Huu ni wivu au ni msimamo mkali?

Mchili

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
725
46
Mdogo wangu kaniajia ana matatizo katika ndoa yake waliyofunga miaka nane iliyopita. Anasema liwalo na liwe hata kama ni kuvunja ndoa hiyo ivunjike kama mkewe hatafuata utaratibu wake.

Hawa wanandoa wana duka ambalo mkewe ndio anasimamia. Siku za karibuni mkewe ameanza tabia akifunga duka saa 12 jioni anapitia bar na marafiki zake wanapata mbili tatu bia ndio anarudi nyumbani - hata saa tatu mpaka tano usiku. Jamaa amemind na kumtaka aache mtindo huo na bibie nae kaja juu ati yeye sio mtoto mdogo kwani hafanyi chochote kibaya anapokua na marafiki zake. Siku hizi hata akumwambia ampitie wakati wa kurudi nyumbani mkewe hataki hivyo jamaa anahisi mapenzi yamepungua au yamehama.

Sasa jamaa anasema amechoka na tabia hii na anatake achukue hatua yoyote hata kama ndoa itavunjika basi kieleweke kwani haoni raha kuwa na mke asiyempa kampani.

Kabla sijamshauri la kufanya naomba mawazo yenu wana JF, mnaionaje hii ni wivu tu wa jamaa au bibie anaweza kuwa na lake jambo?
 
Mwanamke anarudi saa tano usiku kutoka bar alikokuwa anakunywa na marafiki zake(!?)...Maajabu hayataisha duniani!
 
bar mwanamke mwenye ndoa mppaka sa 5?huyo wa wapi?chakula cha mumewe anapika nani,wanakaa sa ngapi nyumbani na kuongea yaliyojiri mchana kutwa na kuusu biashara inavyoenda?nadhani kuna tatizo but isije ikawa mdogo wako ndo chanzo cha matatizo ebu akueleze ukweli,mind u kila jambo liwe neno au action afanyayo mwanamke inamaana tek it seriously.
 
Mdogo wangu kaniajia ana matatizo katika ndoa yake waliyofunga miaka nane iliyopita. Anasema liwalo na liwe hata kama ni kuvunja ndoa hiyo ivunjike kama mkewe hatafuata utaratibu wake.

Hawa wanandoa wana duka ambalo mkewe ndio anasimamia. Siku za karibuni mkewe ameanza tabia akifunga duka saa 12 jioni anapitia bar na marafiki zake wanapata mbili tatu bia ndio anarudi nyumbani - hata saa tatu mpaka tano usiku. Jamaa amemind na kumtaka aache mtindo huo na bibie nae kaja juu ati yeye sio mtoto mdogo kwani hafanyi chochote kibaya anapokua na marafiki zake. Siku hizi hata akumwambia ampitie wakati wa kurudi nyumbani mkewe hataki hivyo jamaa anahisi mapenzi yamepungua au yamehama.

Sasa jamaa anasema amechoka na tabia hii na anatake achukue hatua yoyote hata kama ndoa itavunjika basi kieleweke kwani haoni raha kuwa na mke asiyempa kampani.

Kabla sijamshauri la kufanya naomba mawazo yenu wana JF, mnaionaje hii ni wivu tu wa jamaa au bibie anaweza kuwa na lake jambo?

Unajua mapenzi ni kati ya watu wawili..unachoweza saidia hapo ni kumsikiliza pia huyo shemeji yako na kujua kama kuna lolote kabla hujachukua hatua ya kumshauri mdogo wako maana unajua tena mapenzi mtu wangu ni kisu...yangu mawazo
 
heshima ni muhimu sana kwenye mahusiano yoyote
sasa kama mama ameanza mambo hayo ya kupita pita na shogaz mmmh napata wasiwasi (hii si tabia ya kike )
anyway wake chini labda wayazungumze mama anaweza kubadilika
kuvunja doa, sasa kama wana watoto tena mbona balaaa!!
 
bar mwanamke mwenye ndoa mppaka sa 5?huyo wa wapi?chakula cha mumewe anapika nani,wanakaa sa ngapi nyumbani na kuongea yaliyojiri mchana kutwa na kuusu biashara inavyoenda?nadhani kuna tatizo but isije ikawa mdogo wako ndo chanzo cha matatizo ebu akueleze ukweli,mind u kila jambo liwe neno au action afanyayo mwanamke inamaana tek it seriously.

mara nyingi we (women) react kulingana na action!!
inawezekana kuna jambo upande wa mume limepelekea mama ku-behave hivi!!
 
thats wat i told himTwin,Huyo jamaa aseme tu ukweli,for the yrs they have been together,we wemen loved deeply there must be somthing wrng with the men,Twin nikikasirika naongea vingereza sana.

Jamaa anafikiri inawezekana kwa vile mama ameanza kushika visenti anapata kiburi. Na hivyo anaona pengine hakuwa na mapenzi ya kweli kwake.
 
8 yrs not mapenzi ya kweli?u must be kidding ww!
Jamaa anafikiri inawezekana kwa vile mama ameanza kushika visenti anapata kiburi. Na hivyo anaona pengine hakuwa na mapenzi ya kweli kwake.
 
Mdogo wangu kaniajia ana matatizo katika ndoa yake waliyofunga miaka nane iliyopita. Anasema liwalo na liwe hata kama ni kuvunja ndoa hiyo ivunjike kama mkewe hatafuata utaratibu wake.

Hawa wanandoa wana duka ambalo mkewe ndio anasimamia. Siku za karibuni mkewe ameanza tabia akifunga duka saa 12 jioni anapitia bar na marafiki zake wanapata mbili tatu bia ndio anarudi nyumbani - hata saa tatu mpaka tano usiku. Jamaa amemind na kumtaka aache mtindo huo na bibie nae kaja juu ati yeye sio mtoto mdogo kwani hafanyi chochote kibaya anapokua na marafiki zake. Siku hizi hata akumwambia ampitie wakati wa kurudi nyumbani mkewe hataki hivyo jamaa anahisi mapenzi yamepungua au yamehama.

Sasa jamaa anasema amechoka na tabia hii na anatake achukue hatua yoyote hata kama ndoa itavunjika basi kieleweke kwani haoni raha kuwa na mke asiyempa kampani.

Kabla sijamshauri la kufanya naomba mawazo yenu wana JF, mnaionaje hii ni wivu tu wa jamaa au bibie anaweza kuwa na lake jambo?

ooh jamani huyu mwanamke anayerudi kwake saa tano kila siku bila ridhaa ya mmewe sidhani kama anafata maadili ya ndoa hata kama kuna ugomvi
panahitaji msaada zaidi kujua makosa yanaanzia wapi......
Palipo na ufa paweze kuzibwa

Hii habari kwangu imenishangaza sana ....mwanamke aliteolewa kurudi home saa tano.. anibilivabo
 
Wanasema ukishangaa ya Musa utaona ya .......
 
mwanamke anae itaka bar kila jioni huyo si nubile type. mara moja moja inaeleweka bar kila siku anatafuta nini?.
 
anajasiria mali na wenzie

Maumivu mengine ya moyo huwa ni makubwa sana. Usikute mwanamke alikuwa housewife, jamaa kajinyima kampa mtaji wa biashara ili kuongeza kipato cha familia. Badala ya kusimamia vema biashara sasa kaona ana pesa, kiburi kimeanza na bia za kila siku juu!

Siku akifilika itabidi huyo mume amtafutie kazi ya u-house girl kwa wahindi ndipo atashika adabu!
 
Maumivu mengine ya moyo huwa ni makubwa sana. Usikute mwanamke alikuwa housewife, jamaa kajinyima kampa mtaji wa biashara ili kuongeza kipato cha familia.
wengine huwa hawalioni hili mpaka wapate wa kuwadunda huko ma bar ndio waelewe umuhimu wa jamaa anaejitoleaga
 
Back
Top Bottom