Huu pia ni udhalilishaji, na hapo ndipo Tanzania inapokuwa " Nchi ya kushangaza"

malisoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Messages
1,818
Points
2,000

malisoka

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2012
1,818 2,000
Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ni nchi inayo boresha elimu kwanza na baadaye yanafiata mambo mengine ya barabara, lilimo viwanda na nk.

Cha kuchangaza ni kwamba awamu hii imesahau lkabisa kuboresha elimu hasa ya msingi.

Wengi watanishanga kwamba mbona sijaona elimu bure inatolea nk.

Kutoa elimu bure halafu walimu wanafanya kazi kwa masononeko hiyo inakuwa sio elimu bora.

Kuwajaza wanafunzi hasa wa Msingi darasa moja wanafunzi 100 au zaidi hii mimi ninaita ni siasa za maji taka na ni uzalilishaji wa wanafunzi, kwamba kwa sababu ni elimu bure basi mtu asilalamikie elimu inayotolewa hapo.

Sijui waziri wa elimu yupo au anawaza (stress) za namna ya kugombea ubunge huko Kigoma, ni profesa wa elimu hivi inakuwaje mwalimu akafundisha watoto 100 katika darasa moja na bado mkamtaka eti hao wanafunzi wawe na ufaulu mzuri?

Huyu mwalimu atafuatliaje maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja na kutatua matatizo yao?

Kujenga reli ya kisasa, barabara, madaraja, kununua ndege, meli nk ni sawa na kujilisha upepo.

Ushauri wangu:

Kama ningekuwa Waziri wa Elimu au potelea mbali ningekuwa Rais ningefanya haraka haya yafuatayo:

1. Ningetoa tamko, kwamba shule zote za msingi ziwe na session mbili au tatu kwa siku ili wanafunzi angalau wawe hamsini (50) kwa kila darasa katika shule zote za msingi.

2. Wakati hili likifanyika shule zifanyiwe ukarabati kwa kuongeza majengo ikiwezekana ya ghorofa au zijengwe shule mpya nyingine maeneo hayo hayo na baadaye wanafunzo kugawanywa.

3. Kuajili walimu wapya, au kuhamisha walimu hasa wa sekondari kuja kufundisha msingi (msiseme hakuna pesa " Tanzania ni nchi tajiri sana").

4. Sio vibaya tukisema "Elimu na viwanda nguzo yetu"

5. Mnaweza kusema hakuna fedha " kaa na makampuni ya simu ongezeni shilingi 10 gharama ya kila simu itakayopigwa au bundle la internet nina uhakika mtapata mabillioni ya pesa kwa mwaka.

ILA kwa haya tunayoyaona katika Shule za Msingi ni kama vile waziri hukwenda shule, elimu yako inaonekana ni bure na hata wakati mwingine tunakutilia mashaka.

Mh Waziri, kujivunia kuandikisha wanafunzi wengi darasa la kwanza huku ukiwalundika kama kuku katika darasa moja sio sawa.

Kama tumeweza kununua ndege nyingi, reli ya kisasa SGR, tunajenga madaraja na mabarabara tunashindwa nini sasa kuboresha elimu ya msingi?

Ningetamani siku moja Rais atambue kwamba 90 ya walimu na wafanyakazi wizara ya elimu watoto wao hawasomi shule za msingi au sekondari za serikari kwa nini.

Na hapo angegundua kwa nini wizara ya elimu na maafisa wake(watunga sera) wanapuuza elimu yetu ya msingi hivi!

NB:
Ila hili la elimu bure litazamwe upya, haiwezi kuwa elimu bure halafu elimu hiyo inachezewa namna hii.

Ni bora ikalipwa Shs 5000 kwa kila mwanafunzi na hizi pesa zikasaidia kuboresha elimu ya msingi.

Mlianza na madawati, kuna walimu wa kutosha (msingi) sasa geukieni mrundikano wa wanafunzi madarasani ni aibu, wengine hatuangalii SGR au ndege zinazoruka tunaangalia elimu ya watoto wetu.
 

Forum statistics

Threads 1,391,865
Members 528,491
Posts 34,092,285
Top