Huu ni wizi mkubwa Jamani!! Hakuna anae liona hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni wizi mkubwa Jamani!! Hakuna anae liona hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaneingoma Zom, Apr 3, 2011.

 1. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wadau wa JF na watanzania kwa ujumla wake naomba tujadili jambo hili nyeti ambalo mimi mdau mwenzenu nimeligundua na nikaona si vema kulikalia kimya.

  Wakati bado watu wanalipigia kelele jambo la kufeli kwa kiwango kikubwa kwa wahitimu wa kidato cha nne, hata wengi kuomba vijana hao warudie mitihani yao Baraza la mitihani Tanzania limeonekana kupingana na dhana hiyo waziwazi.

  Ndugu wana JF ikumbukwe kwamba kimbilio la mwisho la vijana hao na wengine wengi walioadhiriwa na mfumo mbovu wa elimu wa hapa nchi ni kurudia mitihani yao kwa gharama kubwa!!

  Watoto wengi ni wale wanaotokea katika familia masikini ambazo hata mkate wa kila siku ni matatizo makubwa. Lakini cha kushangaza watoto hawa wasukumizwa mbali na mifumo ya Elimu kana kwamba wao si sehemu ya jamii yetu hii!! Nasema haya kwa uchungu mkubwa kwa sababu, Kila mwaka Baraza la mitihani limekuwa likikusanya pesa nyingi kutoka kwa watoto au watu wazima wanaotaka kurudia mitihani yao.

  Wengi wa watahiniwa hao ni hao watoto wa shule za kata ambao kwa wao kufaulu inategemea sana kudra za Mwenyezi Mungu kwa kuwa mfumo umewatenga! Kwani mazingira yao ya kujifunzia hayawapi uhakika wa kufaulu. Kufuatia hali hii hawa watoto wamekuwa wakitegea hii mitihani ya kurudia au utahiniwa wa kujitegemea. Kutokana na hali mbaya kiuchumi ya hawa watoto na hata watu wazima wanaorudia mitihani yao huhitaji muda wakutosha kujiandaa ili kuweza kumudu kulipia gharama za kurudia mitihani.

  Pia watahiniwa hao watarajiwa huhitaji huruma kutoka kwa mtu yeye ya kuwapunguzia gharama ili suala lao la kufanya mitihani lisiwe gumu kiasi cha kuwaganya washidwe
  kufanya hivyo, hasa kukizingatia nchi yetu licha ya kuwa na raslimali nyingi ina hitaji wasomi watakao wenzesha matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa manufaa y watanzania.

  Lakini cha kushangaza kila kukicha hali ndo inazidi kuwawia vigumu watu hawa. Kwanza muda wa kujiandikisha kufanya mitihani umepungua tangu mie miezi mitatu hadi miwili, hili peke yake linawafungia wengine milango ya kufanya mitihani! Ikiwa huyu motto wa masikini atakuwa hana pesa ndani ya kipindi hicho basi system itakuwa imeshamtema mpaka mwaka mwingine.

  Miaka yote watahiniwa hupewa muda mzuri wa kujiandaa kutoka siku ambayo mwezi wa pili hasi mwezi wa nne mwishoni! Mwaka huu ambopo sisi tulitarajia serikali ingetoa fursa (muda) ya kutosha kwa hawa watoto ambao kwa makusudi wamefelishwa lakini imebana muda wa watu kujiandi andikisa kutoka muda wa miezi mitatu hadi miezi miwili.

  Pia tulitegemea Serikali ingepunguza hata gharama ili watu hawa wamudu kujaribu bahati yao, lakini mambo ni kinyume kabisa na hivyo ndo kwanza gharama zimeongezeka!! Wameongeza kipengele cha kujiandikisha kwa kuumia mtandao. Kwa hapa Arusha unatakiwa kulipa sh, 3500 ili uweze kujiandikisha kwa njia hiyo lakini gharama za kulipia ule mtihani zinakuwa ziko palepale. Pia katika kufanya hivo hawaakupi kufanya usajili mwenyewe hata kama una uelewa wa kutumia mtandao. Watakufichia neno la siri ili usiweze kufanya hivyo mwenyewe. sasa mimi najiuliza ikiwa watahiniwa hao wanalipa sh. 50, 00 pesa hiyo haitoshi kuwasaidia kusajili mpaka watake tena pesa zingine kutoka kwa hawa watu?

  Na kama suala la kuwasaidia kuandikisha ni gumu kwa nini mtu asiruhusiwe kujiandiishwa mwenyewe? Mimi naona serikali yetu imekusudia kabisa kuwaacha hawa watoto wawe nje ya mfumo! Jambo lingine ni vituo vya kufanyia mitihani vituo hivyo vimekuwa vikiopanga bei zao wenyewe bila mtu yeyote kuwadhibiti. Kituo kunamgharimu kijana huyu kati ya dh. 25,000 hadi 50,000 Je serikali hailioni hili? Au au tuamini hivyo kwamba wao kushidwa kwa vijana hawa ndio lengo lao? Ebu tuangalie Jeduali hapo chini tuone ni kwa kiasi gani inakuwa ngumu kawa vijana hawa kuendelea na masomo yao.

  Kitu kinacholipiwa
  Gharama yake
  Picha
  3,000
  Gharama za kutuma pesa
  5,500
  Kituo
  2,5000 – 40,000
  Gharama za mitihani
  35,00 – 50,0000
  Jumla ya kwanza
  68,500

  98,500

  Kwa maisha ya watanzani wengi hasa waishio vijijini inaonekana kabisa hawatakiwi kuendelea na masomo yao! Kwani kipato cha wazazi wao ni kidogo sana! unapofupisha muda wa kujiandikisha, unapoongeza gharama za kujiandikisha, unapolazimisha wajiandikishe kwa mtandao kwa gharama zingine kuacha ile pesa anayolipa Baraza la mitihani, na unapoacha vituo vya mitihani vijipangie bei vyenyewe ni kwamba unawazuia hawa wa.

  Wana JF Naomba michango yenu ya kimawazo.
   
 2. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii bongo bora iuzwe kila raia apewep chake,vinginevyo ha2taelewana
   
 3. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii bongo bora iuzwe kila raia apewe chake,vinginevyo ha2taelewana
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  umeandika km tofar puuu
  ebu andka fresh bwana
  weka paragraf
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,148
  Trophy Points: 280
  Rose nakuunga mkono, wengine huwa wana "point" nzuri tu, tatizo namna ya kuiwakilisha/andika, mpaka inatowa ladha ya kuisoma.
   
 6. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tanzania zaidi ya uijuavyo; mungu atatusaidia.
   
 7. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu ni kweli yawezekana nimeandika bila paragraph lakini kama umeielewa mada naomba mawazo yako maana hapa sikuwa najaribu kuonyesha ni kwa kiwango gani naweza kuandika kiufundi ila kuwasilisha dukuduku langu ambalo najua ni tatizo kwa watu wengi. hilo unalisemeaje?
   
 8. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri wakati umefika inabidi tuwe siriaz na mambo yanayotuumiza kwani suala la kuuza nchi kila mmoja achukue chake si solution ila kupambana na hawa wala nchi ili nchi yetu ibakie kuwa moja lakini yenye mafanikio!!
   
 9. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mfumo wa elimu tanzania unaibua kila kukicha maswali mengi zaidi. Kiukweli kuna mambo mengi yanahitaji mageuzi. Na pia serikali kupitia wizara husika ilipaswa ibebe baadhi ya gharama naamanisha ada za mitihani kama ulizoainisha hapo juu kimsingi zilipaswa ziondolewe kabisa.
   
 10. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu nakubaliana na wewe kuwa serikali kupitia wizara husika iliangalie hilo, Je kama hawa watu wafaidika na mfumo ulivyo unafikiri kweli watakuwa na moyo wa dhati wa kulishughulikia hilo? au kuna njia gani nyingine tunaweza kutumia mimi nafikiri tusisubiri hao watu waone hilo ila sisi tuanzishe majukwaa mbalimbali na kutoa madukuduku yetu! pia jukwaa hili laJF liwe ndiyo kinara cha kuongoza mijadala yetu
   
 11. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hatutakuwa tumesaidia chochote inabidi tukazanie maadili!
   
 12. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbona umeandika essay kwa taarifa iliyotakiwa summary ya maneno mia moja tu na ukaeleweka vizuri. Jitahidi kusummarize mkuu na achana na maneno yasiyohitajika, ni kupoteza muda na nguvu zako.
   
 13. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inabidi watanzania tuangalie alternative nyingine zaidi ya hayo matokeo ya form four or six

  kusema kweli mimi huwa siwaelewi hao wanaorudia mitihani tena kutokea nyumbani ..... ni sawa kwa wale wanaorudia baadhi ya mitihani labda mmoja mpaka mitatu kwa lengo la kupata uwezekano wa kufanya mtihani wa ngazi inayofuatia kama form six tena tayari akiwa shule kidato cha tano

  nasema hivi kwa sababu itawezekana vipi mtu aliyekaa shule miaka 4 kwa elimu ya form four akafanya mitihani 7 (minimum allowed) mpaka 10 (maximum allowed) akafeli masomo3 au zaidi halafu aje akae nyumbani aweze kufaulu masomo hayo hayo kwa kujisomea kwa miezi isiyozidi 6 (hapa inabidi ukate kipindi cha kati ya mtihani aliofanya akafeli mpaka kipindi matokeo hutolewa na kujikuta amefeli ndipo huanza process nzima ya kuhangaikia kurudia mtihani mwaka unaofuatia)
   
 14. t

  toxic JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Iuzwe mara ngapi?
   
 15. z

  zamlock JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hili ni janga la kitaifa
   
 16. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi ku-resit maana yake ni nini? Ni kufanya mtihani kwa mara nyingine baada ya kufeli mara ya kwanza? Kama ni chuo inaitwa september conference nadhani.

  By the way, mtahiniwa anaruhusiwa ku-resit mara ngapi? Nadhani hakuna limit.

  Halafu, umri wa ku-resit mwishi ni mingapi? Pia hakuna limit.

  Itakuaje watu wakataka kurisit kwa miaka mingi tuu? Tena hata baada ya kustaafu kazi? Nani atalipa hiyo gharama?

  Ninaamini tuwe makini sana na ule mtihani wa mara ya kwanza, hapo tuhakikishe kila mtahiniwa anapata fursa na ikiwezekana asilipe gharama yoyote. Ila kama hakuna limitation ya kurudia mitihani, tafadhali wanaorudia walipe hizo gharama.

  Ni mtizamo wangu tuu..
   
 17. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata kwenye vyuo kuna sheria za supplimentary ... uki supp mara kadhaa unadisco.

  I beleave hii mitihani ya NECTA ingetungiwa sheria pia ili kulimit mtahiniwa aweze kurudia mwisho mara kadhaa tuu na ikibidi kkulimit pia umri.

  Cha msingi hapa serikali ishughulikie tatizo la kwa nini wanafunzi wanafeli ili hatimae wasiwe na haja hata ya kurudia mtihani. Hapo tutakua sawa.
   
Loading...