Huu ni wizi tena wizi wa wazi

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Ndugu wana Jf

Mimi nashangaa sana tena sana kwa baadhi ya mashirika ya simu hapa Tanzania kutumia hii nafasi ya kuupigia kura mlima kilimanjaro kwa kuwalipiza wananchi kiasi cha shilingi 500 kwa sms

huu ni wizi tena wizi ambao upo wazi kabisa,lengo letu ni kutaka mlima wetu kuchaguliwa kuwa ni mmoja wa maajabu saba ya asili duniani,sasa baada ya kuhamasisha ili watu wengi wapige kura sisi tunacharge kila kura moja kwa tsh 500/=hivi ni kweli tunataka mlima huu upigiwe kura ama tunataka pesa toka kwa wapiga kura?

mbona nchi za wenzetu hawafanyi kama tufanyavyo sisi?


Jamani kila kitu bongo ni dili
 
mara nyingi namba 15xxx inakatwa. Kuwa makini.Tayari ishakuwa dili.uzalendo uko wapi?
 
Kuna jamaa alisha wahu kusema hapa Tanzania hadi maisha ya Raia hufanywa Deal.

Yeah kila kitu kimekuwa ni dili sasa,mimi nilidhani hili la mlima ni letu sote kwa manufaa ya taifa,sasa makaburu wanachukuwa pesa,yaani kweli wamefanya watanzania ni shamba la bibi
 
Mimi siwezi hata siku moja nitakaa nipige kura eti mlima k'njaro uwe moja ya maajabu ya dunia.
 
Back
Top Bottom