Huu ni wizi; Sipaswi kudaiwa kodi kwenye biashara ninayofanya kwa hela ya mkopo...

Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,191
Likes
428
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,191 428 180
Hebu ndugu unayesoma habari hii fikiria vizuri hiki kitu. Banks zinafanya biashara ya kukopesha ela, na biashara hiyo inalipiwa kodi. Ina maana bank wakinipa mimi mkopo nifanye biashara, tayari biashara hiyo imeshalipiwa kodi na bank. Kwa maana hiyo sipaswi tena mimi nakadaiwe kodi nyingine kwenye ile biashara, au hata nikidaiwa, basi iwe kidogo...

Ngoja nitoe mfano kama hujaelewa;
Mr X na Mr Y wanafungua kiwanda vya kutengeneza juice kwa kutumia mtaji unaolingana. Mr X anatumia mtaji wa fedha yake mwenyewe, na Mr Y anatumia mtaji wa fedha aliyokopa bank. Mauzo ya kwenye viwanda yanasababisha faida ya sh 100,000 kwa kila kiwanda kwa mwezi. Kati ya laki moja, Mr X analipa sh 20,000 kama kodi yake TRA... Mr. Y nae analipa sh 20,000 kama kodi. Mr Y ana deni bank, hivyo pengine anatakiwa alipe sh 50,000 kila mwezi. Hivyo kwenye ile laki moja, alitoa 20,000 kulipa TRA, alafu anatoa 50,000 kurudisha bank. Kati ya hizi 50,000 elfu 20 pendine ni riba (faida ya bank). Kwenye hii faida ya bank (20,000), TRA wanachaji hapo kodi ya tsh 5,000 labda. Hii elfu kumi na tano iliyobaki kama faida ya bank, kiasi fulani (labda 10,000) kinatumika kulipa wafanyakazi na kununua vitu. Kwenye mishahara ya wafanyakazi wa bank, na vitu ambavyo bank inanunua, kuna kodi ya TRA.

Kwa maana hiyo utaona Mr X ambaye hakutumia mkopo, analipa sh 20,000 tu TRA, lakini Mr Y ambaye kachukua mkopo, analipa pengine 30,000 TRA.

Madhara yake
Inakuwa ngumu sana kwa biashara inayofanywa kwa fedha ya mkopo kuingiza faida. Kutokana na hilo inasababisha kuwepo na biashara zinazotumia mitaji haramu na pia inasababisha ugumu katika biashara na uwekezaji.

Ushauri wangu
Serikali iwe na utaratibu wa kupunguza kiasi cha kodi kwa uwekezaji unaotumia mitaji inayotokana na vyombo vya vyedha ambavyo vinalipa kodi. Kwa kuwa uwekezaji wowote ni mtaji, basi kuwepo na tofauti kati ya tozo kwa uwekezaji ambao unatumia mtaji ambao unalipiwa kodi ukifananisha na uwekezaji ambao unatumia mitaji isiyolipiwa kodi

Faida yake
Itahamasisha ujasiriamali, kwani uwezekano wa kuwa na uwekezaji wenye tija utakuwa mkubwa
Itakuza ufanisi wa taasisi za fedha kwani watu wengi watajitokeza kukopa
Itaongeza soko kwa taasisi za fedha za hapa nchini maana kama mwekezaji atatumia mtaji aliokopa nje (kwenye taasisi isilipa kodo TRA), basi atahesabiwa anatumia mtaji usiolipiwa kodi, wakati akitumia mtaji unaotokana na kukopa kwenye taasisi za ndani, kodi yake itapungua.

Tahadhari
Kutatakiwa kuwe na uwazi katika mitaji na soko la mitaji...

NB; Mawazo haya nimeyatoa tu kwa fikira zangu kwani sijasoma mambo ya uchumi wala mitaji. Naomba wenye taaluma yao wajisikie huru kunielimisha na kunikosoa...
 
Voice of Wisdom

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Messages
537
Likes
40
Points
45
Voice of Wisdom

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2011
537 40 45
Kabla sijajujibu mkuu kuna jambo nataka kujua, je umeshawah kufanya biashara kwa kutumia mkopo wa benki?
Je katika kulipa kodi ulitumia utaratibu gani?
Lakini pia nikupe changamoto nyingine je unajua kuwa kodi ya mapato inatozwa katika kila pato lako upatalo?
 
M

Madaraka Amani

Member
Joined
Mar 9, 2011
Messages
89
Likes
1
Points
0
M

Madaraka Amani

Member
Joined Mar 9, 2011
89 1 0
Ndugu yangu ni wanyonge tu ndio wananyonywa na hao wakubwa kupitia TRA. Wapo wafanya biashara wenye mitaji ya mamilioni hawa wanapowekeza kama wanavyoita wenyewe hupewa kipindi kinachoitwa grace period katika kipindi hicho hawalipi kodi wanasuburi biashara ikomae na kuanza kutoa faaida. wao ni wajanja kipindi cha grace period kinapokwisha wanauza kampuni kijanja kukwepa kodi na mwekezaji anayerithi kampuni nae anadai grace period. kwa mtindo huu wanaondesha serikali ni walalahoi, wajanja wapo salama na wanao watetezi hadi bungeni nadhani mliona waziri wa biashara alivyosema hadi povu likamtoka mdomoni kutetea wasilolipa kodi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariiki waalahoi....... Amina.
 
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
5,106
Likes
49
Points
145
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
5,106 49 145
Hebu ndugu unayesoma habari hii fikiria vizuri hiki kitu. Banks zinafanya biashara ya kukopesha ela, na biashara hiyo inalipiwa kodi. Ina maana bank wakinipa mimi mkopo nifanye biashara, tayari biashara hiyo imeshalipiwa kodi na bank. Kwa maana hiyo sipaswi tena mimi nakadaiwe kodi nyingine kwenye ile biashara, au hata nikidaiwa, basi iwe kidogo...

Ngoja nitoe mfano kama hujaelewa;
Mr X na Mr Y wanafungua kiwanda vya kutengeneza juice kwa kutumia mtaji unaolingana. Mr X anatumia mtaji wa fedha yake mwenyewe, na Mr Y anatumia mtaji wa fedha aliyokopa bank. Mauzo ya kwenye viwanda yanasababisha faida ya sh 100,000 kwa kila kiwanda kwa mwezi. Kati ya laki moja, Mr X analipa sh 20,000 kama kodi yake TRA... Mr. Y nae analipa sh 20,000 kama kodi. Mr Y ana deni bank, hivyo pengine anatakiwa alipe sh 50,000 kila mwezi. Hivyo kwenye ile laki moja, alitoa 20,000 kulipa TRA, alafu anatoa 50,000 kurudisha bank. Kati ya hizi 50,000 elfu 20 pendine ni riba (faida ya bank). Kwenye hii faida ya bank (20,000), TRA wanachaji hapo kodi ya tsh 5,000 labda. Hii elfu kumi na tano iliyobaki kama faida ya bank, kiasi fulani (labda 10,000) kinatumika kulipa wafanyakazi na kununua vitu. Kwenye mishahara ya wafanyakazi wa bank, na vitu ambavyo bank inanunua, kuna kodi ya TRA.

Kwa maana hiyo utaona Mr X ambaye hakutumia mkopo, analipa sh 20,000 tu TRA, lakini Mr Y ambaye kachukua mkopo, analipa pengine 30,000 TRA.

Madhara yake
Inakuwa ngumu sana kwa biashara inayofanywa kwa fedha ya mkopo kuingiza faida. Kutokana na hilo inasababisha kuwepo na biashara zinazotumia mitaji haramu na pia inasababisha ugumu katika biashara na uwekezaji.

Ushauri wangu
Serikali iwe na utaratibu wa kupunguza kiasi cha kodi kwa uwekezaji unaotumia mitaji inayotokana na vyombo vya vyedha ambavyo vinalipa kodi. Kwa kuwa uwekezaji wowote ni mtaji, basi kuwepo na tofauti kati ya tozo kwa uwekezaji ambao unatumia mtaji ambao unalipiwa kodi ukifananisha na uwekezaji ambao unatumia mitaji isiyolipiwa kodi

Faida yake
Itahamasisha ujasiriamali, kwani uwezekano wa kuwa na uwekezaji wenye tija utakuwa mkubwa
Itakuza ufanisi wa taasisi za fedha kwani watu wengi watajitokeza kukopa
Itaongeza soko kwa taasisi za fedha za hapa nchini maana kama mwekezaji atatumia mtaji aliokopa nje (kwenye taasisi isilipa kodo TRA), basi atahesabiwa anatumia mtaji usiolipiwa kodi, wakati akitumia mtaji unaotokana na kukopa kwenye taasisi za ndani, kodi yake itapungua.

Tahadhari
Kutatakiwa kuwe na uwazi katika mitaji na soko la mitaji...

NB; Mawazo haya nimeyatoa tu kwa fikira zangu kwani sijasoma mambo ya uchumi wala mitaji. Naomba wenye taaluma yao wajisikie huru kunielimisha na kunikosoa...
Halafu mnataka maisha bora nchini wakati kulipa kodi hamtaki kweli watanzania hatuwezekaniki. Kwa ufupi ni hivi Benki inafanya biashara na hivyo inalipa kodi kwa mujibu wa sheria za biashara ya benki. Na wewe unafanya biashara kwa mujibu wa sheria ya biashara yako. Kwa hiyo basi kodi lazima ulipe hata kama umekopa hela benki au la. Unatakiwa uyafikirie haya kabla hujaenda kukopa benki sio kazi ya serikali mkuu kalipe kodi usitafute sababu.
 
Ruhazwe JR

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2011
Messages
3,413
Likes
25
Points
135
Ruhazwe JR

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2011
3,413 25 135
mdondoaji sikuelewi na unanitisha katika serikari yako ya uwelew
naomba usome kwanza maelezo ya ndugu yetu kisha utoe maoni.na wakati mwingine si lazima uchangie unaweza kukaa kimya si kila mada utoe upupu unaweza kuacha show your great thinking acha utoto
 
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Messages
4,140
Likes
1,145
Points
280
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2010
4,140 1,145 280
Ni mfanyabiashara au kampuni gani wasingetumia hiyo loophole kwenda kukopa benki ili wasilipe kodi au walipe kodi kidogo sana? Kwa maana nyingine aslimia ndogo ya mapato ya serikali yanayotokana na kodi ndio yasingekuwa yanapatika kwenye mabenki.Katika ile list ya makampuni yanaongoza kwa kulipa kodi umejaribu kuangalia ni benki ngapi zipo kwenye hiyo list na wanalipa kiasi gani? Nani asilimia ngapi ya dola bilioni 7 ambayo ndio bajeti yetu kwa mwaka?

Advantage ambayo ninaiona hapa kwamba tusinge hitaji TRA kwa sababu hakuna wanachokifanya sasa hivi zaidi ya kuwaumiza wachache?
 
Erick_Otieno

Erick_Otieno

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2010
Messages
629
Likes
947
Points
180
Erick_Otieno

Erick_Otieno

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2010
629 947 180
Cha muhimu ni kutumia wahasibu kuandaa mahesabu na malipo ya kodi za biashara zako kwani watazingatia hayo yote unayoyaeleza kwenye mfano wako kabla ya kulipa kodi.....ukienda kichwa kichwa inakula kwako vibaya....
 
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
5,106
Likes
49
Points
145
M

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
5,106 49 145
mdondoaji sikuelewi na unanitisha katika serikari yako ya uwelew
naomba usome kwanza maelezo ya ndugu yetu kisha utoe maoni.na wakati mwingine si lazima uchangie unaweza kukaa kimya si kila mada utoe upupu unaweza kuacha show your great thinking acha utoto
Sikiliza ndugu Tuko or Ruhazwe Jr,

Biashara yeyote utakayoanzisha kinachoangaliwa na TRA ni mapato na sio wewe umekopa au la. Ndio maana serikali imeweka kodi ya mapato kwenye kila nyanja. Si kazi ya serikali kudetermine wewe uliyekopa upewe punguzo la kodi au la. Ulitakiwa uyafikirie hayo wakati unaianzisha biashara yako vipi utakabiliana na changamoto za mkopo na uendeshaji wa biashara. Narudia tena usitafute sababu za kutokulipa kodi mkuu wakati wewe ukiomba upunguziwe kodi mbona makampuni makubwa yanaendeshwa kwa mikopo na hayapunguziwi kodi??

Pia unapozungumzia faida ya 100,000 Tuko kama Mr X and Mr Y wanapata 100,000 wote kama faida ya mauzo basi Mr Y atakuwa amepata faida zaidi kwani katika gharama za matumizi basi deni la mkopo litakuwa limeshalipiwa 30,000 na sio hadi mwisho wa faida ndio alipe mkopo wake. Ikiwa bado hajalipia deni la mkopo basi faida ya Mr Y itakuwa 70,000 na faida ya MR X itakuwa 100,000. Serikali inapokuja kuchukua kodi yake kodi ya mapato itakuwa sawa na asilimia ya Shilingi 70,000 for MR Y wakati kwa Mr X itakuwa sawa na asilimi ya Shillingi 100,000. Lakini kuondolewa kodi hilo halitawezekana kwani ndio pato la serikali linalotumika kuhudumia hospitali, kujenga barabara, bandari, kulipia watumishi serikalini nk.
 
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Messages
5,307
Likes
815
Points
280
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2008
5,307 815 280
Sikubaliani na wewe kabisaaa.

Kwa ungefanya hivyo ungetengeneza incentives za watu kufanya biashara zao zote kwa kukupa, serikali ingekosa hela sana.

Pia utakua unambagua mtu aliyetumia hela yake mwenyewe kuanzisha biashara badala ya kuchukua mkopo.

Na practically kusimamia kitu kama hicho sidhani kama inawezekana, kitu gani kinanizuia kununua shamba na hela zangu kisha kuchukua mkopo kwa kutumia shamba hilo, kisha mkopo naanzishia biashara ili mradi nisilipe kodi?
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
58,805
Likes
23,860
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
58,805 23,860 280
Hujaweka hesabu zako vizuri. Mtaji hauna kodi ikiwa utaonesha kuwa ulipoupata huo mtaji ulikuwa umelipiwa kodi. Faida ndio inalipiwa kodi.
 
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
6,818
Likes
1,673
Points
280
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
6,818 1,673 280
Inabidi utafute an accountant au uzijue sheria za ushuru wa biashara kwa sababu nadhani unachanganya mambo. Kama unatakiwa kulipa benki helfu hamsini you cant declare 100000 as a profit kwa sababu the loan is still is a liablity (expenditure) kwa maana hiyo faida yako ni 50000 tu na si laki. Hapo sasa TRA wakija you entitled to declare the amount left after all the business expenditures as a profit in your case 50000sh only.

Na watakuwa wapumbavu sana kama wanaihemea hata faida ndogo kama hiyo as it is bound to put off people from starting small businesses.
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,369
Likes
2,848
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,369 2,848 280
Conceptually, unajaribu ku argue kuwa equity financing is better than debt financing. Lakini umeacha/umeshindwa kudadavua athari za interest na dividend katika muktadha wa kodi. Wakati wa kukokotoa kodi interest unayolipa benki ni mojawapo ya exepenses hivyo in a way inapunguza kiwango cha kodi wakati dividend sio expense. Na zaidi, katika mfano ulioutoa(wa individual kukopa benki au kutumia pesa yake), interest inayolipwa bank haina kodi ya zuio na hata kama ingekuwepi sio final tax kwa bank wakati dividendvitakuwa na kodi ya zuio na kwa individual itakuwa final tax.

Kwa hiyo hoja yako haiwezi kusimama sawasawa bila pia kuelezea athari za hivyo vitu nilivyovitaja hapo juu.
 
Ruge Opinion

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2006
Messages
1,770
Likes
361
Points
180
Age
64
Ruge Opinion

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2006
1,770 361 180
Conceptually, unajaribu ku argue kuwa equity financing is better than debt financing. Lakini umeacha/umeshindwa kudadavua athari za interest na dividend katika muktadha wa kodi. Wakati wa kukokotoa kodi interest unayolipa benki ni mojawapo ya exepenses hivyo in a way inapunguza kiwango cha kodi wakati dividend sio expense. Na zaidi, katika mfano ulioutoa(wa individual kukopa benki au kutumia pesa yake), interest inayolipwa bank haina kodi ya zuio na hata kama ingekuwepi sio final tax kwa bank wakati dividendvitakuwa na kodi ya zuio na kwa individual itakuwa final tax.

Kwa hiyo hoja yako haiwezi kusimama sawasawa bila pia kuelezea athari za hivyo vitu nilivyovitaja hapo juu.
Ni muhimu vile vile kuelewa kuwa TRA haijiamulii viwango na namna ya kutoza kodi. Ni Bunge linalotunga sheria za kodi. TRA ni mtekelezaji wa Sheria. Sheria ya Kodi ya Mapato inayotumika haitozi kodi kwa kuangalia chanzo cha mtaji. Ila kama anavyosema SMU riba unayolipa kwenye mkopo inapunguzwa kwenye mapato kama expense (gharama ya biashara) katika kufikia kiwango cha pato kinachostahili kutozwa kodi. Wafanyabiashra wakubwa (wawekezaji), mbali na sheria ya kodi ya mapato, wanapewa nafuu ya kodi kutokana na Sheria ya Uwekezaji (Tanzania Investment Act). Huu unaweza kuwa ubaguzi dhidi ya wafanyabiashara wadogo (wazalendo) lakini sheria ya sasa ndivyo ilivyo. Fanya harakati ibadilishwe.
 
Forum statistics

Threads 1,236,755
Members 475,220
Posts 29,267,874