Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Taifa letu tangu limepata uhuru limekuwa likitawaliwa kwa misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi yetu
Ndio maana hatuoni nchi hii ikiendeshwa kwa presidential decrees au ubabe na udikteta.
Tulishuhudia bunge la kumi jinsi lilivyoweza kuiadhibu serikali kwa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wakati huo. Na kila mtu alishangaa kwa namna serikali ilivyowajibika kama ibara ya 53A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inavyosema.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mbunge akifukuzwa uanachama, Mbunge huyo hupoteza uanachama wake. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 67(1)(b). Kwa hiyo Mbunge akifukuzwa uanachama wa chama chake basi hana shavu tena.
Kwa hiyo ili amani kwenye Taifa lolote ili amani itamalaki lazima Katiba ya Taifa hilo iheshimiwe na kusimamiwa.
Hivyo basi Spika wa Bunge letu aheshimu na kusimamia misingi ya katiba yetu. Kama kweli Halima Mdee na wenzake 18 wamefukuzwa uanachama CHADEMA basi sio wabunge halali tena. Watanzania tunaopenda utawala wa sheria tutashangaa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwakingia kifua watu kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.