Huu ni wizi unaofanyika NMB kumlipisha mteja kadi iliyoisha muda wake na wala haijapotea

Kaneeza

Member
Jul 11, 2012
79
15
Nimesikitika sana jana nilipokuwa Bank ya NMB Kenyatta pale mwanza mjini,baada ya kumwona bibi kizee akilipishwa kiasi cha shilingi 20,000/- ili kulipia Kadi yenye account iliyofunguliwa Musoma.Cha kusikitisha bibi mwenyewe hata pesa hiyo hakuwa nayo kwenye account.

Je ni haki kulipisha kiasi hicho cha pesa kwa hoja kwamba ndo gharama za kuisafilisha kutoka Musoma?,Au ni biashara ambayo wanaifanya ili kuwaibia wateja wao kwa kisingizio cha gharama!
 
Niliambiwa 15,000/- kama una renew kwenye tawi ambalo hukufungulia. Hii mada ntairudia baadae. Nzuri mno
 
Hii benki nakumbuka ilikuwa inaitwa benki ya makabwela, labda siku hizi imekuwa benki ya matajiri
 
Back
Top Bottom