Huu ni wizi Vodacom au ni nini?

Straight corner

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
385
132
Kwa wale watumiaji wa Vodacom kuna droo za aina mbili zinaendeshwa kwa wakati mmoja; moja kushiriki ni bure (ya LCD TV) na nyingine inalipiwa (ya TSH 11m). Kushiriki ni hiari ya mteja.
Nilijaribu kushiriki hii ya bure na kuulizwa maswali kadhaa na nikayajibu sahihi (si rahisi mtu ukose maswali haya). Mwishoni nikaletewa ujumbe huu, nanukuu:
“Umedaka pointi zote za leo! Bado kitu… Wataka kuingia droo zote za kila siku za TSH milioni 11? 1=NDIO 2=HAPANA.Tuma 1 au 2 kwenda 15544! Gharama: TSH 550/siku” mwisho wa kunukuu.
Hapa ndo kuna swali langu, nilituma 2 kwenda 15544. Nilikatwa TSH 550/ na kuambiwa nimeingia kwenye droo zote za TSH Milioni 11.
Ndugu zangu nisaidieni, nimeibiwa au inatakiwa nichajiwe kama walivyofanya?
 
Hujaibiwa, sms uliyopokea ilieleza wazi kuwa ujumbe uakaotuma utagharimu 550, ungechuna tu kama hukutaka kuingia gharama.
 
Kwa upande wangu ninapenda kufahamu muda gani droo inachezeshwa maana saa moja dkk 55 wanatangaza tu mshindi tena nahisi ni kipindi ni recorded sio live.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom