MASSIJID (MSIKITINI BRO)