Huu ni wakati wetu kufanya mabadiliko Tanzania…this is the right political moment..

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Huu ni wakati wetu kufanya mabadiliko…this is the right political moment to bring change to Tanzania!

Tumekuwa tukiona kukua na kumomonyoka kwa maadili ndani ya chama tawala(C.C.M) na Serikali yake toka 1995. Maadili ya chama hiki (CCM)yameanza kuKItafuna chama hiki na wanaccm wenyewe(au kuna mpinzani mla rushwa?).

Tumeshuhudia kila kukicha tuhuma za wabaka uchumi na ufisadi uliokubuu katika kila Nyanja yenye ‘ulaji’. Kulingana na report ya haki za binadamu ya idara ya mambo ya nje ya marekani( U.S. STATE DEPT) ya mwaka 2008, Asilimia 20% ya bajeti ya taifa la Tanzania inabakwa na wala rushwa ( kwa maoni yangu inawezekana ikawa zaidi ya hapo).

Kulingana ha hayo, tumekuwa tukijisahau na kunyoosha vidole, kupiga na kufichua madhambi hayo ya wanaccm (CCM kama wanaushaidi wa watu wa vyama vingine wanaotumiiwa kwa rushwa na wautoe). Sasa napenda kusema wakati ni huu wa kuanza kupanga nini cha kufanya 2010. Tusijisahahu na EPA , DOWANS na yote hayo yanayoendana na hili. Ndiyo twendelee kufichua maovu hayo lakini kubwa watanzania wanaloitaji kwa sasa ni dawa ya kudumu ya kuondoa hili tatizo. Inabidi tuweke mwelekeo wa kulinasua taifa letu ifikapo 2010 na kuendelea.

Shime wanaJF, wakati ni huu, tena wakati muafaka naweza kuita ‘this is the right political moment to change the Tanzania’s profil’ na CCM ndio muda wao kuvuna kile ilichopanda kuanzia mambo ya undeguzanition kwenye ajira, wizi wa mali za umma, rushwa /ufisadi et al. MwanaJF, je wewe unachukua sehemu gani katika kuleta haya mapinduzi ya demokrasia 2010 and beyond? Au ndo tunafuata maneno ya Mwalimu JK kwamba upinzani wa kweli utatoka C.C.M?

Tafakari na chukua hatua katika kujenga taifa letu.

Shadow.
 
Back
Top Bottom