Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mojawapo ya bajeti zitakazosababisha mzigo mkubwa kwa wananchi imepitishwa. KUpitishwa kwa bajeti hii nzima kunaashiria jambo moja kubwa CCM imefikia kikomo cha ubunifu wa kutatua matatizo ya wananchi iwe ni katika sera, sheria au utendaji. Kwa mwaka huu uliopita nimekuwa nikisisitiza sana watu kuelewa kuwa tatizo kubwa ambalo limechangia sana kuliingiza taifa kwenye matatizo mengi ni sera mbovu zilizoshindwa (japo hata wapinzani hawaamini sera za CCM ni mbovu).
Bajeti hii inadhihirisha msimamo wangu huo kwani bajeti hutoka kwenda kutekeleza sera mbalimbali. Sera hizi za CCM zimejaribiwa kwa miaka ishirini sasa na tayari zimeonesha kushindwa licha ya kupigwa 'tough' na mipango mbalimbali kama ya MKURABITA, MKUKUTA na Mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
Kama hili ni kweli - na ninaamini ni kweli - basi kuna mgogoro kati ya Watanzania na chama chao tawala; mgogoro ambao hitimisho lake litaanzia 2014 (kwenye serikali za mitaa) na kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Mgogoro huu ni kamili na dhahiri. Ni mgogoro ambao hauwezi kuzimwa na ahadi, vitisho au kupuuzia. Ni mgogoro ambao hauwezi kutoweka hivi hivi isipokuwa kwa chama tawala kushindwa. Hata hivyo, tokeo hili litategemea moja kwa moja CDM itafanya nini to take advantage ya mgogoro huu. Hili ni swali ambalo muda utaamua.