Huu sasa si ufisadi na tamaa ya pesa bali ni pepo kabisa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu sasa si ufisadi na tamaa ya pesa bali ni pepo kabisa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by buyegiboseba, May 7, 2012.

 1. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitendo wa wataalamu wa wanyama,afisa afya na watendaji wa majinchio ya vingunguti kuruhusu kuletwa utumbo na nyama iliyooza na kuuzwa kwa wananchi,kimevuka hata mipaka ya ubinadamu
  Ni kweli nchi inanuka rushwa na ufisadi lakini kwa kiwango cha namna hii,si kawaida ni pepo ndani ya watu!
  Kwa hali ya kawaida,haihitaji kuwa msomi sana kubaini kuwa bidhaa ya kuoza kama ile italeta madhara madhara makubwa sana kwa watu na pengine hata ndugu wa karibu wa wahusika(kwani hakuna namna utafuatilia nani kanunua ili wewe usijikute unakula pia)
  Niliangalia habari ile kwa masikitiko makubwa sana,nikafananisha na ya ekelege wa TBS kuruhusu bidhaa feki.
  Tunahitaji ukombozi wa kiroho pia sio tu wa kupaka siagi wakati mkate ni ule ule uliokwisha muda wake

  I sadly submit!
  Source.ITV habari saa 2 usiku,6/5/2012.
   
Loading...