Huu si wakati wa longolongo; Katiba Mpya, Tume Huru iwe ndiyo wimbo wa Taifa

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,817
Naona kuna dalili za kuyahepesha madai ya katiba mpya na haswa tume huru ya uchaguzi, kuna harakati zimeibuka kutoka kusiko julikana na ni nyingi na zinakuwa kama moto wa nyasi kavu.

Lengo likupinsha muelekeo ulioanza kubaleghe kwa maana uoga umeanza kuondoka juu ya kupiga makelele ya kudai tume huru na katiba mpya.

Chenga wanazotaka kupiga ving'ang'anizi ni kuwaondoa wanancho kwenye mstari.

1) Kesi ya Mbowe
2)Tozo sijui za miamala
3) Utalii wa Rais

Yote hayo yameonekana kufeli sasa wameongezea

4) Msajili wa vyama kuungana na Mkuu wa polisi Mheshimiwa Siro.
Hili la nne hili ni hatarishi lengo sio majadiliano sijui ya makongamano lengo wanalo na nalihisi ni kuataka kuruhusu lakini katika kuruhusu huko iwe ni mwiko na upawa kuzungumzia madai ya Katiba mpya na madai ya tume huru. Hili nimeliota kuwa ndio lengo kuu na ujumbe unaotaka kuvitia Magufuli vyama vya siasa haswa vile vyenye msimamo mkali wa kisiasa,yaani mruhusiwe kufanya mikutano lakini msiwashawishi watu kudai ume huru wala Katiba mpya.

Huu ni wakati wa kampeni kuwainganisha waTanzania wengi juu ya madai ya Tume huru na Katiba mpya, bora muvunje vyama kama hamuwezi kuwashawishi wananchi katika jambo na wananchi wakawasikiliza makamanda mnashindwaje kuwatongoza wananchi na kujenga msimamo kitaifa juu ya madai ya Tume huru na Katiba Mpya? Mnawapa nafasi waliomadarakani kutanua ni lazima muwe mstari wa mbele msiwape nafasi ya kutanua, ni lazima muwakeep bize na mambo makuu hayo wataharuki kuwa sasa kweli nchi inahitaji mabadiliko.

Tuseme ukweli hali ya mwananchi wa kawaida sasa ni mbaya sana, wananchi hawana hela kazi hakuna na wanachokipata kiguru anakiwinda, Raisi anakula bata mguu juu, mtalii.

wananchi wanalia kweli wanashida ngumu sana,angalieni vipindi rushwa kwenye tv za youtube angalieni maximumTv uone shida, serikali inashindwa kutibu raia zake walio katika hali ngumu, hata kwa magonjwa yale yalio hatari na yanatibika,lakini kwa umasikini wa raia hana uwezo. Serikali kwanini haiwavuti pembeni wagonjwa hawa na kuwapa tiba bure.
Katiba mpya na tume huru ndio kila kitu .
 
Katiba ndio hitaji namba moja kwa taifa hili kwa watu wanaojielewa na kujali kesho bora ya watoto, wajukuu na vitukuu vyao.
 
Naunga mkono hoja, ni lazima tujenge Taifa lenye uwajibikaji

Serikali ina matumizi ya anasa, posho kubwa kubwa, na kunyonya masikini.

Viongozi wamekuwa watawala, miungu watu.

Serikali inaumiza wananchi kwa posho kubwa kubwa, na maV8

Kuna wakati Pinda alijaribu kuzungumza kuhusu kuacha ununuzi wa maV8. CCM walimpiga vita, Pinda akaufyata

Katiba mpya na Tume huru

Serikali iache matumizi ya anasa
 
Tatzo lenu wachumia tumbo wa kisiasa wa nchi hii hamjui hitaji hasa la vijana wa nchi hii na wapi muekeze nguvu zenu muende nao sawa ili na wao wawa suport kwenye yenu.

Vijana wanawaona wabinafsi tu mnavyopigania agenda zenu izo mbili bora hata mngeongeza moja ya ajira kwa vijana zikawa tatu mkaenda nazo kwa pamoja.

Na hamtakaa mfanikiwe milele. Ingawa kweli hatuitaki ccm ila Tanzania hii bado hakuna chama cha upinzani chenye nia kweli yakushka dola.

Wote ni wachumia tumbo tu.
 
Back
Top Bottom