Huu sasa ndio ufisadi uliokufuru! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu sasa ndio ufisadi uliokufuru!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Mar 25, 2011.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Hivi sasa nchini kwetu Tanzania kuna noti za aina mbili zitumikazo:'mpya' na 'za zamani'.Kwa mujibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Profesa Benno Ndulu,noti za zamani zitaendelea kutumika pamoja na mpya hadi pale zitakapoisha kwenye mzunguko wa fedha.Gavana Ndulu hakutaja mwisho wa huo mzunguko.

  Ingawa mimi si mchumi na sijui sana kuhusu fedha,ninahisi harufu ya ufisadi mkubwa juu ya noti za zamani.Nijuavyo mimi,mzunguko wa noti huanza na kuishia Benki;kama si Benki Kuu basi ni hizi za kawaida kama CRDB,NMB,NBC,BARCLAYS,STANBIC na nyinginezo.Sasa,kwanini Mabenki haya yote yanaendelea kutoa noti za zamani? Kwanini Gavana asiweke tarehe ya mwisho ya utumizi wa noti za zamani?

  Je,kama wahuni wachache wakiendelea kuchota mabilioni Benki kuu (kwa noti za zamani )na kuyarudisha kwenye mzunguko yakiwa yao,nani atajua na nani alaumiwe? Tafadhali,nawaomba wananchi wenzangu hasa Wabunge,Usalama wa Taifa,Polisi na Raia wa Kawaida tutafute ukweli wa harufu hii ya ufisadi wa kufuru.Nisipopata ushirikiano wenu,nitafanya jambo ambalo halijawahi kufanywa hapa nchini.Mtailaumu maiti yangu.....
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu hata mimi nimeliona hilo na majuzi nilikwenda benki wakanipa za zamani nikauliza kulikoni?

  Majibu yao ndio fedha iliyopo ktk mzunguko na wanazopewa na sii noti mpya..Ufisadi unaendelea na tukisema watasema ni chuki zetu kwa serikali ya JK..
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180

  Mi kinachonishangaza ni kuwa huko benk bado noti za zamani zinatoka zikiwa mpyaaaaaaaa, ina maana walikuwa na stock kubwa sana, au bado zinachapishwa? na zinachapishwa kihalali?
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kwa kweli inashangaza ukienda benki unapewa bundle jipya kabisa la noti za zamani inahuzunisha utendaji wa bot ni kama chama cha mapinduzi
   
 5. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna wizi wa kutisha hapo. Ni dhahiri kuwa JK na serikali yake wako kimya. Hii ni namna nyingine ya kutengeneza hela za 2015
   
 6. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  wakati umefika Gavana wa Benki KUU atoe tamko rasmi mwisho wa mzunguko ni lini..
  sitashaangaa tukiendela kutimia noti mpya na za zamani mpaka ikafika wakati wanabadilisha tena noti.
   
 7. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mpya hizi pia ukipata noti 10 za elfu 10 basi tano ni bandia. Sasa nazo zimeingizwa ktk matumizi halali ya fedha. Usiulize mchapishaji, chunguza mtaani.
   
 8. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 584
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Beno na timu yake watakuwa wanafanya mipango ya kubadilisha ubora wa noti mpya kinyemela ili zenye ubora unaotakiwa zikishapatikana ndio hizi mbovu na zamani zitakapotoweka!
   
 9. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  hizo mpya siku zina ingia tu, wajanja walizikwiba airport(Kam 5Bl au zaid) na kupelekea kutolewa taarifa kwamba hazitatumika tena,ila kwa mshangao ngoma zikaingia kwa mtaa.
  Na ubora wa noti mpya haurizishi, kwani zinatoa rangi utadhani jeans ya kuchovya!
  Kwa utetezi wa Beno ati ndo security hiyo(kuchuja rangi)
  jiulize hapo,....!!
   
 10. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,896
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  we ndugu yangu, kuna watu wana manoti ndani huko masaki na mbezi beach waliyoyapata isivyo halali wanayatoa kidogo kidogo. wakiweka tarehe ya mwisho itakuwa balaa kwao. wanahakikisha yanaisha ndani ndiyo wanasitisha matumizi ya manoti ya zamani.
   
 11. d

  dotto JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna noti mpya bandia au feki nyingi sana kuliko halali kwenye mzunguko. Jaribu kuchunguza uone. HAijawahi tokea katika historia ya Tanzania ushenzi kama huu kutokea. Benno anajua na wenzake hasa hasa baada ya uchanguzi maana halisi ya kubadilisha noti punde tu baada ya uchaguzi. Ni hatari hakuna usalama. Intellegensia zote zimekaa kimya. Wenye nchi wanajua wanalofanya. MAskini tumwachie Mungu anajua mwisho wake!!! Tutafika tumechoka sanaaaa.!!!
   
 12. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2014
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Manoti bado yanaendelea tu
   
 13. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2014
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa, hata mimi nimepewa noti za zamani za Tsh.2000 kutoka Benki ya DTB tawi la Mbeya. Ni ajabu maana ni mpya kabisaaaaa.
   
 14. g

  gebu Member

  #14
  Jan 31, 2014
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 25
  Bora noti za zamani hizi mpya ni kimeo kabisa,mfano mia5,elfu moja na elfu mbili zinawahi kuchakaa..na makonda nao ukiwapa au ukienda kununulia kitu dukani wanazikataa yan tabu kwenda mbele..hapa kuna harufu tena kali sana ya ufisadi
   
Loading...